
Mtunzi: Richard Mwambe
SEHEMU YA THELATHINI NA TATU
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Akaismama na kutoa shukrani kwa Yule dada, akavaa shati lake jeupe ambalo sasa lilikuwa halitamaniki kwa vumbi. Alipokuwa akitoka, mlangoni alikuta kuna majaketi yametundikwa, akajichagulia moja la rangi nyeusi akajitupia juu yake na kutoka nje, hakuwa na usafiri. Akatazama magari yaliyoegeshwa hapo, akaona moja inayomfaa.
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
Ford Cortiner ya rangi ya buluu ilikuwa imeegeshwa pembeni kidogo mwa jengo hilo na mwenyewe alikuwa ameliacha likiunguruma yeye akiwa ndani kunywa kahawa, bila shaka lilikuwa linatoka safari ya mbali, Kamanda Amata aliingia na kukanyaga mafuta akarudi barabarani, muziki mzuri wa You are not alone uliopigwa na Michael Jackson alikuwa ukitumbuiza. Saa katika dashboard ya gari hiyo ilionesha ni saa nane za usiku ikielekea saa tisa.
Mwendo haukuwa wa kawaida barabarani, Kamanda Amata akili yote ilikuwa imehamia kwa Bill, sasa alikuwa anataka kumaliza biashara yake na Bill. Alikata mitaa michache na kushika barabara inayopita mbele ya kanisa kuu, akalitazama kwa mbali na kupitiliza, akalikaribia hekalu la Don Andreas, kwa kujifanya kuwa hana kazi nalo alipitiliza na kwenda kusimama mbali kidogo, akaegesha gari karibu na kituo cha mafuta, akaliacha linanguruma kama alivyolikuta, alipokuwa anatoka akawasha taa ya ndani kuangalia hiki na kile, hakuamini macho yake alipoiona AK 47 double barrel, akaitoa na kuvunja katikati kama kawaida, haikuwa na risasi, akapekua hapa na pale akakutana na kikebe chenye risasi kama kumi hivi akakichukua, akajaza risasi zote katika mashine hiyo na kujivuta kwa mguu kulielekea jumba hilo lenye ulinzi mkali. Haikumchukua muda kuifikia himaya hiyo yenye utulivu wa pekee, kwa nje ya jumba hilo alifanikiwa kuona gari mbili zimeegeshwa, moja ikiwa ni ile Vogue, ‘Hisia zangu zimesema kweli, Bill yupo hapa na atafia hapa, leo sina huruma na kiumbe cha mtu,’ kamanda Amata alijisemea moyoni, hasira ikiwa inamtawala kila baada ya nukta. Alitazama ulinzi ulivyojipanga akaona kuwa juu kuna walinzi lakini hakujua atafanyaje wasimuone.
Akachomoa bastola yake yenye kiwambo cha sauti, akamlenga mmoja na kumpata sawia kichwani, bajati nzuri aliangukia juu kulekule. Akaona sawa, mmoja tayari, alipokaribia ule wigo wa wavu maalum, akasita, kitu kikamwambia geula kulia, alipogeuka akakutana na taa kubwa inayoongozwa na sense, ukiingia umbali Fulani kutoka ule wigo, taa ile inakumulika kwa mwanga mkali na vingola vinaasha walinzi, hakuwa na mda wa kuhangaika na taa ya mtu, akaifumua kwa risasi moja, kisha akarudi nyuma na kutimua mbio kuuelekea ule wigo akapiga samasoti maridadi kabisa akapita juu ya wigo ule bila hata ya kuugusa, alipotua tu tayari AK 47 ilikohoa na kumteremsha mlinzi mwingine mpaka chini, alipogeuka kushoto kuna mwingine, kwa kutumia bastola yake akamfyatulia moja makini sana iliyochana bega upande wa moyo, Kamanda Amata akahama pale alipokuwa kwa maana alijua ataonekana, akapenya katika ya maua na kuifikia maiti ya mlinzi mmoja akaivua shot gun semi automatic, akaibeba mgongoni. Kamanda Amata akaendelea kusafisha nje kote, alihakikisha si mbwa si binadamu habakishi kitu.
Milio ya risasi ilifikisha taarifa ndani kuwa huko nje hakufai, Bill akanyanyuka na kuwaambia vijana wake wawe tayari. “Bila Shaka, tumevamiwa,” akmwambia Don Andreas ambaye alionekana wazi presha ikipanda. “Nani atuvamie wakati Kamanda amekwishakufa?” Bill akatoka nje ya nyumba hiyo, hakuna mtu, akiwa amefyumu kwa hasira, akiwagombeza vijana wake kwa uzembe wa kushindwa kuimarisha ulinzi. Akarudi ndani, hakumkuta Don Andreas, kaenda wapi, bahati nzuri vyumba vyake vya siri Bill anavijua, akaingia cha kwanza, cha pili akamkuta, “Hapa si pakukaa Andreas, tuondoke,” Bill alimwambia Andreas.
“Ramani ile pamoja na monstrance lazima tuondoke nazo,” Andreas alimsisitizia Bill, “Don, hatuna muda huyu jamaa ni kichaa,” Bill aliendelea kumnong’oneza. Wakatoka pamoja pale mafichoni na kuukimbilia mlango mkubwa lakini Andreas akarudi tena akiuendea ule mlango ambao una zile hazina zake zote. Bill alimtazama Andreas akiwa anahangaika kuufungua ule mlango. Bill akapotelea upande mwingine wa jumba hilo, sasa akiwa na bastola yake mkononi, akimuwinda huyo aliyevamia.
Kamanda Amata alikuwa akinyata kuuelekea mlango wa siri uliokuwa ukitokea upande wanyuma, aliutazama mlango ule ulikuwa wa chuma imara, sio shida, akaizungusha saa yake nayo ikaanza kuzunguka kwa kasi na kutoa mionzi iliyoweza kukata eneo la kitasa la mlango ule, aliporidhika akaizikma ile saa, akaujaribu mlango ukafunguka bila kipingamizi, akajitoma ndani. Akiwa katika kutembea taratibu, akahisi kitu kama kitu chenye ncha kali kikipenya eneo Fulani la shingoakaanguka chini na kupoteza nguvu, alijaribu kupambana na hali hiyo ikawa ngumua sana, akakumbuka vidonge alivyopewa na Madam S, akapenyeza mkono wake kwenye mfuko wa ndani wa suruali akachukua kimoja na kutumia nguvu yake ya mwisho kukimeza, mara akalegea na kujilaza.
“Ha ha ha ha ha ha ndege mjanja hunasa katika tundu bovu,” Kamanda Amata alisikia sauti hiyo kwa mbali sana, akafumba macho. Mara akasikia kitu kama kiatu kikimkanyaga kwa nguvu kichwani mwake. Akaamka l;akinin hakuonesha kukurukakara yoyote, bado alikuwa palepale chini, “Utafia ughaibuni, Mbwa mweusi wewe, wewe unaweza nkujifanya polisi wa dunia wewe? Wenzako FBI wamefeli, we una nguvu bgani na hiko kishirika chenu cha upelelezi kuvuka mipaka kuja huku, sasa leo ndio mwisho wako, nitakuua huku nakurekodi kwenye mkanda wa video niwatumie wenziwako huko kwenu Afrika wakaushuhudie mwisho wako ulivyokuwa wa taabu na mateso, mwenzako anaejifanya kasisi kumbe ni jasusi tayari ninae na chamoto ameshakiona japokuwa hajafa, nitaua mmoja baada ya mwingine,” Bill aliwaamuru vijana wake wamburuze Amata kwenda shimoni kwenye mashine ya kifo.
§§§§§
FR FRANK Edson, alipojuwa kuwa Kamanda Amata ameingia katika mtanange hivyo anaweza kumuwahi kumpoteza Bill ilhali yeye anatakiwa ampeleke akiwa hai, aliamua kuyavulia maji nguo na kujikita katikati ya hatari hiyo, alilivamia jumba la Don mapema sana hata kabla Bill hajarudi akajificha katika moja ya stoo zilizokuwa ndani ya jumba hilo. Kwa bahati mbaya au nzuri alipoikuwa katika harakati za kutafuata pazuri pa kujificha kamera ndogo sana ya usalama ilimuona na kupeleka taarifa panapohusika ndipo shughuli ilipoibuka humo ndani, kipigo alichokipata kwa mkono wa Iron Man The Killing Machine alibaki hoi hajiwezi na kutupwa huko shimoni ambako hakuna hewa hakuna chochote ni mateso mpaka unakufa.
Fr Frank alishindwa kujitetea kwa jitu hilo la miraba mine baada ya kupata kipigo cha mbwa mwizi. Alikuwa nusu mfu katika chumba kile.
Kamanda Amata alijilegeza huku akiburuzwa mpaka katika lango la chumba hicho ambamo kinachofanyika ni kukutumbukiza, utakaa umo ufe kisha inamwagwa dawa maalum ambayo inakusagasaga na kuwa katika vipande vidogovidogo kisha wanaflash kama chooni na taka hizo zote hupelekwa baharini kupitia mfumo wa maji taka. Walipofika mlangoni, tayari kumtupa mle shimoni, Kamanda Amata alijitikisa kidogo, wale jamaa wakashtuka, mmoja akainama kumwangalia kama ni mzima au la, Amata akamtemea mate, kwa uzembe wa Yule mlinzi akauchia mkono wa Kamanda ili ajifute mate usoni, kosa. Konde moja zito lilitua tumboni kwa jamaa Yule akatema damu, huyu mwingine hajakaa sawa akachezea kipepsi kimoja kilichjomfanya ajisjike tumbo, sasa Kamanda Amata alikuwa huru na nguvu zake zilezile, alijurusha kiufundi na kuwapiga mateke ya migongoni kisha wale wawili wakaingia shimoni.
Kamanda akasonya na kurudi kwa njia ileile. Akapenya hapa na pale na kutokea eneo lenye veranda kubwa, akawa kizungukazunguka ajui nini cha kufanya, akiwa katika hali hiyo alihisi mkono wenye nguvu umekamata bega alipogeuka akakutana uso na jitu la miraba minne, mara akasikia vicheko kutoka sehemu asiyoijua. Lile jitu likamnyanyua na kumbwaga chini, Amata alijitonesha tena katika majeraha yake, akabaki kugugumia maumivu tu. Aliinua kichwa na kumwangalia huyo aliyemfanyia kitendo hicho, lilikuwa ni jitu lenye pande la mwili, lililojaa misuli mikubwa, kamanda Amata akaona wazi kuwa Frank Edson hakuwa na budi kuwa katika hali ile kama alipambana na dubwana hili, akajikokota kunyanyuka ajaribu bahati yake, konde la pili lilimrusha nyuma na kujibamiza vibaya ukutani, Kamanda Amata akatema damu, alipokuwa akijaribu kuinuka akapigwa teke la mbavu, nguvu ya teke lile ilimsukuma mpaka ukuta wa pili, Kamanda alijikuta akiwa na hali mbaya, alijitahidi kuinuka lakini ilikuwa ngumu, alibaki kutambaa.
Mara sauti ikasikika kwenye chombo maalumu kilichofungwa darini, ilianza na kicheko; “Ha ha ha ha ha ha, Kamanda Amata, wewe unajua sana kufuatilia nyendo za watu sio za miungu kama sisi, sasa leo pambana huyo Israel mtoia roho, kama wewe unaweza kukishinda kifo basi leo tutaona ujanja wako uko wapi, ha ha ha ha ha ha hapo ulipo ndio kuzimu ulipokuwa ukikusikia kwenye vitabu vya dini zenu, pambana na mashine ya kifo hiyo, ukiishinda nitakupa utajiri wangu wote,”
Maneno yale yaliyokuwa yakisemwa na mtu asiyemuona yalimtia hasira sana Amata, “Utajiri wako baki nao mwenyewe, kwa kuwa sikutaka kukutoa roho sasa umeniladhimisha kufanya hivyo,” ilikuwa sauti ya uchovu kutoka kwa Kamanda Amata. Vicheko vikaanza tena kwenye kile chombo, sasa vikiwa kwa fujo zaidi, Kamanda Amata alihisi kitu kama upepo kimepita sikioni mwake pindi alipokuwa akigeuka, kumbe guu la lile jitu lilipita akiwa na lengo la kumpiga teke la kichwani pale chini alipojiinamia, Kamanda Amata kwa kasi akaona amepata nafasi nzuri ya kufanya mambo, alipiga ngumi moja iliyotua kwenye korodani za jitu hilo, likaguna kwa maumivu.
Akajiinua kwa ustadi na kujisahaulisha maumivu yake, akawa wima, alikusanya nguvu zake zote na kuruka hewani alikoichanua miguu yake na mateke yote mawili yakatua shavuni mwa lile jitu, lakini halikutikisika hata kidogo. Kabla mguu wa Amata haujatua chini, ulidakwa, Kamanda akautumia kama nguzo na kujivuta kuelekea usoni mwa lile jitu, akalipiga kichwa cha jichoni kwa maana alijua kwa vyovyote atalipoteza maboya, kama aliota. Kile kichwa kilipotua jichoni lile dubwana lika muachia Amata na kujishika jicho, Kamanda Amata akatua sakafuni kwa miguu miwili baada ya kuruka samasoti safi sana, alitahamaki na kuliona lile jitu likimjia kasi kama mbogo, akalikwepa nalo likajibamiza ukutani, Kamanda Amata akatazama huku na kule akaona taa iliyosimamishwa kwenye nguzo ya chuma,
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi