Mtunzi: Global Publisher
SEHEMU YA TISA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
“Selina, ni kwa nini mama anatoa maamuzi bila kuniuliza mimi akasikia nitajibuje?” aliuliza palepale mama Shua… “Kivipi?” “Yeye ananihukumu tu kwa vile kasikia eti nimeonekana nikiingia na kutoka baa… anajua nilifuata nini? Pengine niliingia kuzungumza na mtu je? Hotelini si kunakuaga na ukumbi wa mikutano!”
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
“Dada Sesilia….mama akuulize wakati yule mzee amekuwa akikuona ukiingia chumbani na unakaa sana humo! Huo ukumbi upo chumbani dada Sesilia? Unajua mpaka ile presha ya mama ilishuka! Yaani wewe dada Sesilia…mh! Mi mwenyewe sijaamini hata kidogo…yule mzee akasema alikusalimia kwenye korido ukampotezea.” Mama Shua alikata simu. Hakuwa tayari kuendelea kusikia maneno yenye maumivu makali kama hayo… “Mh! Yule mzee akasema alikusalimia kwenye korido ukampotezea’,” mama Shua aliyarejea maelezo ya mdogo wake kiasi kwamba, alitamani ardhi ipasuke.
Alipowaza sana, mama Shua akakumbuka kwamba, ni kweli siku moja akiwa anatoka kwenye hoteli anayokutanaga na Musa, alimwona mzee mmoja ambaye aliachia tabasamu na akamsalimia. Alikumbuka kwamba, sura ya mzee huyo haikuwa ngeni machoni pake lakini aliamini ni wazee wa Jiji la Dar es Salaam ambao wanapenda dogodogo! “Aaaa! Mzee Magunia…yule aliyenisalimia siku ile ni mzee Magunia wa kijijini kwetu…da! Ndiyo maana nilijiuliza huyu mzee mbona kama namfahamu vile! Lo!”
***
Mchana wa saa saba, Musa alimtumia meseji mama Shua… “Haloo…” Mama Shua baada ya kuisoma meseji hiyo alisonya, akasema moyoni… “Ungejua ulivyoniletea matatizo wala usingetuma helo zako.” Musa alipoona hajibiwi na mama Shua aliamua kupigia simu. Iliita weeee! Mpaka ikakatika! Ikaita tena wee mpaka ikakatika… “Khaa! Huyu ana nini sasa?” alijiuliza Musa. Akapiga tena… simu ikaita weee mpaka ikakatika! Akamtumia meseji… “Kuna tatizo baby?” Meseji hiyo haikujibiwa, Musa akasema moyoni kwamba kama angekuwa anapajua ofisini kwa mwanamke huyo angekwenda ili akajue kuna nini kilichotokea! Baada ya nusu saa, baba Shua alimtumia meseji mkewe… “Kama mama amejua uovu wako, ni zaidi sana mimi.
Jua umesimama katikati. Unaweza kuingia au kutoka. Lakini yote hayo yametegemea maono ya moyo wako katika kuamua baya na zuri.” Mama Shua alijikuta akichukia sana, akamjibu… “Unahukumu kama mchungaji au hakimu?” “Kama wote…” “Ungechunguza kwanza kabla ya kusema…” “Namshukuru Mungu nimechunguziwa na mama yako.” “Niache tafadhali…nataka niendelee na maisha yangu…” “Uachwe mara ngapi?” “Basi hakuna haja ya meseji zako,” alisema mama Shua. Lakini naye akawa hajui mumewe amemwacha kwa maana gani? Kwamba hamtumii tena meseji… hamfuatifuati na mambo yake au anamwacha kwa maana ndoa basi tena! Kweli, baba Shua hakutuma tena meseji kwa mama Shua kiasi kwamba, mwanamke huyo alichanganyikiwa.
***
Muda wa kutoka kazini ulifika, mama Shua alitamani siku hiyo asirudi nyumbani kwake kwa mambo yaliyotokea. Alijisikia kulalalala mahali mpaka saa mbili usiku au tatu ndipo arudi nyumbani. Lakini kama angekwenda kulala mahali, angekuwa na nani? Maana kuwa peke yake pia ilikuwa tatizo, mawazo yangekuwa palepale. Alihitaji kampani, tena ya mwanaume. Ilibidi amkumbuke Musa. Aliaga wenzake akatoka, nje akampigia simu Musa… “Uko wapi baby?” “Niko baa…we si unasikia kelele hapa!” “Baa wapi?” “Posta.” “Tunaweza kuonana?” “Wapi?” ”Wapi! Si kule mahali kwetu!” “Saa ngapi?” “Mimi ndiyo nimetoka, naelekea.” “Oke, nakuja.” “Please, usichelewe baby.” Mama Shua alichukua usafiri, ukampeleka hadi kwenye hoteli hiyo.
Alishuka, akamalizana na mwenye usafiri, akatembea mpaka mapokezi. Alilipia chumba yeye mwenyewe, akapelekwa chumbani. Alikuwa ameshavua nguo, amejifunga taulo tu na alilala kitandani simu ikiwa mkononi akianza kuchati. Kwanza kabisa alimtumia meseji mumewe… “Natoka kazini napitia kwa rafiki yangu Rukia… kuna ishu ya kuzungumza naye…” Hakujibiwa meseji hiyo lakini yeye hakujali, akamgeukia Musa… “Mimi nimeshafika, wewe uko wapi baby?” “Nakaribia baby,” alijibu Musa. Mara, ikaingia meseji nyingine. Hii ilitoka kwa mama yake kijijini… “Kwa hiyo hiyo hoteli ndiyo umeigeuza nyumbani kwako sasa??!!”.
Mama Shua alijikuta akiingia wasiwasi, akatoka kwa kasi huku macho pima… “Mungu wangu…Mungu wangu. Yule mzee kaniona tena jamani, kamtumia mama meseji,” alisema moyoni mama Shua huku akiseti simu yake ili ampigie mdogo wake… “Selina, mama kanitumia ujumbe tena. Inaonekana yule mzee ameniona tena. Mimi nilikuja hapa kuonana na mwanamke mwenzangu, wala si Musa…” “Musa ni nani kwani dada?” mdogo wake alimuuliza. “Ha! Nilikosea.” Mama Shua alikata simu, akatoka hadi nje kabisa na kusimamisha teksi tayari kwa kurudi nyumbani kwake.
“Hivi yule mzee ananitafuta nini mimi? Ana maana gani kunifuatilia kiasi hiki?” alijiuliza akiwa anapanda kwenye gari hilo. Alisahau kabisa kumpigia simu Musa kumjulisha mpaka Musa alipopiga yeye… “Uko wapi baby?” “Ah! Baby nimepata dharura bwana, nimeondoka. Please tukutane kesho baby au nyumbani nitakwambia.” “He! Dharura gani mpaka unafikia hatua ya kuondoka bila kuniambia mapema. Mimi nimeingia mpaka hotelini sasa.” “Sikia Musa, twende kwingine tukatafute hoteli nyingine.” “Kama wapi?” “Popote pale lakini si hapo,” alisema mama Shua na kukata simu ili asome meseji ambayo iliingia wakati anaongea na Musa…
“Umeona aibu kuingia hotelini na kuamua kuondoka siyo? Ungeingia tu. We mtoto huo mwenendo wako kama utaendelea kuwa hivyo sijui kama utadumu kwenye ndoa,” ni ujumbe uliotoka kwa mama yake. Mama Shua aliishiwa nguvu kabisa kiasi kwamba alitamani ardhi ipasuke sasa ili afie humo. Mara, Musa akampigia simu… “Haloo Musa…” “Ee, sasa sikia. Nakwenda Makumbusho, tukutane kule,” alisema Musa… “Sawa. Sehemu gani?” “Pale baa. Lakini tukitoka pale tunakwenda gesti, sawa?” “Sawa baby.” Mama Shua alihisi mwili unamsisimka kwa maneno ya Musa, akajikuta anaachana na wazo la kwenda nyumbani. Akamwambia dereva ampeleke Makumbusho. Alifika Makumbusho, akashuka.
Akatembea hadi kwenye baa hiyo lakini hakumkuta Musa, akampigia simu. “Uko wapi sasa, mbona hapa baa haupo?” “Nilikuja kuchukua chumba huku gesti.” “Wapi nije?” Musa alimwelekeza mama Shua. Wakati anakwenda, njiani mama Shua alikasirika sana kuhusu yule mzee na mama yake hivyo akaamua moyoni kwamba akikutana na Musa ampe mahaba mazito kama kulipa kisasi kwa mama yake na yule mzee. Mama Shua aliingia, akapita kwenye korido mpaka kwenye chumba kwa mujibu wa maelekezo ya Musa. Akazama ndani.
Ile anafika tu, akiwa bado amesimama alimkumbatia Musa na kumpiga mabusu kibao, mara akaomba denda, wakazama kwenye denda kwa muda wa kama dakika tano nzima huku wakitoa miguno ya mmmh …mmmh! Mama Shua, wakiwa bado wamesimama, akapeleka mkono kwenye suruali ya Musa na kuanza kumfungua kizuio chake kisha akamshusha suruali hadi chini. Baada ya hapo akamvua shati, mara akamvua singilendi mpaka Musa akabaki mweupe. Musa naye kuona hivyo, akaanza na yeye mpaka mama Shua akabaki mweupe kama yeye. Wote wakabaki weupe, wakapanda kitandani. Mama Shua alikuwa akihema sana hivyo kumfanya Musa naye kuambukizwa na mhemo wake, hawakuchukua muda wakaingia kwenye uwanja na kuanza kucheza.
Mama Musa huku akijua kwamba Musa atafika haraka safari yake ilibidi aanze kumsemesha… “Unajua mwenzako nina msala…” “Msala gani?” “Mama angu amejua mimi ninaingia hotelini pale. Kuna mtu ananionaga. Sasa leo pia kaniona. Akamwambia mama, mama akanitumia meseji nzito sana. Yaani jamani.” “Mh! Kwa hiyo?” “Kwa hiyo nini sasa. Nilitaka kwenda nyumbani lakini nikajua wewe utakwenda pale na wanawake zako.” “Umeanza baby. Kwa nini tusisubiri tumalize ndiyo uanze kunishutumu?” “Hakuna bwana, we unapenda sana wanawake. Mi unanikera sana ujue.” “Uliwahi kuniona na mwanamke wapi?” “Najua tu. We endelea.” Ilifika dakika ya kumi siku hiyo, mama Shua ndiyo aliyeanza kutangaza nia kwa Musa ikabidi Musa naye ahemuke na kutangaza na yeye wakafika mwisho wa mchezo.
***
Waliendelea kulala humo chumbani huku mama Shua akimtekenyatekenya Musa mpaka Musa akawa ngangari tena. Wakaingia tena uwanjani. Safari hii, mama Shua alimsemesha sana Musa maneno ya kila aina… “Siku nikikuona na mwanamke mwingine Musa utanijua mimi ni nani!” “Kivipi?” “Nitakufanyia fujo hata mbele za watu mimi sitajali ujue… ohooo.” “Haitatokea.” “Haitatokea kwa sababu unajificha sana si ndiyo?” “Hamna,” alisema Musa hapohapo akatangaza nia.
***
Mama Shua aliingia nyumbani akijifanya mnyonge kwamba, hajisikii vizuri maana alimkuta mume wake amesharudi na amekaa sebuleni. Lakini mumewe hakumuuliza mbona mnyonge, alimwangalia tu. “Hivi baba Shua mimi naumwa hata kuniuliza hutaki? Hayo ni mapenzi gani lakini? Ina maana wewe uumwe mimi nikae kimya nakuangalia tu utajisikiaje?” “Kama unaumwa si ungeenda hospitali?” “Kwani sijaenda?” “Pale gesti Makumbusho ndiyo hospitali?”
Mama Shua alishtuka sana kumsikia mumewe akisema hivyo, akajikuta anamtumbulia macho.
Kusema amuulize kama alimwona alishindwa kwani alijua lazima mumewe amemwona akiingia au akitoka kwenye gesti hiyo ya Makumbusho…
“Au kama hajaniona yeye kuna mtu amemwambia,” alisema moyoni mama Shua huku akiwa na uso wa aibu…
“Da! Nimeumbuka hivihivi…yaani hapa napotea huku najiona,” mama Shua aliendelea kusema moyoni na kuingia chumbani huku miguu yake ikikosa nguvu ya kutembea…
“Hizi salam zikifika kwa mama ndiyo tabu,” aliendelea kusema moyoni mama Shua huku akilitupa begi lake chini.
Jambo lililomshangaza sana ni kuona mumewe amelichukulia suala la yeye kuingia gesti Makumbusho kama utani…
“Ina maana awe ameniona au ameambiwa halafu aniulize kirahisi vile? Haiwezekani,” alisema moyoni.
Baba Shua aliendelea kukaa sebuleni bila kumfuata mumewe chumbani, alikuwa akiwaza…
“Huyu dawa yake ni moja tu. Ni kumtema. Nikisema nimvumilie nitakufa kwa presha. Hivi kwa nini ananifanya mimi mtoto mdogo? Atakapokuwa mbali na mimi ndiyo atajua umuhimu wa kuheshimu ndoa yake.”
***
Kule chumbani, mama Shua alikaa kitandani akiendelea kuwaza na kujiuliza maswali kadhaa kichwani…
“Na kama aliniona yeye mwenyewe si ina maana aliniona nikiwa na Musa? Da! Nimeumbuka kwelikweli.”
***
Musa naye alikuwa chumbani kwake. Alihisi joto la mahaba, akatamani amwite mama Shua walicheze libeneke ili alale usingizi mnono. Akamtumia meseji…
“Baby.”
Mama Shua hakuchukua muda kuijibu meseji hiyo, tena kwa haraka sana…
“Niambie baby! Siko poa sana.”
“Pole baby, unaumwa?”
“Hapana… basi tu.”
“Sasa si uje, nimekumisi sana.”
“Da! Musa bwana…unanipa majaribu ujue.”
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi
