
Mtunzi: Richard Mwambe
SEHEMU YA KUMI NA SABA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
ninyi mnatazama mauaji ya Fr Gichuru, na kumsaka muuaji na monstrance iliyopotea, lakini hali sivyo ilivyo, kwa uwezo wenu nyie lazima mtaishia katikati kwani katika kesi hiyo kuna mkono wa kimataifa, mkono nambao pambano lake lazima liwe la kimataifa vilevile,”
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
kabla hajaendelea, sergeant Maria alimkatisha, “Unasemaje wewe?” Yule kijana akarudia kumwambia yale yote aliyokwisha sema, “Mimi nilishuhudia Fr Gichuru alivyotekwa, alivyofungwa na kupewa mateso makali, lakini usiku huo akatoweka pale alipofungwa, nilikuwa mlinzi katika godown moja ambalo huyo marehemu alifungwa, na tulipata shida sana baada ya kutoweka kwake, na wale waliomteka waliapa kumuua pindi tu watakapomuona, na ndivyo ilivyokuwa”
Sasa sergeant Maria alionekana kuvutiwa na simulizi hii tamu ambayo iliifanya damu yake kuchemka kikazi, “Nambie kwa nini unasema ya kimataifa?” akamuuliza.
“Nasema ya kimataifa kwa kuwa kati ya watu waliomleta kulikuwa na bosi wao ambaye kwa mazungumzo yao ya harakaharaka anatoka nje ya nchi na ndiye aliyewatuma hawa majambazi na aliwaahidi pesa nyingi sana,” Yule kijana akaeleza. Sergeant Maria akavuta kumbukumbu na kukumbuka kuwa walipoikuta maiti ya Cheetah kulikuwa na burungutu la hela, hela nyingi kuliko unavyofikiria zikiwa zimetupwa juu ya mwili huo, akatikisa kichwa juu chini kuonesha kuwa ameliafiki hilo.
“Ok, hebu nambie, hao waliomleta au kumteka hasahasa walikuwa wanataka nini kwake?” Maria alitupa swali linguine.
“Walikuwa wanadai awaoneshe monstrance, lakini yeye alikataa kata kata ndiyo maana walimtesa sana hata kuzimia mara nyingi kwa kipigo,” Yule kijana alijibu.
“Na alitoweka vipi?” Maria aliuliza, huku akindiki vitu Fulani katika kijitabu chake.
“Hapo ndipo utata unapojitokeza, maana asubuhi mimi na mwenzangu tulipoenda kumtazama hatukumkuta, lakini miongoni mwetu mlinzi mmoja pia hakuonekana mpaka baada ya siku mbili tulipogundua mwili wake katika pipa la takataka ukiwa hauna uhai, tukateswa sana tuseme ni wapi ametorokea mateka wao lakini hatukujua, ndipo name nilipotoroka na kujificha huko Korogocho, najua kuwa sakata hili halijaisha ipo siku hata mi nitakuwa mikononi mwa wanaharamu wale, najua wataniua kwani ninalijua hili, nikaapa kumtafuta Yule atakayekuwa ameishika kesi hii ndipo nilipojua ni wewe nikakutafuta,” Yule kijana alimaliza maelezo yake.
“Sasa wewe unanisaidiaje katika hili?” sergeant Maria aliuliza.
“Sina msaada afande zaidi ni kukuambia tu, usiumize kichwa, ukilifuatilia hili hakika utakufa, waache wakubwa wafanye yao,” Yule kijana sasa aliongea kwa msisitizo kidogo. Sergeant Maria alikuwa akimuangalia kwa kugeuzageuza kichwa chake kana kwamba haelewi analoambiwa, akainama chini kufikiri kitu Fulani alipoiunua kichwa chake kumtazama Yule mtu, hakumuona pale alipokaa, badala yake kiti kile kilikuwa kimekaliwa na askari mwingine wa kike, wakasaliamiana lakini Mria alionekana kuchanganyikiwa kwa hilo, “Afande, aliyekaa hapa yuko wapi?” aliuliza. “Mbona hapa hapakuwa na mtu afande!” lile jibu likazidi kumdidimiza katia shimo la mawazo, akanyanyuka haraka na kutoka nje ya mgahawa huo, akatazama huku na huku asione mtu, akazunguka upande wa pili hali hiyo hiyo, akajishika kiuno na kufikiria mara mbili kama alikuwa amekaa na mzimu au binadamu wa kweli. Lakini katia yote hayo bado hali ilikuwa ileile kuwa Yule mtu hayupo pale.
˜˜˜
“Baby, mbona hivyo? Unaniumiza mwenzio, umenitafuta usiku wenye baridi kali nije nikuliwaze lakini tuko kitandani, mwenzangu huoneshi ushirikiano, mmm sweet nambie shida nini?” Kahaba Rose alikuwa akinung’unika kitandani alipokuwa amelala na Kamanda Amata usiku huo, baada ya Amata kumtafuta kahaba huyo kati viunga vyote vya mji wa Nairobi, ndipo alipoambiwa na mmoja wa makahaba katika mtaa wa Koinange kuwa Rose alipata ‘Big Deal’ hivyo ni siku kadhaa hayupo barabarani, lakini kwa msaada walimuelekeza wapi anaishia naye kamanda akamfungia safari mpaka nyumbani kwake na kumkuta, akamchukua na kumueleza shida yake kuwa anataka huduma yake usiku huo, kwa kuwa Rose alikuwa hana kaziingine usiku huo alikubaliana naye na kutoka mpaka kwenye hoteli moja isiyo na jina katika mitaa ya Mathare na kuchukua chumba hapo. Kamanda Amata hakutaka penzi la kahaba huyo bali alikuwa na yake moyoni, alimtazama Yule kahaba na kutingisha kichwa, alikuwa mwanamke mzuri wa sura, mtamu wa umbo, mwenye miguu minene ya kuridhisha, hips zilizojaa, macho ambayo yakikutazama utaona jinsi mwili wako unavyolegea mbele yake, hakika alikuwa mrembo.
“Sikia mrembo,” Amata alinguruma, “Yes Baby,” Rose alijibu huku akijisogeza na kujilaza juu ya kifua cha Amata, “nimekutafuta sana leo siku ya saba, ulikuwa wapi? Maana sifa za urembo wako zimenifikia nikiwa Kongo,” uongo ukaanza kuchukua nafasi, Rose akatabasamu na vibonyo viwili vikajitokeza katika mashavu yake.
“Nilipata kazi ya wiki mbili kwa tajiri mmoja wa kizungu, ana pesa kama matundu ya neti, lakini hatujamaliza kazi yetu, simuoni tangu juzi na simu zake hazipatikani, kwangu si shida maadamu kanilipa parefu,” Rose alieleza kwa sauti yake tamu ya kumtoa nyoka pangoni.
“Hongera motto mzuri, huyo tajiri ni nani anayeiacha starehe tamu kama yako na kutokomea?” Kamanda Amata alitupa swali. “Aaaa si unajua tena wenye pesa wanafanya lolote, muda wowote wanapoamua, anaitwa Mr Bill, lakini tusiongelee habari za mwanaume mwingine, tuongee yetu,” Rose alijibu.
“Sawa, lakini mimi nataka nimuone Bill, amenidhulumu pesa yangu, kuna kazi alinipa nimemfanyia kwa ukamilifu lakini hajanilipa,” Amata aliendelea.
“We Bill unamjua?” Rose akauliza kwa mshangao na kujitoa katika kifua cha Kamanda Amata. Amata akatoa picha ndogo na kumuonesha, “Huyu siyo?” akamuuliza na kumpa ile picha.
“Ni yeye,” Rose alijibu huku akimrudishia ile picha, “Pole sana nafikiri itakuwa mmedhulumiana na si kakudhulumu, mbona ni mtu poa sana huyu!” aliendelea. “Lazima awe poa kwako lakini si kwangu, Bill alikupa deal gani mrembo?” alijibu hoja ya Rose na kumuunganishia na swali.
“Aaa, starehe za ngono na kazi binafsi za kukutana na watu wake anaowataka,” Rose akaanza kumpapasa Amata maeneo ya kitovuni mara akaanza kukinyonya kitovu hicho huku mkono wake mmoja ukiwa safarini kuelekea ndani ya boxer ya Kamanda, hali ikawa tete kidogo kwani macho ya Kamanda yalipotua katika kiunno cha binti huyo alikuwa katika mtindo wa kifudifudi na kulifanya shuka llililomsiti kuangukia upande wa pili, alishuhudia kiuno kicho kutangulia na makalio yenye kuvutia, mkono wake ulitamani kuyaminyaminya lakini akajikataza kwani bado alikuwa hajakamilisha analotaka kwanza.
“Baby, nipe cha asubuhi,” Rose alilalamika huku akijiinua na kupiga magoti huku akiiweka kati ya mapaja yake miguu ya Amata, mokono wake ukiwa tayari umeshachoropoa ndungula ya Kamanda na kuiweka nje.
“Rose, najua na nitakupa subiri kidogo.” Akamtoa pale alipo na kuliendea dirisha kisha akamuita Rose pale dirishani, “Tazama,” akamuambia, “Nini?” Rose akauliza, Kamanda Amata akamgeukia Kahaba Rose na kumtazama usoni, “Leo hii usingeyaona haya yote kwa maana ulitakiwa kuuawa kabla ya mawio,” Rose alishtuka kwa kauli hiyo, Kamanda akaendelea, “Nilikuja kwako nikuokoe kwa hilo na siyo mapenzi, rafiki yako Bill alitaka kutekeleza mauaji hayo kwa kutumia vijana wake,” alipomaliza kumwambia hilo akaichukua ile simu ya Yule marehemu na kumuonesha ile meseji, Rose akajitupa kitandani na kulia kwa uchungu.
˜˜˜
Wambugu alijikuta anashindwa kuchanganyikiwa baada kujua kuwa viajana wake wameuawa kule hotelini, na Kahaba Rose hayupo nyumbani kwake, alibaki kajifungia ndani akiogopa hata kutoka nje, macho yake yote yakiwa kwenye TV na simu yake. Hakuna akili nyingine iliyokuwa kichwani mwake zaidi ya kutoroka nje ya nchi, lakini kila alipomuwaza Bill alijikuta anaishiwa nguvu na kurejea kitini, maji yamezidi unga!
‘Nitagundulika,’ alijiwazia. Lakini bado maswali mengi yalikuja juu ya nani aliyetekeleza mauaji ya vijana wake pale hotelini, hakupata jibu. ‘Bill kaniachia msala, kanitoroka,’ alijiwazia mara kwa mara, lakini hakupata muda wa kujijibu, mara mlango wake ukagongwa, akashtuka nusu ya kuanguka ijapokuwa alikuwa ameketi kitini, taratiibu akaufuata mlango na kuufungua kwa woga, ‘Polisi?!’ alijiwazia, alipoufungua akakutana uso kwa uso na mwanamke kibonge alijitumbukiza kwenye baibui jeusi lililoruhusu macho tu kuonekana, kabla hajamkaribisha Yule mwanamke akapitiliza ndani na kuubamiza mlango nyuma yake.
“Unatetemeka nini mwanaume?” Yule mwanamke akauliza, Wambugu akabaki ameduwaa kwa sauti hiyo aliyoitambua vyema, “Nyie ni washenzi, wewe na Yule nguruwe wako, Bill,” ilikuwa ni sauti kavu ya Mellina ikimueleza hayo Wambugu ambaye alionekana hana la kufanya, Mellina akaendelea, “Ujio wangu hapa unapopaona wewe mafichoni, ni kuchukua pesa yangu, nataka kusepa leo hii, mji ushachafuka, njagu kila kona, haya fanya fasta”
“Mbona pesa zako tulimpa Cheetah,” Wambugu akajibu.
“Cheetah!? Msinifanye mi mjinga, Bill kamuua Cheetah na nimeiona hiyo action kwa macho yangu kwa taarifa yako, sasa sema napata pesa sipati? Mi sina muda wa kupoteza,” Mellina alifoka.
“Pesa nakupa Mellina, lakini naomba jambo moja,” Wambugu akatulia kidogo, kisha akendelea, “Mimi hapa nilikuwa nataka kutoroka na kiukweli Bill alishasema wewe uuawe, ila sioni umaana wa hilo, tufanye mpango tutoroke pamoja, unasemaje?” Mellina alitulia kimya kwa sekunde kadhaa, kisha akanyanyua uso wake kumtazama Wambugu, “Sikuamini hata kidogo,” Mellina alimwambia Wambugu, akatulia kidogo na kuendelea, “Nipe pesa kwanza mengine tutaongea.” Wambugu akavuta begi lake na kuingiza mkono ndani yake, alipoutoa akaibuka na donge nono la pesa, mellina akatabasamu alipokuwa anapokea pesa yake, akaitia ndani ya baibui lake na kugeuka kuondoka, “Kila mtu afe na dhambi zake,” alitamka maneno hayo akiwa ameshika kitasa tayari kutoka nje, mara nyuma yake akasikia mlio hafifu wa kilinda usalama cha bastola, kabla hajageuka, chuma baridi kikamgusa kisogoni, “Ha ha ha ha ha, huwezi kutoka hapa ukiwa hai, never” sauti ya Wambugu ilisikika nyuma yake …
Mellina alisimama ghafla, akameza funda la mate lililokuwa kinywani mwake, hakugeuka haraka kwa kuwa hakujua adui yake sasa amejiandaa vipi.
“Kwa hiyo ndio hila zako sio?” Mellina akamuuliza Wambugu huku bado akiwa anaangalia mbele.
“Nilishapewa kazi na Bill nikumalize ili kuondoa ushahidi wowote usio na tija,”
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi