MAUAJI YA KASISI (14)
Jina: MAUAJI YA KASISI Mtunzi: Richard Mwambe SEHEMU YA KUMI NA NNE ILIPOISHIA... “Uuuuhhhhh!!!!” akashusha pumzi nzito kwa mara nyingine, akajilaza kitandani kwake huku mawazo lukuki yakiwa yamemtawala kichwani mwake. Akafikiri la kufanya na kumpigia daktari wao pale Muhimbili , ushauri aliopewa aliuona una maana sana, yule daktari alimshauri ikodiwe ndege ya haraka kutoka Nairobi imlete Dar, badala ya kukodi kutoka Dar. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Utaratibu ukaandaliwa haraka kwa ushirikiano na Bwana Shikuku kule Kenya. Usingizi haukuja tena kwa Madam S, akaifungua kompyuta yake ya kazini ambayo imeunganishwa moja kwa moja katika kitanda chake, alipojaribu kuingiza password yake, ikagoma, haikufunguhka, akajaribu tena na tena, wapi. Alipoona imeshindikana, akampigia simu Chiba , mtaalamu wa ICT wa kitengo chao, naye akajaribu kuifungua lakini ikawa ngumu, akatumia mbinu zote kuitafuta maana alisha…