MAUAJI YA KASISI (33)
Jina: MAUAJI YA KASISI Mtunzi: Richard Mwambe SEHEMU YA THELATHINI NA TATU ILIPOISHIA... Akaismama na kutoa shukrani kwa Yule dada, akavaa shati lake jeupe ambalo sasa lilikuwa halitamaniki kwa vumbi. Alipokuwa akitoka, mlangoni alikuta kuna majaketi yametundikwa, akajichagulia moja la rangi nyeusi akajitupia juu yake na kutoka nje, hakuwa na usafiri. Akatazama magari yaliyoegeshwa hapo, akaona moja inayomfaa. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Ford Cortiner ya rangi ya buluu ilikuwa imeegeshwa pembeni kidogo mwa jengo hilo na mwenyewe alikuwa ameliacha likiunguruma yeye akiwa ndani kunywa kahawa, bila shaka lilikuwa linatoka safari ya mbali, Kamanda Amata aliingia na kukanyaga mafuta akarudi barabarani, muziki mzuri wa You are not alone uliopigwa na Michael Jackson alikuwa ukitumbuiza. Saa katika dashboard ya gari hiyo ilionesha ni saa nane za usiku ikielekea saa tisa. Mwendo haukuwa wa kawaida barabaran…