
Mtunzi: Richard Mwambe
SEHEMU YA KUMI NA TATU
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
akachukua bastola zake pale mlangoni nakuiendea lift iliyompandisha hadi juu na kutoka mlango mkubwa wa hoteli. Katika maegesho ya magari alimuona Amata akiwa na yule mwanamke, sasa ilionekana wazi kuwa mapenzi yanachukua nafasi yake, akajifanya anapiga simu, ili kupoteza muda ajue kitachoendelea.
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
Muda si mrefu, ikasimama gari pembeni yao, Jeep Cherokee ya kibuluu hivi, yule mwanamke akamvutia ndani Amata na gari ile ikatoweka. Melchior alitazama hapa na pale na kuona gari nyingi zilizokuwa zimeegeshwa na wamiliki wake walikuwa wakila starehe ndani ya hoteli ile, akaiendea moja wapo, Toyota Celica, akatoa funguo yake, wengi huiita Malaya, funguo inayoweza kufungua takribani lock zaidi elfu kumi za magari bila shida achana na switch zake.
Alizungusha mara mbili tu mult lock zikaachia akaingia nyuma ya usukani na kulitekenya nalo likacheka, taratibu akaingia barabarani na kuifuata ile Jeep Cherokee, alikanyaga mafuta na kuhakikisha haiachi mbali gari ile, kati yake aliacha gari kama mbili hivi na kuendelea kuifuata, baada ya barabara tatu nne na vichochoro kadhaa ilianza kuuacha mji na kuchukua barabara ya kuelekea Thika, Melchior aliendelea kuwafuata na walipokaribia maeneo ya Kalimoni, akaona hapana, akaongeza mwendo na kuifikia ile Jeep, akaipita na kukaa mbele yao.
Kila dereva wa ile jeep alipoijitahidi kuipita ile gari ya Ndege haikuwa rahisi, Melchior akaongeza kasi na kuiacha kama mita ishirini hivi kisha akafunga breki kali sana na ile jeep ilikuja na kuigonga ile Toyota kwa nyuma, kutoka katika ile jeep, mtu mmoja akateremka na kuifuata ile Toyota akaangalia ndani lakini hakuona dalili ya mtu, alitazama huku na kulea asione kitu, akarudi garini mwake na kuingia, alipofunga mlango tu alihisi kitu cha baridi kikigusa shingo yake, “Tulia hivyohivyo,” sauti ilimwambia, kisha Ndege akaunyoosha mkono wake na kuichomoa bastola ya yule dereva, wakati huo tayari kipigo cha haraka kilishampa usingizi wa muda yule mwanamke aliykuwa na Amata, “Toa gari barabarani, weak kando ile,”
Melchior Ndege aliamuru na amri ikafuatwa, mbele kabla ya mahali alipoambiwa aiegeshe gari ile palikuwa na daraja kubwa sana la mpishano wa barabara, wao sasa walikuwa barabara ya juu, yule dereva akafanya hila kwa kugongesha ile gari katika ukingo wa daraja, ile gari ikayumba kidogo, Melchior, mle ndani ya gari akaangukia upande wa pili na kumpa nafasi yule dereva kufanya lolote, lakini kabla hajafanya hivyo, maana Melchior alimuona akichomoa bastola nyingine sehemu Fulani ya dashboard yake, kitendo bila kuchelewa, kwa kutumia miguu yake miwili alimbana kabali njema, gari iliyumba lakini Melchior hakujali, mara akasikia kishindo kikubwa, ile gari ilijipiga kwenye ukingo wa daraja, ikahamia upande wa pili ikakutana na Toyota prado na kujibamiza kisha akaangukia nje ya barabara.
Kamanda Amata akiwa hajui lolote linaloendelea kutokana na usingizi mzito alioulala mara tu baada ya kuingia mle garini, alijigonga kichwa kwenye muhimo wa dirisha, akshtuka na kuanza kushangaashangaa, huku damu zikimtiririka kutoka kwenye jeraha dogo lililotokea katika kichwa chake baada ya kujigonga kule.
Melchior alitoka kwa shida kidogo katika gari ile baada ya kuvunja kioo cha mbele, kisha akamsaidia Kamanda Amata kutoka nje, bado Kamanda alikuwa hajarudiwa na akili sawasawa alikuwa kama zezeta hivi, Melchior akamshika mkono na kutembea nae kuelekea pale alipoiacha ile gari alioichukua kule hotelini, aliwakuta polisi wawili akiitazama ile gari huku wakiwa na wanaandikaandika vitu Fulani wakisaidiwa na taa za barabarani. Melchior aliufungua mlango wa mbele na kumtumbukiza Kamanda kiti cha kushoto kisha yeye akazunguka kiti cha kulia, “Halo, vipi, mbona unakuwa kama hauheshimu mamlaka?” mmoja wa wale askari akauliza, Melchior akawasha gari huku akimwangalia yule askari, “Nenda pale karibu na njia panda utakuta ajali ya gari aina ya Jeep Cherokee, hiyo ndiyo ukaipime, hii sio ajali,” kisha akaondoka kwa kasi mpaka kwenye mzunguko mkubwa na kuhama njia kuchukua njia inayorudi mjini, kwa mwendo uleule wa kasi ya ajabu.
Melchior ndege aliegesha gari katika lango la hospitali ile na daktari mmoja alikuwa pale tayari na kitannda cha magurudumu, akisaidiwa na manesi wawilli walimlaza kamnda Amata na kuingia naye ndani, moja kwa moja wakamuweka kitandani kwemye chumba cha peke yake, wodi maalumu, daktari alipomuangalia vizuri aliona wazi hali yake si nzuri, hivyo akaamuru awekewe drip ya glucose ili iweze kumrejeshea nguvu japo kidogo. Wale wauguzi wakafanya hivyo lakini pia walicheki mapigo ya moyo na kuweka kumbukumnbu zake kati faili maalumu lililokuwa pale, Kamanda Amata alilala kimya akiwa hajitambui tena, jeraha lake lilishonwa na kuwekwa katika hali ya usafi.
Melchior Ndege, alipekuwa kwenye mifuko ya Amata lakini hakuona chochote, akabaki kumtazama pale kitandani alipozungukwa na mitambo tiba ya kisasa ambayo ilikuwa inaangalia mwenendo wa mwili kwa ujumla kama mapigo ya moyo na mambo mengine. Melchior Ndege alitoka nje na kufunga mlango mkubwa kioo kisha kurudi ofisini kwa daktari.
“Rafiki yako inaonekana amepewa sumu kali sana ambayo imempotezea fahamu na kuathiri mfumo wa urendaji kazi wa mwili wake, itamchukua masaa mengi sana kuirudia hali yake ya kawaida,” Daktari alimweleza Melchior Ndege, haikuwa rahisi kulielewa swala hilo, lakini aligundua kuwa Bill alidhamiria kummaliza Amata. Akashusa pumzi ndefu na kumtazama daktari.
“Huyu ni mtu wetu, katoka Tanzania,” akamwambia kwa kifupi, daktari akatikisa kichwa kuashiria kuwa ameelewa, kisha Melchior akampa habari nzima jinsi alivyomuona kuanzia pale hotel ya Safari park mpaka kule kwenye ajali.
Hasira zilizidi kumtawala Melchior na moyoni akaapa lazima Bill alipe yote ayafanyayo, hapo akagundua kuwa Bill ni jasusi la kimataifa lenye mbinu za kuua bila kutumia silaha na kuwafanya watu kutojua ni nini chanzo cha kifo. Aliagana na daktari na kuomba kurudi baadaye kidogo lakini apewe taarifa ya kila kinachoendelea.
Safari yake na gari ile ya kukodi iliishia katika mtaa wa Riara, akashuka na kuilipa tax hiyo kisha akaliendea geti kubwa jeusi lilofungwa sawia, akabofya kengele, mara likafunguka naye akajitoma ndani, “Karibu sana kijana!” alikaribishwa na sauti ya boss wake bwana Shikuku, “Vipi mbona usiku sana ?” akaongeza swali, ndipo Melchior alipoinua mkono wake kuitazama ile saa yake iliyomuonesha kuwa ni saa nane kasoro robo usiku. Wakaingia sebuleni na kuzungumza machache, Melchior alimpa habari yote ya Kamanda Amata. Shikuku alisikitishwa sana na habari hiyo, kisha wote wawili usiku huo wakatoka na kuelekea kule hospitali kumuona Kamanda, walimkuta katika hali ileile isipokuwa sasa ilikuwa mbaya zaidi kwani mapigo ua moyo yalishuka sana, hata daktari alikuwa na wasi wasi juu ya hilo maana hayakuonekana kupata unafuu wowote.
“Shiiiittt!!!!” aliinua simu yake na kubofya namba Fulani kisha kusikiliza sauti ya upande wa pili, baada ya mazungumzo mafupi aliikata na kuiweka mezani, akajishika kichwa kwa masikitiko, mara simu yake ikapata uhai na kujitikisatikisa pale mezani, aliinyakuwa na kusikiliza, “Yeah… ndiyo… ee. Fanyeni haraka tafadhali,” akakata simu na kuitia mfukoni.
“Vipi, ni nani hao?” Ndge alimuuliza bosi wake.
“Nilikuwa nawapa taarifa juu ya mtu wao huko Tanzania, ili wajue ni nini watafanya, sasa wamesema wayanijibu haraka iwezekanavyo,” Shikuku alijibu.
“Hivi Bill amedhamiria haswa kufanya mauaji ya mtindo huu sivyo?” Ndege alimuuliza Shikuku.
“Yule ni shetani, sio binadamu, hivi umesema yuko wapi saa hii?” Shikuku aliuliza swali kwa Ndege.
“Niliwaacha, Safari Park casino, lakini sidhani kama bado wako hapo, ngoja tufatilie wale watu wa kwenye ile gari ili tujue kwa undani juu ya sakata hili na nini kipo nyuma yake, simpendi kabisa Bill, na aombe Kamnda Amata asiamke milele, lakini Shikuku nakuhakikishia, Kamnda akiamka atavunja mpaka miiko ya kazi yake ili amtafute huyu hayawani na kwanza atamuua kisha amuulize maswali anayoyataka,” melchior Ndege aliongea kwa hasira na kutoka nje ya chumba cha daktari.
Mkono wa bwana Shikuku ulimshika bega Melchior Ndege pale alipokuwa ameegemea ukuta akiwa amewaka hasira zilizojaa uchungu.
“Malchior, punguza jazba, pamoja na FBI kuwa hapa, isiturudishe nyuma, ingia kazini, mimi nakuamuru, kama kuna swali mi nitajibu; Kamanda atapona tu, najua walimuwahi katika namna ambayo hakuitegemea,” yalikuwa ni maneno ya Shikuku kwa Melchior, akageuka kumtazama mtu huyo mwenye mwili mkubwa, mkuu wa idara ya usalama wa Taifa hapo Kenya, Melchior alitabasamu kwa bashasha baada ya kuambiwa ‘Ingia kazini’, alitoka pale alipo na kuelekea tena chumba cha daktari kisha akaingia kumuona Kamanda, alimutoa alama ya saluti ya heshima, na kumuhakikishia Kamnda kuwa sasa analipiza kisasi kwa ajili yake, kishapo akatoka nje na kuagana na Shikuku.
˜˜˜
Saa 9:15 Usiku
KELELE za simu ya mezani ya Madam S ilipiga kelele usiku huo, mlio wa dharula ulimshtua kutoka katika usingizi mzito, “Aaaa nini tena saa hizi?” aliongea kwa sauti ya hasira na kuinyakua ile simu masikioni mwake, “Hallo nini saa hii?” aliipokea na kutupa swali hilo; huku akisikiliza sauti ya upande wa pili, “Madam, kuna taarifa kutoka Nairobi kuhusu Kamanda Amata, hali yake ni mbaya sana yuko kufani,” sauti hiyo iliongea kwa upole, ilikuwa ni simu kutoka ofisi ya usalama wa Taifa ikimpa taarifa hiyo Madam, mkuu wa kitengo maalum chenye watu wachache makini wanaofanya kazi za umakini kwa umakini wa kimakini. Aliishika ile simu bila kuongea.
“Unasemaje?” akauliza, akajibiwa tena jibu lilelile. Madam S alishikwa na kigugumizi, midomo ilimchezacheza, hakuamini anachoambiwa, ni jana tu mchana alipoagana na Kamanda wake pale JNIA na kumpa usia wa nguvu, Madam alibaki kimya na simu ikiwa hewani nab ado hajaishusha kutoka sikioni mwake, akashusha pumzi kisha akafungua kinywa chake, “OK, asante kwa taarifa, fanya kila kinachowezekana Kamanda afike hapa mara moja,” akakata simu na kurudisha mkono wake mahali pake, “Uuuuhhhhh!!!!” akashusha pumzi nzito kwa mara nyingine, akajilaza kitandani kwake huku mawazo lukuki yakiwa yamemtawala kichwani mwake. Akafikiri la kufanya na kumpigia daktari wao pale Muhimbili, ushauri aliopewa aliuona una maana sana, yule daktari alimshauri ikodiwe ndege ya haraka kutoka Nairobi imlete Dar, badala ya kukodi kutoka Dar.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi