
Mtunzi: Richard Mwambe
SEHEMU YA THELATHINI
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
“Ndiyo, Bill kaja akaniteka hapa leo asubuhi na kunipeleka huko kwenye maficho yao,” Frank akaeleza. “Sasa nani kakuokoa?” lilikuwa swali la Kamanda.
“Si nimekwambia mi ni FBI yaani Federal Beureau of Investigation, sishindwi kujiokoa kwa watu dhaifu kama hawa,” Frank alitamba, sasa akiwa amevua ile kanzu ya kikasisi.
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
“Laiti ningepata hiyo nafasi ningemmaliza huyo mtu palepale, maana sihitaji mahojiano naye, nimetumwa kuirudisha roho yake kwa muumba wake, bas,” Kamanda akamwambia Frank. “No Kamanda, sikiliza, unatakiwa unisaidie tumpate Bill akiwa hai, serikali ya Washington inamtaka akiwa hai ili akaungane na wenzake kule Guantanamo bay,” Frank akamwambia Amata.
“Hamna shida, mimi serikali ya Dodoma imenituma niitenganishe roho na mwili wake, so tutagawana, wewe utamchukua akiwa hai na mi nitamtoa roho yake,” Kamanda Amata alimwambia Frank, kisha wakatazamana si kirafiki tena sasa kiadui zaidi. “Na hapa siwezi kuishi, hapanifai, kwa heri ya kuonana,” Amata akamalizia, kisha akamuacha Frank bado amesimama akitweta kwa hasira wakati yeye anaifungua ile darubini yake pale dirishani.
Saa moja baadae, Kamanda Amata alikuwa nje ya uwanja wa misheni hiyo, hakuna aliyejua kuondoka kwake, akiwa kava kofia kubwa aina ya pama na miwani myeusi akasimamisha tax iliyokuwa ikipita mbele yake, “Novotel tafadhali,” Kamanda alimwambia Yule dereva, naye bila kushangaa alipiga gia na kusonga mbele, dakika chache walikuwa mbele ya hotel hiyo, “Deutsche Mark 75 tafadhali,” Yule dereva alimwambia Amata, “Bado unatumia hiyo pesa ya kizamani? Hapa nina Euro na Dollar,” Kamanda akmwambia yule dereva, “Ok, US Dolar 65” akabadilisha, Kamanda Amata akampatia pesa yake kisha akaiendea kaunta ya bhotel ile.
“Nikusaidie boss,” mmoja wa wahudumu alichukua suitcase ya Amata na kutangulia Kaunta kisha akasubiri pembeni.
“Jina tafadhali,” sauti ya mhudumu mrembo kama Malaika ikamuuliza Kamanda Amata. Kama unavyojua ugonjwa wa kamanda Amata, warembo, akatabasamu, “Fransisco Kintu,” akajitambulisha kwa jina bandia. Yule mhudumu akaandika kwenye kompyuta yake, “Passport yako au kitambulisho tafadhali,” Yule mhudumu akaomba vitu hivyo kimojawapo.
Kwa kuwa Kamanda daima alikuwa habahatishi, alivuta wallet yake na kuchomoa moja ya kitambulisho akampa, ‘Fransisco C. Kintu – Utaifa: Uganda – Kazi: Muandishi wa habari UBC.’ Maelezo hayo yalionekana juu ya kitambulisho. Baada ya kuingiza maelezo hayo katika kompyuta yake, akamrudishia kile kitambulisho. Kamanda Amata akauliza bei kwa siku, akatajiwa akahesabu fedha ya siku mbili akampa Yule dada, “Oh samahani bwana Fransisco, tuhitaji Maestro card au Visa card kama hauna basi kadi yoyote ya malipo,” Yule mhudumu alimwambia Amata, akili ya Kamanda ikafanya kazi haraka, “Samahani situmii hivyo vitu, ninalipa cash, kama haiwezekani basi.”
“Ok, nitakusaidia kwa leo, lakini mara nyingine ukija Ulaya hatulipi kwa cash, sawa bwana?” Yule mhudumu akamwambia Kamanda kwa lugha safi ya kiingereza.
“Ich danke Ihnen” (nakushukuru) Kamanda Amata alishukuru kwa Kijerumani msaada huo.
“Danke, gleichfalls!” (nakushukuru pia) Yule mhudumu naye akajibu, huku akisimama na kelekea sehemu Fulani, akaja na kadi mkononi akampatia, Kamanda Amata akaitazama, kisha akatoa kadi yake ya kibiashara na kumuwekea mezani, akaondoka pale kaunta na kuelekea ghorofa ya juu kwa kutumia lift.
175 ilikuwa ni namba iliyosomeka mlangoni mwa chumba hicho, Kamanda Amata kama kawaida yake aliingia ndani na kukikagua chumba hicho kwa staili ileile aliyoizoea kuona kama kuna chochote cha kufanya ajulikane uwepo wake.
9
CHAKULA cha jioni kilikuwa tayari, simu ikapigwa chumbani kwa Amata kutoka pale kwenye chumba cha chakula ambapo Fr Frank na wageni wengine walitumia. Simu iliita kwa muda mrefu haikujibiwa, ikarudiwa na kurudiwa lakini wapi. Ikabidi Fr Frank aende chumbani kwa Kamanda Amata akamwangalie, alipogonga mlango hakuna jibu lililotoka ndani, akanyonga kitasa na mlango ukafunguka, alipoingia ndani hakukuta mtu, chumba kilikuwa tupu, kitanda kilitandikwa vizuri kana kwamba hakukuwa na mtu aliyekuwa akikitumia chumba hicho.
Akili ikamzunguka Fr Frank, akaona sasa kazi yake inakuwa ngumu ya kumpata Bill akiwa hai kutokana na kutoweka kwa Kamanda Amata.
Fr Frank alirudi mezani akiwa na hasira, “Mgeni wetu hayupo, kaondoka bila kuaga,” wale wahudumu wakashangaa kapitia wapi kwa kuwa hawakumuona kupita hata katika mlango wa kutokea nje. Fr Frank ndipo alipoelewa maneno aliyoambiwa tangu mwanzo na wakuu wake wa kazi, ‘Mtazame sana Kamanda Amata, ni mjanja zaidi ya CIA, huyo ni TSA no 1 ana uwezo wa kujigeuza hewa,’ Fr Frank alipokumbuka maneno hayo akaanza kucheka mwenyewe, kisha akaketi na kuendelea kula huku akifikiri zaidi juu ya Amata, kama alitaka kufanya kazi aliyopewa kwa muda mrefu basi sasa ilimlazimu kubadili utaratibu huo kwani Kamanda Amata alitaka kuifanya kwa muda mfupi zaidi, kasheshe.
§§§§§
KAMA ILIKUWA ni siku ya bahati kwa Kamanda Amata basi hiyo ilikuwa mojawapo kati ya chache katika maisha yake. Alipotoka kaunta alipewa kijikaratasi kama brosure ndogo, hakuwa na muda wa kuifungua ndani, baada ya kujiweka sawa, alipomaliza kuoga na kuchagua suti safi kati ya zile alizozikuta ndani ya kabati hilo, akaijonge meza yake na kukinyanyua kile kijikaratasi kilichopambwa kwa rangi za dhahabu za kuvutia, akakifungua na kukisoma, kilikuwa ni juu ya shindano la kamali ambalo lingefanyika siku hiyo saa 3:30 usiku katika casino iliyopo katika hotel hiyo, matajiri wengi walialikwa, hakuamini kabisa kama katika walioalikwa alikuwemo Don Andreas.
Akajua hapo kuwa Don Andreas ni mcheza kamali maarufu sana kwa jinsi alivyoelezewa pale katika hiyo karatasi, pia matajiri wengine wengi walialikwa, hivyo hata yeye alipewa nafasi kama angependa kushiriki, ama kwa kutazama shindano hilo au kwa kushindana kama ana uwezo. Tabasamu pana likaupamba uso wa kijana shababi, Amata. Katika ile karatasi ya mualiko kulikuwa na namba za kupiga kama utahitaji kushiriki kucheza, akavuta simu ya mezani na kupiga hizo namba kisha akaongea na mchezweshaji wa huo mchezo na kusajiliwa. Kamanda Amata akasubiri muda ufike ili aweze kushiriki mchezo huo na pia kuonana na Don Andreas ana kwa ana.
SAA 3:00 USIKU
POKER POINT
WAGENI walianza kuingia katika ukumbi huo mkubwa wenye kila aina ya starehe, huku kukiwa na muziki wa jukwaani ukipigwa na mwanamama mkongwe aliyealikwa siku hiyo Tina Turner kutoka Marekani. Watu walikuwa wengi na kila mmoja alionekana akiwa ametingwa na shughuli zake ama kunywa pombe na wapenzi wao au wakicheza michezo kama roulette, slots machine, lucky wheel na mingineyo mingi.
Ni meza moja kubwa sana ilibaki wazi hakuna mtu aliyeketi kwenye viti vilivyozunguka meza hiyo, viti kumi na nne, saba kwenye mstari wa mbele uliopakana na meza hiyo yan kijani yenye michoro kadhaa na saba vingine vilikuwa nyuma yake, lundo la karata maalum zisizochoka lilikuwa limewekwa hapo juu, taa angavu kabisa isiyokusumbua macho ilikuwa ikiwaka na kumulika eneo lile nyeti kwa watu nyeti. Mmoja baada ya mwingine waliingia eneo lile wakisindikizwa na akina dada warembo kabisa na kuwapanga vitini kwa namba. Baada ya kutimia vilibaki viti viwili, kimoja cha mbele na cha nyuma cha mpambe.
Wote walishangaa kumuona mtu anayeletwa na mwanadada mrembo, kijana mweusi, aliyependeza kwenye suti nyeusi iliyotanguliwa na shati jeupe na tai ndogo ya kubana shingo (neck tie), akakribishwa na kuketi katika kile kiti kimoja, akawatazama mmoja baada ya mwingine kisha mchezo ukafunguliwa na mchezeshaji akiwataka wachezaji kujitambulisha mmoja baada ya mwingine. Kila mmoja alijitambulisha na Kamanda Amata alijitambulisha kwa jina lile la bandia akijisema kuwa yeye ni mwanahabari lakini ni mcheza kamali mzuri sana katika macasino ya Afrika Mashariki.
Akakribishwa kwa kupigiwa makofi. Kamanda Amata alijikuta akiwa amekaa uso kwa uso na Don Andreas. Mtu mmoja mnene, mwenye sura ya tabasamu muda wote, alikuwa akimtazama kijana huyu bila kummaliza. Mchezo ulianzishwa na kila mmoja alitakiwa kuweka dau la kuanzia lisilopungua $ 2500, matajiri hao wakaanza kuweka na kuweka pesa zao kwa kutumia chungu maalumu kilichopitishwa mezani na mmoja wa wachezeshaji. Kila mtu aliweka kiwango anachojua kuwa anaweza kumudu.
Zamu ya Kamanda Amata, kila mmoja alimtazama usoni, akaingiza mkono ndani ya koti na kutoa $ 5000 na kuweka katika chungu hicho. Mcehezo ukaanza taratibu kila mtu akiwa na karata zake. Mchezo ulikuwa mgumu kidogo kwa maana kila mmoja alikuwa anatumia akili sana katika kuzifananisha karata hizo na zile zilizofichwa, kila aliyeshindwa alitoka, hivyo wakazidi kupungua, Kamanda Amata alikuwa wa nne kutoka na kuwaacha watatu, Don Andreas, na tajiri kutoka Venezuela pamoja na mwanamama tajiri kutoka Berlini. Mchezo ukaendelea na mwisho wa mchezo Don Andreas akatoka mshindi na kukusanya maelfu ya dola za Kimarekani.
Makofi ya pongezi yakatawala katika meza ile. Mchezo ule ukaisha, ukatakiwa kuanza mwingine kwa wale wanaohitaji kuendelea. Wote walirudi tena mezani na ‘betting’ zikaanza kwa mara nyingine, chungu kikapita na kila mmoja akatia mkono kuweka chochote lakini wenzako sharti waone kile uwekacho, zamu ya Kamanda Amata, kama kawaida wote walimtolea macho, akaingiza mkono wake tena katika koti na kutoa kitita kama kilekile, $ 5000 zingine akaweka, wengine katika katika mchezo ule wakaguna, kwa jinsi walivyomtazama hakuwa na muonekano wa kuwa na pesa kiasi hicho anachotoa katika kila bett moja.
Yeye mwenyewe hakuwajali, kwa kuwa hakuna aliyejua mpaka hapo kuwa ni nini anachokitafuta, hivyo hakuona tatizo kutumia pesa hizo anazopewa maalum kwa ajili hiyo ili kupata kile anachotaka. Mchezeshaji aliendelea kuchezesha mchezo ule kwa makini na mbwembe za hali ya juu. Mchezo ukaendele, poker, mchezo wa karata ambaon unatakiwa ucheze kwa kupanga kareta zako zifanane na ile iliyofichwa ambayo hakuna anayeijua, mchezo wa matajiri unaochezwa kwa kuwekeza pesa nyingi, wengine huweka magari au majumba.
Kamanda Amata mchezo huu aliupanda sana na sehemu yake kubwa ya kucheza ilikuwa pale New Africa casino, Dar es salaam. Wachezaji walianza kupungua katika mchezo kwa kuwa hawakufaulu, walizidiwa maarifa na wengine, mara hii Kamanda Amata alidumu katika mchezo, japokuwa hakushinda lakini alitoka wa pili na mchezo wa mwisho alicheza na Don Andreas, ambapo alizidiwa kwa ujanja mdogo sana.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi