MAUAJI YA KASISI (24)
Jina: MAUAJI YA KASISI Mtunzi: Richard Mwambe SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE ILIPOISHIA... akasoma maelezo ya Wambugu na kuitazama picha yake, akaangalia na maelekezo mengine mengi, akaichukua namba ya simu iliyojitokeza hapo ambayo Amata aliitumia kuchukua maelezo hayo, akatabasamu na kumsifu Amata kimoyomoyo kwa jinsi alivyokuwa mtundu wa kufikiri pindi anapohitaji maelezo Fulani. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Alikumbuka jinsi anavyoweza kuiga sauti na saini za watu pindi anapohitaji kufanya hivyo, hakushangaa kusikia kuwa ameweza kupenya mtandaoni kwa kutumia password yake. Alijiuliza mwenyewe, nani anaweza kukaa katika cheo cha Kamanda Amata na akatosha katika kila idara, mapambano ya mikono, utumiaji wa silaha za aina na aina, lugha za kutumia, utundu wa kuendesha vyombo vya ardhini, majini na angani, utundu wa kuiga sauti za watu, saini za watu, vyote hivi nani angeweza, kama isingehitajika watu waw…