MAUAJI YA KASISI (25)
Jina: MAUAJI YA KASISI Mtunzi: Richard Mwambe SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO ILIPOISHIA... Alipofika tu pale hospitali alikutana na Bwana Shikuku, kila mmoja alimkumbuka mwenzie, waksalimiana kwa bashasha kwa kuwa ni miaka mingi hawajaonana. Baada ya hapo wote wawili wakaelekea ndani ya hospitali hiyo kumuona Ndege aliyekuwa amelala usingizi. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... “Kwa nini usimrudishe Nairobi kwa matibabu?” Madam S akauliza. “Amesema hatotoka hapa mpaka amuone Kamanda Amata,” Shikuku alijibu. “Ok, wameivana hawa. Ulikuwa unajua kama AmaTa yuko hapa?” madam S aliuliza tena. “Ndio kwanza nafahamu sasa kuwa yuko hapa siku nzote sikuwa najua,” Shikuku alidanganya, wakati Ndege alishamwambia kuwa kamanda Amata yupo Nairobi kwa shughuli hiyo ila si kiofisi. Madam S alitulia kimya akitafakari jambo Fulani, alionekana wazi kukosa raha usiku huo, aliitazama saa yake ilikuwa tayari ni saa kumi alfajiri. §§§§§ …