MAUAJI YA KASISI (13)
Jina: MAUAJI YA KASISI Mtunzi: Richard Mwambe SEHEMU YA KUMI NA TATU ILIPOISHIA... akachukua bastola zake pale mlangoni nakuiendea lift iliyompandisha hadi juu na kutoka mlango mkubwa wa hoteli. Katika maegesho ya magari alimuona Amata akiwa na yule mwanamke, sasa ilionekana wazi kuwa mapenzi yanachukua nafasi yake, akajifanya anapiga simu, ili kupoteza muda ajue kitachoendelea. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Muda si mrefu, ikasimama gari pembeni yao, Jeep Cherokee ya kibuluu hivi, yule mwanamke akamvutia ndani Amata na gari ile ikatoweka. Melchior alitazama hapa na pale na kuona gari nyingi zilizokuwa zimeegeshwa na wamiliki wake walikuwa wakila starehe ndani ya hoteli ile, akaiendea moja wapo, Toyota Celica, akatoa funguo yake, wengi huiita Malaya, funguo inayoweza kufungua takribani lock zaidi elfu kumi za magari bila shida achana na switch zake. Alizungusha mara mbili tu mult lock zikaachia akaing…