CHUZI NDIO HILO, HAKUNA KUONJA (9)
Jina: CHUZI NDIO HILO, HAKUNA KUONJA Mtunzi: Global Publisher SEHEMU YA TISA ILIPOISHIA... “ Selina , ni kwa nini mama anatoa maamuzi bila kuniuliza mimi akasikia nitajibuje?” aliuliza palepale mama Shua … “Kivipi?” “Yeye ananihukumu tu kwa vile kasikia eti nimeonekana nikiingia na kutoka baa… anajua nilifuata nini? Pengine niliingia kuzungumza na mtu je? Hotelini si kunakuaga na ukumbi wa mikutano!” JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... “ Dada Sesilia ….mama akuulize wakati yule mzee amekuwa akikuona ukiingia chumbani na unakaa sana humo! Huo ukumbi upo chumbani dada Sesilia? Unajua mpaka ile presha ya mama ilishuka! Yaani wewe dada Sesilia…mh! Mi mwenyewe sijaamini hata kidogo…yule mzee akasema alikusalimia kwenye korido ukampotezea.” Mama Shua alikata simu. Hakuwa tayari kuendelea kusikia maneno yenye maumivu makali kama hayo… “Mh! Yule mzee akasema alikusalimia kwenye korido ukampotezea’,” mama Shua aliyarej…