Mtunzi: Global Publisher
SEHEMU YA NANE
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
"Poa usitume meseji tena mi ndo natoka"
Poa.
Mama shua aliiweka simu chaji, akatoka kama alivyopanga akaingia bafuni, akaiweka kanga moja ikiwa inaning'inia akaingia chumbani kwa Musa, haraka haraka wakalianzisha sebene.
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
Baba shua alirudi toka dukani na kuingia ndani, alikuta nguo za mama shua akagundua kuwa ameenda kuoga, alipoangalia mezani akaiona simu ya mama shua ikiwa chaji, aliichukua na kuanza kuipekua upande wa meseji, bahati nzuri meseji zote alizifuta, Baba Shua alipokosa meseji yoyote yenye kutia shaka, aliizima, akairudisha simu kwenye chaja kisha akatoka sebuleni. Alikaa akisikiliza maji yanavyomwagika bafuni mkewe akioga lakini hakusikia…
“Mh! Huyu amekwenda bafuni kweli au..?”
Baba Shua wakati ameshtuka hivyo, mama Shua alitoka chumbani kwa Musa haraka. Akanyata mpaka uani, akazama bafuni.
Baba Shua alitoka sebuleni, aketembea, naye kwa kunyata mpaka uani. Akasimama.
Mama Shua alipozama bafuni, alianza kuoga maana alitoka uwanjani, hivyo lazima awe msafi.
Baba Shua aliposikia maji ‘chwaa’ akatingisha kichwa kwa maana ya kukubali…
“Maana usikute mtu kasema anakwenda kuoga kumbe ameingia kwa mwanaume wake,” alisema moyoni baba Shua huku akirudi sebuleni.
Musa alianza kuona njia nyepesi ya kumpata mama Shua… “Kumbe hata kwangu hapahapa nyumbani inawezekana? Sasa kuna haja gani ya kupoteza pesa hotelini?” alijihoji Musa.
“Basi itakuwa nikimhitaji na’mbuku mapema ili ajipange jinsi ya kumpiga chenga mumewe.”
***
Mama Shua aliingia chumbani, akajifuta na kupanda kitandani huku akijifanya hana habari na mumewe.
***
Ilikuwa usiku wa saa saba, baba Shua alishtuka akiwa amelala kuangalia juu au chali. Akamwamsha mke wake …
“Mama Shua…” “Abee,” mama Shua aliitika haraka sana. Ilionekana hata yeye hakuwa amelala usingizi…
“Hivi unajijua kwamba umebadilika nyendo zako?”
“Mimisijabadilika, ila wewe mawazo yako yanasema hivyo.” “Mh! Mawazo yangu yanasema hivyo…ama kweli wanawake mwalimu wenu kipofu! Hivi unadhani wewe uliyekuwa na mimi mwaka jana ndiye nakuona yuleyule wa mwaka huu?”
“Si ndiyo maana nimesema mawazo yako.”
“Mawazo yangu ee? Sawa bwana, mawazo yangu, usiku mwema,” mama Shua alilala zake. Mama Shua hakutaka kunyoosha maneno wala kuweka sawa hali hiyo. Kwake akaona ni sawasawa tu. Alishalewa penzi la Musa.
***
Asubuhi kulikucha, mama Shua kama kawaida yake, anakuaga wa kwanza kutoka uani na binti yake, Shua na kumkuta msichana wa kazi akiwa wa kwanza kutoka kuliko yeyote ndani ya nyumba hiyo.
Baba Shua siku hiyo alichelewa kidogo, wakati mkewe ametoka kuoga, yeye ndiyo akaenda kuoga.
Musa siku hiyo alipotoka, hakukutana na mama Shua wala Shua mwenyewe, ila msichana wa kazi wa mama Shua alikuwa akifagia… “Mchumba wangu yuko wapi?” alimuuliza msichana wa kazi…
“Kaingia ndani na mama yake.”
“A…haa! Kaamka poa lakini?”
“Eee.” ***
Musa ndiye aliyekuwa wa kwanza kufika nje, akawa anavaa viatu tayari kwa kuondoka. Mara akafuata mama Shua. Baba Shua alisimama mlangoni akisikiliza…
“Za asubuhi?” alisalimia Musa…
“Salama, mzima wewe?” “Mimi mzima, naona kumekucha.”
“Eee…ndiyo unaondoka?” aliuliza mama Shua…
“Eee…”
“Nitapata lifti?” mama Shua aliomba lifti huku akiwa hajui kama mume wake anasikiliza… “Itakuaje sasa? Utaeleweka?”
“Ah! Achana naye huyu.”
Baba Shua alimwomba Mungu amsaidie katika kusimamia uvumilivu wake ili asijitokeze akiamini kwamba anaweza kufanya jambo baya kuliko inavyofikiriwa…
“Eee Mungu, nipe uvumilivu kwa ushahidi huu,” alijisemea moyoni baba Shua huku macho yake yakiwa kwa Shua kitandani.
“Teh! Teh! Teh!” alicheka Musa kwa kicheko kile cha ‘da! Jamaa namwibia hivihivi anaona’.
Musa ndiye aliyeanza kutoka, mama Shua akachelewa nje kidogo akijifanya anaweka sawa gauni lake jekundu alilovaa siku hiyo. Baba Shua hakutoka nje, alikwenda kukaa kwenye kitanda na machozi yakaanza kumchuruzika kiasi kwamba alijuta, si kumuoa mwanamke huyo bali hata kukutana naye siku ya kwanza…
“Hivi kumbe ameumbwa hivi? Hakuna haja ya kuelimishana tena, dawa yake ni kuamua kuachana naye tu,” alisema moyoni baba Shua, akasimama, akapiga ishara ya msalaba kifuani kama kuashiria kwamba, anamuachia Mungu.
Kwa upande wake mama Shua, alishangaa kutomwona mumewe akitoka ili kumsindikiza kwa macho kama ilivyo kawaida yake…
“Huyu vipi? Mbona hatoki wakati mimi nataka kuondoka?” alijiuliza mama Shua, akarudi ndani, tena mpaka chumbani… “Mi naondoka,” aliaga Mama Shua huku macho yake yote yakiwa kwenye simu. Aliamini Musa atamtumia meseji.
Baba Shua hakumjibu mkewe, alikaa kitandani. Alikuwa akimuangalia tu!
Ilibidi mama Shua atoke mbio kuwahi lifti huku moyoni akijua kwamba mumewe ana kitu moyoni… “Au jana alijua niliingia chumbani kwa Musa? Lakini hapana, asigeweza kuacha kuniambia. Lakini lazima ana jambo ndani ya moyo wake.”
Mama Shua alipanda gari la Musa huku akiwa hana amani. Pia alipanda kimachale sana akiangalia nyuma. Aliamini mumewe anaweza kutokea ghafla
“Ondoa gari haraka Musa, tunaweza kufuatwa,” alisema mama Shua akifunga mlango na kutulia kama kibaka aliyepakiwa kwenye ‘difenda’. *** Siku hiyo, mama Shua alifanya kazi lakini si kwa kasi ya kawaida. Ilipofika saa saba mchana, meseji ya mama yake mzazi iliingia kwenye simu yake ikiwa imeandikwa… “Najua tabia yako imebadilika, lakini jua kwamba upo kwenye ndoa. Aibu unayoitengeneza, usije kutuletea hapa nyumbani.” Mama Shua jasho jembamba lilimchuruzika. Alihisi amejivua nguo kwa wazazi wake…
“Ina maana mama amejua mimi nachepuka?” alijiuliza mama Shua. Mapigo ya moyo yalibadilika, yakashika kasi. “Musa,” aliita mama Shua… “Naam…” “Mama amenitumia meseji sijapenda…” “Mama mwenye nyumba au?” “Mama yangu mzazi…” “Inasemaje?” Mama Shua aliisoma tena ile meseji ya mama yake mzazi, lakini safari hii kwa sauti ili Musa asikie. Alijiuliza sana mama Shua, nani alimpa mama yake taarifa maana anaishi mkoani. Aliamua kumpigia simu mdogo wake aitwaye Selina ambaye anaishi hukohuko mkoani… “Shikamoo dada…” “Marhaba mdogo wangu….za hapo nyumbani?” “Njema, hajambo Shua?” “Shua hajambo sana…eti nisaidie kitu mdogo wangu… mama kanitumia meseji, anasema nijitambue nipo kwenye ndoa, aibu ninayoitengeneza nisije nikaileta nyumbani…ana maana gani? Baba Shua kaleta habari gani huko?” “Kwani sasa we unavyoona baba Shua anaweza kuleta habari gani kuhusu wewe?” “Sasa mbona unaanza ligi Selina?” “Sianzi ligi bali nimeshangaa sana swali lako.
Wewe kuna mtu kakuona mara mbili unaingia sijui gesti sijui hotelini. Unaingia peke yako kutoka na mwanaume ana gari…huyo ndiye kampigia mama simu jana, akamuuliza ‘yule binti yako Sesilia si bado anaishi na mwanaume yuleyule?’ Mama akajibu ndiyo. Akasema ‘sasa mbona mara mbili namwona akiingia na kutoka hotelini na mwanaume mwingine?’ ndiyo mama juzi na jana presha imepanda,” alisema Selina. Mama Shua palepale alikata simu, akakunjua kiti na kukilaza kwa nyuma, yeye naye akalalia kiti huku akitetemeka… “Oya vipi, kuna nini?” aliuliza Musa macho yakiwa mbele barabarani.
“Kuna soo nyumbani Musa…” “Nyumbani wapi?” Musa aliuliza huku akionekana kupunguza spidi ya kuendesha. Aliamini hilo soo ni nyumbani kwake mama Shua walikotoka hivyo angehitaji kurudi… “Mkoani…” “Kuna soo gani sasa?” Mama Shua alisimulia kila kitu kuhusu meseji ya mama yake na maneno aliyoambiwa na mdogo wake kuhusu wao kuingia hotelini na kutoka… “Daa! Hatari baby…sasa?” “Hata sijui baby…nahisi sasa mambo yatafumka zaidi…” “Una maanisha nini?” “Yalishaanza kufumka kwa mbali…” “Wapi?” “We jua hivyo.” Mara, meseji nyingine ikaingia kutoka kwa mumewe, baba Shua, ilisomeka… “Bado tuna imani na wewe baba Shua lakini kama ukiona mwenendo wa mkeo si mzuri, hafai kuwa mke ruksa kumwacha na hapa kwangu asije-Mama.”
Baada ya meseji hiyo, baba Shua alisindikizia na meseji yake yeye akisema… “Sijamwelewa mama lakini nahisi ujumbe huu wewe umeuelewa ana maana gani na ni kwa nini!” “Musa nishushe hapo please,” alisema mama Shua… “Vipi kwani mambo yamezidi kuwa mabaya?” aliuliza Musa akiwasha indiketa kwenda kushoto ili aegeshe gari… “Ah! Nitakupigia simu baadaye,” alisema mama Shua huku akishuka. Mama Shua alitembea kama mtu aliyelowa maji ya baridi bila ridhaa yake. Hapo alikuwa akikitafuta kituo cha daladala.
Kila aliyekutana naye macho, alihisi anajua yeye ni mchepukaji mpaka wazazi wake mkoani wamejua na kumwambia… “Hii ni kali. Mimi mama Sesilia ndiyo nimefikia hatua hii kweli? Hapana…hapana…iko haja ya kujitafakari upya,” alisema moyoni. Alipanda daladala kuelekea mjini lakini akiwa ndani ya basi, kuna mwanamke mmoja alikuwa akimsimulia mwenzake namna jirani yake mmoja alivyoachika kwa sababu ya uchepukaji… “Yaani mimi nataka nilimshangaa sana yule mwanamke. Yaani unachepuka mpaka unaachwa? Si laana hiyo? Kwanza ni kutojitambua gani huko?” “Si ndiyo walivyo wanawake wa siku hizi. Wanasema kichwani wana akili kumbe wana matope. Wanataka mume akirudi saa nne usiku basi yeye awe amerudi saa nne kasoro dakika saba.”
***
Siku hiyo mama Shua alifanya kazi kama mfanyakazi mgonjwa aliyegomewa ruhusa na mwajiri wake asiende hospitali. Mchana, alijikuta akivutwa na hisia za kumpigia simu mama yake ili amdanganye kutoka kwenye tuhuma zake. Alidhamiria kumwambia kuwa, pale hotelini walikuwa wanatoka kwenye semina tu na mwanaume aliyeonekana naye ni mfanyakazi mwenzake. Alipoona wazo hilo limesimama, akampigia. Simu iliita wee, alipokata tamaa, mama yake akapokea… “Unasemaje?” alipokea mama yake… “Shikamoo baba.” “Marhaba…nakusikiliza…” “Mama nilipokea meseji yako kwamba…” “Mimi siyo mahakama,” alisema mama mtu na kukata simu huku akisikika akisonya.
Mama Shua alibaki ameduwaaa asijue la kufanya kwani majibu ya mama yake yalimpa picha kamili ambayo hakuwahi kuiona hata siku moja. “Loo! Yamenikuta…huyo mzee wa nyumbani aliyeniona hotelini mpaka akapeleka umbeya huu kwa mama sijui nani?” alijiuliza moyoni… “Lakini kwani lazima nikiwa naingia hotelini iwe kwa sababu ya kufanya zinaa? Kwa nini mama asiniulize mimi kwanza halafu jibu langu ndiyo likatoa mwanga wa uamuzi wake?” aliendelea kujiuliza mama Shua, alikosa raha. Pia akakosa amani ya moyo. Palepale akampigia simu mdogo wake, Selina… “Ee dada…” “Selina, ni kwa nini mama anatoa maamuzi bila kuniuliza mimi akasikia nitajibuje?” aliuliza palepale mama Shua… “Kivipi?” “Yeye ananihukumu tu kwa vile kasikia eti nimeonekana nikiingia na kutoka baa… anajua nilifuata nini? Pengine niliingia kuzungumza na mtu je? Hotelini si kunakuaga na ukumbi wa mikutano!”
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi
