MAUAJI YA KASISI (18)
Jina: MAUAJI YA KASISI Mtunzi: Richard Mwambe SEHEMU YA KUMI NA NANE ILIPOISHIA... “Kwa hiyo ndio hila zako sio?” Mellina akamuuliza Wambugu huku bado akiwa anaangalia mbele. “Nilishapewa kazi na Bill nikumalize ili kuondoa ushahidi wowote usio na tija,” JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Wambugu alijibu kijeuri. “Kwa hiyo katika orodha uliyopewa, umeshaua wangapi?” Mellina aliuliza, alitumia mbinu ya kuongea ikiwa ni moja ya kumzubaisha Wambugu kabla hajapanga ni nini cha kufanya katika hali kama hiyo amabayo kwayo hakuna masikhara kwani maisha yako yapo kwa adui yako. “Bill alishamaliza kazi yake, na alishapata kile anachokitaka, hivyo basi ninyi mlioshiriki ambao mnaweza mkatoa siri hii lazima msiwepo katika uso wa dunia, Gichui amekwenda, Cheetah hayupo, umebaki wewe na Kahaba Rose ambaye muda si mrefu roho yake itakuwa mikononi mwangu,” Wambugu aliongea kwa pozi, wakati Mellina alikuwa akifikiri juu ya…