MAUAJI YA KASISI (28)
Jina: MAUAJI YA KASISI Mtunzi: Richard Mwambe SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE ILIPOISHIA... “ Kamanda Amata , hilo jengo unaloliangalia ndio jumba la Don Andreas ,” Fr Frank alimwambia Kamanda Amata, “Nimekupa chumba hiki kwa makusudi mazima ili uweze kuliona jumba hilo, sasa sisi tunakuacha ratiba zako utapanga wewe, kama utahitaji msaada kutoka kwetu basi usisite kunijulisha,” Fr Frank akondoka zake. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Kamanda Amata alifunga vifaa vyake ikiwemo camera kubwa moja na darubini yenye nguvu kabisa ambayo inaweza kuona umbali wa kilomita kadhaa pia yenye madini ya kukuwezesha kukuonesha gizani, akaiweka pale dirishani pamoja na kamera ndogo ambayo ingeweza kupata picha nzuri za mnato na mjongeo kupitia darubini hiyo. Alipohakikisha vyote viko sawa, alijaribu kuangalia kwa kupitia darubini ile, aliweza kuona walinzi waliokuwa wakizunguka huku na kule wakiwa na mambwa mwakubwa ya kutis…