MAUAJI YA KASISI (29)

Zephiline F Ezekiel

SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA
ILIPOISHIA...
Alikuta watoto wakicheza cheza katika ngazi za kanisa hilo, mara mbele yake gari oja ilikuwa ikija pale aliposimama, Bill akaisimamisha, alikuwa ni Fr Frank, akitoka kwenda mjini kutafuta mahitaji, Bill aliiendea ile gari na kufungua mlango akaingia na kuketi kiti cha pembeni bastola mkononi,

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
“Unahifadhi wanausalama sio?” alimuuliza Fr Frank ambaye alionekana kutetemeka mwili mzima. “Hapana, hapana,” akamjibu. “Huyo kasisi wenu mweusi ni nani? Si Kamanda Amata?” swali lingine lilitua sikioni mwa Fr Frank. Kisha Bill akamuamuru Fr Frank kuendesha gari mpaka maeneo anayoyajua yeye. Lilikuwa ni shamba kubwa ambalo lilikuwa na aina mbalimbali ya miti na mazao, Bill alimshusha Fr Frank na kumuongoza katika banda Fulani, akaingia, alichokifanya ni kumfunga kamba kisha kuanza kumpa mateso makali ili amueleze kama ni kweli wamemficha Kamanda Amata ndani ya nyumba yao, Fr Frank hakujibu kabisa swala hilo. “Unajifanya jeuri siyo, basi yatakupata yaliyompata Fr Gichuru kule Nairobi,” Bill alimwambia Fr Frank huku akimpa kipigo kikali kwa kutumia mkanda wa kijeshi.

Kisha akamuacha ndani ya banda hilo nay eye akaondoka kurudi mjini. Breki yake ilikuwa moja kwa moja ofisini kwa Andreas, kumpa habari hiyo nyeti. Andreas hakuonekana kuumiza kichwa kwa swala hilo. “Bill, nimeshakwambia fanya nunaloweza umuue bas, sitaki habari nyingine,” Andreas alisisitiza. Kabla hajajibu kitu, Andreas akamwambia Bill, “Ila leo jioni tukutane pale nyumbani kuna tafrija fupi kwa ajili ya kijupongeza kwa kukamilisha hili swala, na Fr Gustav atakuwepo maana tayari yuko njiani.” Bill aliupokea mualiko huo na akawa tayari kujumuika na wageni watakaokuwepo siku hiyo.

Fr Frank alibaki kule bandani peke yake, mwili wake ukiwa hoi kwa maumivu makali ya kipigo alichokipata kwa Bill, kwa kutumia ujanja alionao alijua jinsi ya kujinasua katika kifungio hicho, akafanya makeke yake na baada ya dakika kumi na tano alikuwa huru, sasa kilichomsumbua ni kupata funguo ya kutokea nje. Fr Frank alitafuta mahali pazuri kwa kujificha ndani ya banda lile akapapata, akajificha na kutulia tuli akisubiri yeyote atakayekuja aelewane nae.

Fr Frank hakuwa mjinga katika mapigano iwe ya mikono au ya silaha, alikumbuka sana alipokuwa jeshini mara baada ya kuhitimu masomo yake huko Austria, alipokuwa akijifunza karate na kungfu akiwa seminari, alimstahi Bill kwa kuwa alihisi labda kuna kitu atakachokigundua mahali hapo. Fr Frank aliajiriwa na FBI kisirisiri na alikuwa hapoa Aachen kwa kazi moja tu ya kumnasa Bill na kupeleka taarifa zote huko Marekani ili wajue jinsi ya kumnasa na kumuweka chini ya ulinzi. Hakutaka kujionesha juu ya hilo hivo alikuwa makini sana katika kulifanya. Ni miezi mitatu sasa tangu ahamishiwe katika kanisa hilo kuendelea na uchunguzi wake, na alikuwa akiju kila ktu kilichotokea kule Nairobi. Akiwa katika mawazo kule katika maficho yake alisikia mlio wa gari ikija maeneo yale akatulia na kusubiria watu hao ambao walikuwa wakizungumza wao kwa wao, harakaharaka alielewa kuwa watu hao wa[po watatu.

Mara mlango ulifunguliwa na wale jamaa wakaingia ndani wakashangaa kukuta kiti wazi, hayupo Fr Frank. Mmoja wao akainua redio yake na kutoa taarifa kwa waliowatuma kuwa mtu wao katoroka, akiwa tayari kamaliza kuongea na simu hiyo, aliirudisha mahala pake na kwaamuru wake wenzake kumfuata, lakini kabla hajafika mbaliki lilikuwa ni t eke zito lililotua nyuma ya sjingo yake, kisha akajiviringa na kusimama upande wa pili, wale wawili nao wakaja kwa pamoja Fr Frank akaruka juu nakuitawanya miguu yake na kumpiga kila mmoja kwa mguu wake, mmoja alijibamiza vibaya katika nguzo iliyokuwa katika banda hilo na kupasuka sehemu ya nyuma ya kichwa chake.

Akajibwaga chini akiwa tayari hana uhai, wakati mmoja akiwa tayari katoka nje mwingine aliendelea kumkabili Fr Frank, alirusha ngumi ikakwepwa, akarusha nyingine ikakwepwa tena kwa mtindo uleule, kabla hajakaa sawa Yule jamaa akapigwa teke hafifi katika kanyagio la mguu wake, aliposhusha sura kuangali chini, alijikuta anachezea makonde yasiyo na idadi ambayo yalimpeleka chini sakafuni akiwa hajiwezi, akiwa anatambaa alipigwa teke moja la nguvu mbavuni na akalala chini bila kipingamizi.

Fr Frank alimwangalia Yule jamaa akigalagala pale chini, mara akakumbuka kuwa kuna aliyetoka nje, akaichomoa bastola katika mfuko wake na kuvuta hatua chache kuuelekea mlango, mara akasikia nyuma yake mlio wa kiondoa usalama cha bastola, kwa kazi ya ajabu aligeuka na tayari kidole kilikuwa kwenye trigger, aligeuka huku akiwa anaenda chini kupiga goti moja akachezesha kidole na risasi mbili zikamtwanga Yule jamaa kifuani, akatoa yowe la maumivu nay eye akajiunga na wenzake pale sakafuni.

“Mwambe Bill, sina shida nae, na hsinifuate fuate,” alimwambia Yule aliyekuwa hai bado lakini hali yake ilikuwa mbaya kwani alimvunja mbavu mbili.

Akatoka nje ya ile nyumba na kuingia katika gari yake iliyotumika kumleta pale akapotelea mjini kama kawaida, akarudi mpaka misheni, akaegesha gari palepale, na kuingia ndani.

§§§§§

KAMANDA Amata hakuamini anachokiona katika darubini yake, mmoja wa wahudumu wa misheni, aliyempokea siku alipofika alikuwa akiongea na watu Fulani katika jumba la Don Andreas, Kamanda Amata akagundua hapo kuwa kumbe siri zingine za yeye kufika pale ijapokuwa ilikuwa kwa njia ya siri ni yeye aliyeipeleka kwa watu hao, akatoka na kuelekea jikoni, pale aliwakuta wafanyakazi wengine wakiandaa chakula cha jioni, hakuongea na mtu, akakiendea kibao kinachoonesha zamu za wafanyakazi, kweli siku hiyo Yule mfanyakazi alikuwa off, akaondoka akarudi ndani kila mtu mle jikoni alikuwa akimwangalia mtu huyu mweusi, walimdharau kwa rangi yake lakini yeye hakujali. Alirudi tena chumbani kwake mara hii hakumuona Yule mtumishi pale alipokuwa mwanzo. Akatembeza tena darubini yake na kunasa dirisha linguine lakini hakuwaona wale watu waliokuwa wakiongea na Yule mhudumu.

‘Msaliti’ alijisemea, na mara mlango wake ukagongwa, akauendea na kuufungua taratibu, alikuwa Fr Frank, akaingia na moja kwa moja akasimama mbele ya Kamanda, “Bill ameshajua kama tuko hapa?” Frank alisema, Kamanda Amata akatulia kumwangalia, hakuielewa kauli yake, “Uko hapa na nani?” akauliza. Fr Frank akagundua kuwa ametereza katika maongezi yake, akamtazama Amata, akakutana na sura ilijikunja kuwa sasa haina utani hata kama na askofu, Kamanda Amata akatoa bastola yake na kumnyooshea Fr Frank, “Niko na nani?” akauliza tena, “Mmeamua kunicheza shere sio? Mpishi wenu anatoa siri za mimi kuwapo kwa Bill sivyo, kumbe mnajua kila kitu, niambie niko na nani?” akazidi kuuliza. Fr Frank hakuwa na la kujibu, “Usihofu Kamanda, mimi si mbaya kwako,” akasema huku akitetemeka.

“Ninyi wote ni wasaliti humu ndani,” Kamanda Amata bhakuonesha kabisa masihara katika hilo, uso wake uliloa jasho la hasira. Fr Frank akamtazama tena Kamanda, “Mimi niko upande wako Kamanda,” akamwambia.

“Naitwa Frank Edson, kutoka FBI, idara ya upelelezi ya Marekani, nipo hapa kwa kazi maalumu lakini hakuna anayejua,” akajieleza.

“Lete kitambulisho,” kamanda akaomba, Fr Frank aktoa kitambulisho katika mfuko wake wa ndani na kumpa Amata akakisoma, ni sahihi kabisa.

Frank Edson, mpelelezi kutoka shirika la kipelelezi la Marekani FBI, alikuwa amepewa kazi maalum na ofisi yake, kazi ya kumfuatili Bill ili amtie mkononi na kumpeleka Marekani akajibu mashitaka yake. Frank kama alivyo alikuwa kasisi katika kanisa la Katoliki huko Texas Marekani, ijapokuwa alikuwa akifanya kazi hiyo kwa siri kubwa sana lakini viongozi wake wa juu walilifahamu hilo.

Katika harakati za kumsaka Bill kama jasusi linaloendesha shughuli zake kwa kukodiwa kwa nia mbaya na matajiri mbalimbali duniani, Marekani ilianza kumsaka tangu pale alipotekeleza mauaji ya balozi wao kule Iraq miaka kadhaa nyuma. Walimsaka kila kona bila mafanikio. Bill akaibuka tena katika sakata hilo la Nairobi, kwa kuwa wale waliokuwa wametumwa Kenya walishindwa kumnasa Bill, Frank alitumwa muda mrefu huko Ujerumani kabla Bill hajaenda Nairobi, hivyo akapewa kazi ya kuhakikisha anamtia mkononi hukohuko.

Frank alifika Aachen kama kasisi aliyekuja kwa kazi maalum na kufikia katika kanisa kuu la Aachen. Hivyo alijua kila kitu kinachoendelea juu ya Bill, hata Kamanda ASmata alipokuwa anakuja, Frank alikuwa akimfuatilia tangu akiwa Nairobi hivyo alijuwa wazi kuwa lazima atafika kwa kazi hiyo. Ili asilete Madhara, kwa kuwa yeye alitakiwa ampfikishe Bill akiwa hai huko Marekani, alijua kuwa Kamanda Amata kaja kwa mawili kummaliza. Hivyo alimpokea Amata kwa maelekzo toka ubalozi wa Tanzania, wakijifanya kuwa kanisa linataka kushirikiana na Tanzania katika sakata hilo hasa kwa kuwa walikuwa wanaitaka monstrance yao kumbe sivyo.

Bill alimjua vyema Frank Edson, na alipewa taarifa kuwa yuko hapo kitambo na mmoja wa mashushushu wake ambaye ni mfanyakazi wa misheni hiyo. Frank Edson, siku zote hakugundua kuwa ndani ya misheni hiyo kuna mamluki mpaka alipokuja kupewa siri hiyo na Kamanda Amata.

§§§§§

Fr Frank akamuonesha Kamanda Amata beji yake maalum ya FBI iliyobanwa vizuri katika loop ya suruali yake. Kamanda Amata akashusha bastola yake na kuirudisha kiunoni. “Samahani, si unajua hizi kazi zetu hakuna kuaminiana,” akamwambia Frank, “Hamna shida hata ningekuwa mimi ingekuwa hivyohivyo,” akajibu Frank, kisha wote wakasogea pale dirishani.

“Sikiliza, unamjua huyu?” kamanda akamuuliza na kumuonesha baadhi ya picha zilizopigwa na ile camera yake aliyoiunganisha na ile darubini pale dirishani, Frank alipigwa na bumbuwazi akabaki midomo ikimchezacheza, “Kaka ungeshakufa muda mrefu sema tu huo ukasisi wako umekulinda, la tayrai mauaji ya kasisi yangeshafanyika hapa Aachen,” Kamanda alimwambia Frank huku akimpigapiga kifuani kwa ngumi yake.

“Sasa Kamanda, hapa mambo yameshaharibika inaonekana huyu mpishi anajua na ameshawapa kila habari zetu, ndo maana walikufuata kule makaburini. Bill huwa hatoki ovyo lakini alinifuata leo hapa,” Frank akmwambia Kamanda. Habari hiyo ilimfanya Kamanda kushtuka, “Unasema Bill alikuja hapa?!” kamanda akauliza.

“Ndiyo, Bill kaja akaniteka hapa leo asubuhi na kunipeleka huko kwenye maficho yao,” Frank akaeleza. “Sasa nani kakuokoa?” lilikuwa swali la Kamanda.

“Si nimekwambia mi ni FBI yaani Federal Beureau of Investigation, sishindwi kujiokoa kwa watu dhaifu kama hawa,” Frank alitamba, sasa akiwa amevua ile kanzu ya kikasisi.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni