MAUAJI YA KASISI (34)

Zephiline F Ezekiel

SEHEMU YA THELATHINI NA NNE
ILIPOISHIA...
Kile kichwa kilipotua jichoni lile dubwana lika muachia Amata na kujishika jicho, Kamanda Amata akatua sakafuni kwa miguu miwili baada ya kuruka samasoti safi sana, alitahamaki na kuliona lile jitu likimjia kasi kama mbogo, akalikwepa nalo likajibamiza ukutani, Kamanda Amata akatazama huku na kule akaona taa iliyosimamishwa kwenye nguzo ya chuma,

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
akaiwahi na kuichukua akaivunja taa yake nayo ikabaki bila taa, akaiinua na kumpiga nayo mgongoni, lilipoguka kamanda Amata akatumia ule mnara wa taa akamchoma tumboni, lakini hakufanikiwa hata kumtoboa kutokana na ulaini wa chuma kile lakini alimpiga shoti moja mbaya ya umeme kutokana na kwamba alikuwa hajaichomoa kwenye soketi pale ukutani, Amata akatabasamu kwa hilo.

Lile jitu, lilipigwa shoti iliyolisukuma na likajibwaga zimazima pale chini. Vicheko katika kile chombo vikasimama ghafla. Kamanda Amata aligundua kuwa jinsi ya kulishinda lile jitu sio nguvu bali akili, alipi mguu chini na mara kitu chenye ncha kali kikachomoka kwenye sehemu ya mbele ya solo ya kiatu chake, na mguu mwingine vivyo hivyo, Kamanda Amata sasa akaanza kutumia miguu kuilishmbulia lile jitu, mateke ya usoni, mbavuni yalilifanya jitu lile lipoteze nguvu maana kila alipopigwa kwa teke aliachiwa jeraha kubwa kutokana na vile vyuma kenye viatu vya Amata. Zilikuwa dakika tatu za shughuli kubwa ya kulikalisha chini lile dubwana. Kamanda akasimama tayari kwa pambano akiliangalia lile jitu likigalagala sakafuni huku damu zikitapaka kila mahali.

Upande wa pili, Bill na Andreas walikuwa kimya wakitazama pambano hilo kupitia luninga ndogo ndani ya chumba nyeti cha Andreas, hawakuamini kile wanachokiona, kile kinachofanywa na Kamanda Amata, jinsi anavyotumia akili kuliadhibu jabali lile, mashine ya kifo kama wanavyoiita.

Tangu Andreas amnunue binadamu huyo wa ajabu huko Honduras na kumsafirisha kwa siri mpaka Ujerumani na kumuhifadhi katika nyumba yake, alishamtumia kwa kuua watu wengi sana wakiwezmo maafisa wa polisi, wanajeshi na wote wanaofuatilia nyendo zake kwa ukaribu, hakuna aliyewahi kufurukuta, wengi walikata roho kwa pigo moja tu, kisha miili yao aliitupi ‘kuzinu’ katika chumba alichokiandaa kwa kazi hiyo,. Akishakutupa humo hufungulia hewa yenye chemical kali amabayo hukukausha na kukumeng’enya kuanzia nyama yako mpaka mifupa vyote vinakuwa unga, kisha maji mengi huingia katika chumba hicho na kuondoka na mmeng’enyo huo kupitia mabomba yha maji taka, watu wako watakutafuta miaka nenda rudi na hawatakuona, umefutwa katika orodha ya binadamu duniani.

Leo ilikuwa tofauti, alimshuhudia Kamanda Amata akitoa dozi mbaya kwa jitu lake hilo analolitegemea kwa kazi hiyo. Kijasho kilipita kutoka kwapani na kufika mpaka kwenye kiuno kabla hakijaishia katika nguo alizovaa.

Kamanda Amata alipohakikisha dude hilo limezimika alitzama huku na kule ili kuona cha kufanya, sasa akili yake ilirudi kwa Bill na mwenzake Andreas, akiwa katika kutazamatazama mara akasiki kama nyayo za binadamu zikimfuata kwa nyuma, akatazama kwenye kioo kikubwa kilicho mbele yake na kuliona lile dude limesimama likielekea kwake kwa nguvu zote, Kamanda Amata hakuwa na silaha yoyote ya maana, akajua sasa kuwa amekwisha, kabla hajaona la kufanya, lile jitu likamfikia, likiwa na hasira mbaya, lilimpiga kikumbo Amata akapitiliza mpaka kwenye kioo cha mbele yake, alijibamiza na kile kioo kikamwagika pakabaki wazi, Kamanda Amata akadondokea upande wa ndani wa kile chumba kilichotenganishwa na kile kioo. Ilikuwa ni ofisi ndogoi lakini iliyojaa kila aina ya nakshi na samani za gharama, Kamanda Amata akanyanyuka na kuchukua chungu kilichokuwa na ua ndani yake na kukirusha sawia kichwani mwa jitu lile, likapepesuka kidogo, kabala halijatuliya, Amata akajirusha doule kick na kutu kifuani mwa lile jitu, kutyokana na kupoteza nguvu liliyumba na kujibamiza ukutani, ule mtikisiko wa ukuta ulifanya pambo la juu ambalo lilikuwa ni bichwa la Nyati lililotengenezwa kwa chuma.

Lilianguka na kumpiga kichwani, kisha lile bichwa la nyati liakadondoka sakafuni. Lile jitu likajitahidi kusimama lakini ilikuwa ngumu kutokana na kugongwa vibaya na lile bichwa la nyati bandia, ilikuwa ni nafasi ya Amata ya kumaliza mopja kwa moja akaanguka juu ya lile sanamu la kichwa cha Nyati, akachomwa na pembe za nyati zilizojinyomnga vizuri zikitanguliwa na ncha kali, likatoa kelele za uchungu huku macho yakiwa yamemtoka pima, likakata roho. Kamanda Amata akakung’uta mikono yake kwa kuashiria kazi imeisha, hakuamini kiama kalimaliza hayawani hilo.

Bill aliinuka na bastola mkononi, akiuelekea mlango ili atoke nje, mkono mmoja akiwa na ile fimbo yake ya kutembelea.

“Bill, hapa pameshakuwa pabaya, mi nafunga vyangu najificha dhidi ya huyo mtu wako,” Andreas alimwambia Bill, wote wawili walikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa, wakivujwa na jasho jingi. Andreas alichukua begi tupu, akainyanyua ile monstrance na kuiti begini kisha ile ramani, akaenda ukutani na kushusha picha moja, nyuma yake nkulikuwa na vibonyezo au vitufe kumi na mbili vikiwa na nmba pamoja na alama chache, akaanza kuvibonyeza ili mlango wa siri ulio kwenye sakafu ya chumba hicho ufunguke, nukawa unagoma kufunguka, alipojaribu mara ya pili nay a tatu mlango ule ukakubali, taratibu ukawa unapanda juu ili kuwezesha mtu kuingia.

Bill aliona taanyekundu ikiwaka juu ya dari la chumba hicho, ikiashiri kuna hatari, mara alishuhudia ule mlango mnene wenye ulinzi mkali ambao huwezi kuingi bila kuthibitisha vitu vitatu, namba ya siri, alama za vidole na alama za macho, na hivyo vyote vilikuwa ni Andreas peke yake aliyeunganishwa. Mlango ule ulionekana kwa ndani ukikatwa duara kutoka nje, Bill akajua sasa hapa Kamanada anaingia, akaiweka sawa bastola yake, hakuwa tayari kufa wakati anayemlinda anatoroka, akainyosha bastola kwa Andreas, Andreas akasikia mlio wa bastola hiyo ikiwekwa sawa kulipua, “Bill vipi tena?” Andreas akamuuliza Bill. Sikia bwege wewe, yaani huna shukrani, kazi yote niliyokufanyia, sasa hivi unaona mambo yameharibika unakusanya vyako unataka kutoroka na kuniacha mimi hata kunipa chochote sio, sitaki maelezo, nakumaliza mwenyewe,” Bill alimwambia Andreas kwa ukali.

“Sikia Bill, mi naokoa hii mali ya thamani, wewe ukishamuua huyo Kamanda Amata tuonane nitakupa donge nono,” Andreas alijitetea. “Siki, mi si motto, Kamanda Amata keshakufa mara mbili na kafufuka sasa unafikiri hapa atakufa tena?” Bill alimuuliza Andreas, Mara lile pande la chuma linalokatwa kwa saa ya Kamanda Amata, lilikuwa tayari kutoka mahala pake na kuruhusu mtu wa nje kuingia ndani, Bill alipiga risasi moja na kufumua kifua cha Andreas, Andreas akaanguka chini na kutoa yowe la maumivu, Bill akanyanyua tena mkono wake ulioshika ile bastola na kulenga lile tundu ili ampate Kamanda Amata, alipofyataua, viligongana vyuma tupu, hakuna risasi, akaitupa chini bastola na kunyanyua lile begi alilochukua Andreas na kuingia kwenye ule mlango na kuzama ardhini huku mlango ule ukijifunga nyuma yake.

§§§§§

Kama alitegemea kupona basi ilikuwa kwa asilimia ndogo sana, Frank Edson, aliona kile alichofanya Kamanda Amata pale mlangoni alipokuwa ameletwa na wale watu ili kutupwa ndani ya shimo hilo kusubiri kifo chake. Aliona kitu kidogo ambacho Kamanda Amata alikiangusha kwa makusudi wakati alipowaadhibu vikali wale jamaa wawili na kuwatumbukiza mle shimoni.

Ilikuwa ni kitu kama kidonge kidogo, kwa tabu sana Fr Frank Edson alijivuta kwa kutambaa mpaka akakipata kile kidonge alipokitazama alikijua vyema, kidonge kinachotumika kurudisha nguvu kwa haraka kwa mtu aliyekuwa na uchovu mwingi wa kupigwa au wa shuruba yoyote, pia kinaondoa maumivu kwa muda mrefu. Fr Frank Edson alimuona Amata kama Malaika wake, alikiokota na kukitia mdomoni, akakimung’unya, muda kumi na tano tu alipata nguvu taratibu mpaka akawa sawa na maumivu yake yakapotea, akajinyanyua kutoka pale alipo, akasimama wima, akatazama wale jamaa waliolala pale, waliotupwa na kwa kipigo kikali na Kamanda Amata. Akawapekua katika nguo zao na kupata bastola moja iliyobakiwa na risasi mbili tu, ‘Sio mbaya’ akajisemea.

Sasa kazi ilikuwa atatokaje kwenye chumba kile kisicho hata na dirisha, aliuangalia mlango ulikuwa juu umbali wa mita kumi na ukuta wote ulikuwa umewekwa kitu kama niru ambayo kamwe huwezi kuzikwea kwa jinsi zinavyoteleza, ulikuwa mtihani mgumu kwake, akakizunguka kile chumba akigusa hapa na pale, baada ya kuchunguza sana ndipo alipogundua ile sehemu ya kuingizi maji ndfani ya chumba kile, haikuwa na bomba bali ni uwazi mwembamba wa futi mbili kwa upana na uwazi wake ulikuwa ni kama milimita tano, palitengenezwa hivyo ili maji yakitoka yatoke kwa mbinyo na kasi kubwa kutokana na msukumo wa pampu.

Akapaangalia na kuona kama anaweza kupita katika upenyo huo, lilikuwa ni wazo finyu sana hata kama angekuwa motto mdogo, sehemu ambayo asingeweza kupenya hata mjusi, lakini yeye alidhamiria kupenya hapo, akiwa kama aliyechanganyikiwa ndipo akagundua kuwa haiwezekani kufanya hilo analotaka kufanya, akajicheke mwenyewe hasa alipojua kuwa yale maji kuna yanapokwenda, akaenda kwenye moja ya kona za chumba hicho, alipotazama kwa makini sana akaona kuna kitu kama kimebandikwa katika ukuta huo, lakini kilikuwa kimefanana sana na ule ukuta, akajua kwa vyovyote hapo pana kitu, akaanza kugongagonga ukuta kwa ile bastola aliofika eneo hilo akasiki ule mlio unabadilika na kuwa mkubwa kiasi akagundua kuwa nyuma yake lazima kuna uwazi, hakuwa na budi, kwa kutumia bastola hiyo hiyo alifyatua risasi moja na ikatengeneza tundu zuri ambalo lilimuwezesha kuona mpaka upande wa pili.

Kweli kulikuwa na uwazi mkubwa, Frank alisikia sauti ya maji yanayotembea, lakini alipochungulia kwa jicho lake aliona mwanga hafifu sana, akaanza kubomoa lile eneo kwa kupiga na ile bastola kama nyundo mpaka akafanikiwa kutengeneza tundu la kutosha, akajipenyeza na kudondokea kwa ndani. Lilikuwa ni bomba kubwa la maji taka, aliweza kutembea kwa kuinama kidogo huku akipita kwenye maji hayo na asijue ni wapi anaelekea, harufu iliyokuwa humo haikuwa tatizo kwake, alitembea mwendo mrefu kidogo, kwa mbele akaona kuna pacha ya bomba hilo ikiungana na bomba linguine ambalo nalo lilikuwa likileta maji kuunga na hili nkisha kuelekea yanakokwenda, Frank alipoifikia ile pacha akasikia kelele ya mtu anayekimbia katika maji, akatul.ia kusibri aone mtu huyo ni nani.

§§§§§

KAMANDA Amata alipoona kuwa lile lango la kwenda chini alikoingia Bill limejifunga,

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni