MAUAJI YA KASISI (6)
Jina: MAUAJI YA KASISI Mtunzi: Richard Mwambe SEHEMU YA SITA ILIPOISHIA... na muda huohuo alijipenyeza tena kuelekea upande mwingine ndipo alipogongana kikumbo na sajenti Maria ambaye kwa uzoefu wake wa kazi ya kipolisi alikuwa tayari amekwisha mpekua kwa kumgusagusa. “Dada, we vipi? Mbona unagonga watu ovyo, huoni njia?” yule dada aliuliza “Samahani nilikuwa nasoma saa hata sikukuona, samahani sana” JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... sajenti Maria aliomba radhi, kila mtu aliyekuwa pale aliawaangalia wanawake hawa. Sajenti Maria alikua amehisi kitu kigumu katika ubavu wa kushoto wa mwanadada yule na kwa uzoefu wake aligundua kuwa yule dada amehifadhi bastola katika ubavu wake, aliishusha saa yake machoni na kutazama kama picha aliyoipiga imetoka vizuri, akaridhika nayo kisha akajiondoa na kurudi garini. “Vipi?” koplo Otho’ aliuliza “Ah, clear, nina wasiwasi na yule dada, kwanza inaonekana ana bastola kiunoni…