CHUZI NDIO HILO, HAKUNA KUONJA (12)

Zephiline F Ezekiel
CHUZI NDIO HILO, HAKUNA KUONJA (12)
Jina: CHUZI NDIO HILO, HAKUNA KUONJA Mtunzi: Global Publisher SEHEMU YA KUMI NA TATU ILIPOISHIA... akaondoka zake bila kuaga mtu. Wakati anaondoka, mama Shua alikuwa uani. Alijua mumewe angeenda kuoga lakini alipoona kimya, akaingiwa na wasiwasi, akaenda chumbani na kukuta kiasi cha pesa juu ya meza, JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... lakini baba Shua hakuwepo… “Khaa! Huyu kaenda wapi tena?” alijiuliza. Alimwamsha Shua na kumuuliza lakini alionekana hajui lolote maana alikuwa usingizini. Aliingiwa na wasiwasi kwamba, huenda ameamua yeye ndiyo ahame kwenye nyumba hiyo na kumwacha yeye na Musa wake, lakini alipofungua kabati la nguo hakuona mabadiliko. Wingi wa nguo ulikuwa uleule na haikuwa rahisi kubaini kwamba, mumewe ametoka na begi lenye nguo chache. Hata alipokwenda kwenye sehemu ya viatu alibaini kuwa, ni pea moja tu haipo kwa tafsiri rahisi ni kwamba ndivyo alivyovaa… “Mh! Mimi sijui sasa,” alijisemea m…