
Mtunzi: Richard Mwambe
SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Ilikuwa ni usiku ambao Madam S alibanwa na kazi nyingi, akikumbuka kikao chake cha machana na watu wengine wa idara ya usalama wa taifa alihisi jambo jipya hasa kutokana na kutoroka kwa Amata hospitali na kwenda kusikojulikana.
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
Walimtuhumu kuwa ni mtovu wa nidhamu, asiyejali yale anayoambiwa na wakubwa wake, wote kwa sauti moja wakaona Kamanda Amata anyang’anywe cheo chake hasa kutokana na uzembe anaouonesha kwenye kazi za maana kama hizo. Ijapokuwa mvutano ulikuwa mkubwa sana kati ya wana kikao, lakini mtu mmoja alionekana kushikia bango sana kamanda ashushwe cheo, kwa kuwa hafai tena, lakini kabl;a ya yote atafutwe, arudishwe kasha apewe barua ya kushushwa cheo na abadilishiwe idara.
Kichwa kilizunguka, Madam S alibaki njia panda, hoja imepitishwa lakini bado moyoni mwake anamhitaji sana maana alijua wazi kuwa hakuna mtu anayeweza kushika nafasi hiyo ngumu. Atafanyaje, lazima afuate maamuzi ya kikao, Madam S alianza kuwaza kustahafu kazi endapo Kamanda Amata atashushwa cheo, amtetee vipi? Aliumiza kichwa kwa hilo. Alipoona hapati jibu kwa hilo, aliamua kuachana nalo, ataona wakati ukifika, alijipanga kwa safari ya Nairobi ili akakutane na Kamanda, waongee wamalizane hukohuko, aliamua kufanya safari hiyo kwa siri sana, asijue mtu yeyote.
Akafunga ofisi na kuondoka zake kujipumzisha nyumbani kwake Masaki. Hakuwa na muda wa kupoteza, alipotoka tu ofisini aliwasiliana na watu wa uwanja wa ndege akapata ndege yashirika la Swiss ambayo ilikuwa iondoke saa nne usiku huo kuelekea Zurich, kwa kuna watu waliokuwa wapandie Nairobi, kwa heshima yake alipatiwa siti moja kwa bei ya kawaida yenye punguzo la asilimia 25. Aliweka kibegi chake cha mgongoni tayari, nguo chache na vitu muhimu, bila kusahau kikoba cha vipodozi. Bastola zake mbili aliziandaa tayari kwa safari hiyo, alipohakikisha yuko poa alijiswafi kidogo kisha akajitupia jeans moja kali na fulana nyeuzi kichwani nakavaa kapelo nyekundu iliyomrudisha katika ujana kwa kila atakayekutana naye.
Saa nne kasoro robo ilimkuta uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, akaegesha gari yake mahala pa usalama ndani ya uzio wa uwanja huo kwa kibali maalumu kisha akingia ndani katika eneo la kuondokea wasafiri. Akatoa hati zake na kumkabidhi mwanadada aliyekuwa hapo kwa kazi hiyo.
“Ooh, karibu sana, tulikuwa tunakusubiri wewe tu, watu wote wako tayari kwenye ndege,” alizungumza Yule mwanadada aliyevalia nadhifu kabisa alimkaribisha Madam S na kuingia nae ndani moja kwa moja kwenye ndege hiyo ya kisasa kabisa, alimuonesha siti yake na Madam akaketi tayari kwa safari, baada tu ya yeye kuwa ameingia, ndege ile ilijitoa katika vizuiz vyake ikisukumwa na gari kubwa kuipeleka barabarni.
§§§§§
NDEGE na Kamanda Amata walikuwa wameegesha gari yao pembezoni mwa jengo la Posta katika mji wa Nairobi, wakijadiliana hili na lile jinsi ya kumnasa Wambugu. Kamanda Amata alichukua simu ya Wambugu, simu ya kisasa kabisa akaigeuzageuza na kumtazama Wambugu, “Unamjua Wambugu kwa sura?” akamuuliza.
“Hapana, sijawahi hata kumuona, hata hilo jina ni geni sana kwangu,” Ndege alijibu. Kamanda Amata akaichukua namba ya Wambugu na kuiingiza katika simu hiyo, akaiunga kwenye mtandao wa internet, kisha akaingiza nambari Fulani Fulani na kufungu mtandao wa usalama wa Tanzania, akaingiza ile namba pamoja na jina Wambugu katika na kujaribu kufananisha vitu hivyo. Haikumchukua muda mrefu simu hiyo ilimpa majibu, namba, jina na picha vyote vitatu vilionekana kwa wakati mmoja na maelezo mengine kedekede.
“Ndege!” Amata aliita na kumpa ile simu, “Unahisi huyu anaweza kuwa ndiye?” akamuuliza, Nege akaitazama ile picha kwa makini sana akatikisa kichwa.
“Naijua sura hii vizuri, ni moja kati ya wahalifu wanaoisumbua serikali,” Ndege alijibu huku akiirudhisha ile simu kwa Kamanda, kamanda Amata akaihifadhi ile picha katika sehemu maalumu kwa kazi hiyo ndani ya simu ile. Kisha akafunga ule mtandao na kurudisha simu katika hali ya kawaida, hakuishia hapo, “Ndege, piga simu kwa jamaa yako wa kampuni ya simu, atuambie simu tatu za mwisho za Wambugu zinasemaje tunaweza kupata majibu ya shaka letu.” Ndege akaichukua ile simu na kufanya hivyo kisha wakasubiri jibu watakaloletewa. Haikuchukua muda ukatumwa ujumbe wa sauti katika simu hiyo, Ndege akaufungua na kusikiliza, hawakukosea, ilikuwa sauti ya Bill ikimtaka Wambugu aende Iryamurahi akajifiche huko.
“… najua kuwa una mahangaiko makuu, najua kuwa Mellina amekamatwa, sasa sikiliza, na husijibu simu hii bali tekeleza unaloambiwa, ondoka haraka Nairobi kwa njia za siri unazozijua wewe, njoo Iryamurahi utanikuta hapa, kisha tupange mpango kabambe wa kuondoka katika nchi hii, nakusubiri, ukifika hapa mjini nitakupigia…”
Ilikuwa ni mwisho wa ujumbe ule wa sauti.
“Ina maana Bill yupo Iryamurahi?” Ndge aliuliza kwa mashaka, huku akiwasha gari na kuliingiza barabarani kuchukua barabar ya kueleka Embu.
“Ndege, Bill ni jasusi la kimataifa, hawezi kukaa nchini kwako wakati kazi aliyopewa imekwisha,” Amata alimjibu Ndege, akaichukua tena simu ya Ndege nakuanza kufanya utundu mwingine wa kupata uelekeo ambao Wambugu atakuwepo kwa wakati huo.
“Unafanya nini?” Ndege akauliza.
“Natafuta uelekeo wa Wambugu atakuwa wapi, kama katoka Nairobi au bado hajatoka tusije tukapoteza muda,” Kamanda Amata alijibu.
“Hiyo kazi ndogo Kamanda, piga simu kwa huyo jamaa atatuambia point gani alipigia simu mara ya mwisho na sasa atakuwa maeneo gani kadiri ya signal inavoonesha,” Ndege alimuelekeza Kamanda.
“Ndege acha kutumia njia za kianalogia hizo, sasa hivi namtafuta kwa GPS na nitakwambia alipo,” Kamanda Amata akaiweka simu katika program ya GPS akajaribu kuingiza namba za Wambugu na kuitafuta simu anayoitumia, jibu likaja, ikatumwa namba ya IMEI ya simu ambayo kwa wakati ule ilikuwa imebeba sim card ile, akaendelea na utundu wake mpaka akaweza kuunganisha mtandao huo, taraytibu ramani ya Nairobi na vitongoji vyake ikaonekana katika kioo cha simu hiyo, kidoti chekundu kikatua katika maeneo ya Juja. Kamanda Amata alicheka kwa ushindi huo.
“Wambugu hayupo mbali sana,” Amata alimwambia Ndege, akamtajia na vpimo vya ardhini kabla hajamaliza Ndege akamwambia hilo ni eneo gani.
Gari ikaongeza moto kuelekea barabar ya Embu kumuwahi Wambugu, “Tusifanye lolote, twende nae mpaka Iryamurai tukaone kuna nini,” Kamanda Amata alimwambia Ndege aliyekuwa katika usukani akiendesha gari hiyo kwa kasi ya ajabu.
“Kamanda, kimpata Bill utamfanyan nini?” Ndge aliuliza swali la kizushi.
“Sijui, ila shetani anajua maana nina hasira nae, na nitamfuata popote alipo katika dunia hii, mpaka nimtie mkononi,” Amata alijibu. Wakati huo walipita maeneo ya Kasarani na kuendelea kuikanyaga lami kusonga mbele.
§§§§§
Saa sita usiku, ndege ya Swiss ilikanyaga ardhi ya Nairobi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta. Madam S alikuwa ni mtu pekee aliyeshuka katika ndege hiyo, aliwashukuru wafanyakazi kwa ukarimu wao na kuzishuka ngazi hizo kwa fujo. Alipomaliza itifaki zote, alitoka nje lutafuta usafiri wa kwenda mjini.
“Karibu Madam, karibu sana Nairobi,” ilikuwa ni sauti ya kiume iliyotokea kwa nyuma yake, madam alisita kwa kuwa hakutegemea kupata ukaribisho wa aina yoyote hapo Nairobi, mkono mmoja ukiwa ndani ya jacket aliloliva muda mfupi uliopita katika kukabiliana na baridi ya Nairobi, aligeuka nyuma na kumuona kijana huyo mwembamba mrefu, sura yake haikuwa ngeni sana machoni, alimtazama tena na tena kisha akamkubuka, “Mashaka?” alimuuliza.
“Ndiyo, Mashaka, kutoka ubalozi wa Tanzania,” alijibu Yule kijana ambaye jina lake ni Mashaka, alietumwa miaka kadhaa nyuma kufanya kazi za idara ya usalama katika ofisi za ubalozi wa Tanzania huko Kenya.
“Kwangu?” Madam aliuliza.
“Ndiyo,” Yule kijana akajibu, kisha madam akaondoka eneo lile na kuelekea kunakoegeshwa tax, akaingia na kuketi ndani, Yule kijana akarudi na kuingia kwenye gari binafsi nyingine. Dereva wa tax hiyo akageuka nyuma na kumtazama Madam S, kabla hajaongea chochote Madam S alimwambia, “Safari Park Hotel,” kisha akampa noti tatu za shilingi elfu moja moja za Kenya, safari ikaanza.
Kwa kuwa ni usiku haikuwa tabu na wala haikuchukua muda kwao kufika katika hotel hiyo. Akiwa ameketi katika gari hiyo mara alihisi mfinyo katika mkono wake wa kushoto, akauinua na kuitazama saa yake kisha akabofya kitufe Fulani, mara mkanda mwembamba ukatoka kwa chini ukiwa na maadishi Fulani, akausoma na kuukata kisha akautia kwenye mfuko wa suruali.
‘…Kamanda Amata yupo Nairobi, kwa sasa yupo barabara iendayo Embu akielekea upande wa kaskazini, nimemnasa pindi alipotumia mtandao wetu wa usalama kwa kupitia nywila yako. Chiba…’
Ulikuwa ni ujumbe uliokuwa katika kijimkanda hicho. Madam S alikunja sura, ‘mshenzi kabisa Amata, kaipata wapi password yangu?’ alijiuliza.
Ilimbidi Kamanda Amata kutumia password ya Madam S baada ya kugundua kuwa ile yak wake ilikuwa imefungwa hivyo hakuweza kuingia kwenye mtandao wa usalama wa Tanzania, alijaribu kuibuni password ya Madam S mara mbili, mara mbili ya tatu akaipata na kuingia kwa kutumia jina hilo, baada ya kumaliza kazi hiyo ndipo Chiba alipojua kuwa kamanda Amata yupo Nairobi kwa jinsi alivyokuwa akichukua data ambazo zinaendana na kazi aliyotumwa tangu mwanzo huko Nairobi.
Ubalozi wa Tanzania huko Kenya kupitia mtaalamu wa mawasiliano aliyepelekwa kwa ajili ya kublock password zilizoibwa na Bill, Frank Masai aligundua kuwa muingiliano huo uliotokea Nairobi kwa vyovyote madam S alikuwapo hapo, alipowapa taarifa hiyo wengine wakafanya uchunguzi wa haraka na kugundua kuwa Madam S yupo njiani kuja hapo Nairobi, hivyo wakamtuma Mashaka kumuwekea ulinzi kutokana na hali halisi ilivyo katika jiji hilo.
Madam S aliweka kambi katika hotel ya Safari park, alihakikisha kila kitu kipo salama, na kupanga jinsi ya kumsaka Kamanda Amata kwa udi na uvumba. Aliifungua laptop yake ndogo na kuingia kwenye mtandao wa idara ya usalama, kwanza akaangalia ni nini Kamanda Amata alikuwa akifanya katika mtandao huo, akasoma maelezo ya Wambugu na kuitazama picha yake, akaangalia na maelekezo mengine mengi, akaichukua namba ya simu iliyojitokeza hapo ambayo Amata aliitumia kuchukua maelezo hayo, akatabasamu na kumsifu Amata kimoyomoyo kwa jinsi alivyokuwa mtundu wa kufikiri pindi anapohitaji maelezo Fulani.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi