
Mtunzi: Richard Mwambe
SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
na muda huohuo alijipenyeza tena kuelekea upande mwingine ndipo alipogongana kikumbo na sajenti Maria ambaye kwa uzoefu wake wa kazi ya kipolisi alikuwa tayari amekwisha mpekua kwa kumgusagusa.
“Dada, we vipi? Mbona unagonga watu ovyo, huoni njia?” yule dada aliuliza
“Samahani nilikuwa nasoma saa hata sikukuona, samahani sana”
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
sajenti Maria aliomba radhi, kila mtu aliyekuwa pale aliawaangalia wanawake hawa. Sajenti Maria alikua amehisi kitu kigumu katika ubavu wa kushoto wa mwanadada yule na kwa uzoefu wake aligundua kuwa yule dada amehifadhi bastola katika ubavu wake, aliishusha saa yake machoni na kutazama kama picha aliyoipiga imetoka vizuri, akaridhika nayo kisha akajiondoa na kurudi garini.
“Vipi?” koplo Otho’ aliuliza
“Ah, clear, nina wasiwasi na yule dada, kwanza inaonekana ana bastola kiunoni mwake” Maria alijibu
“Tumsubiri?”
“Haina haja lumsubiri, huyo hapo anakuja, hakikisha hatumpotezi kwenye sight yetu.”
Yule mwanadada alitoka getini na kupinda kushoto kwenye maegesho ya magari na kuingia kwenye moja ya magari yaliyopo hapo, na gari ile taratibu iliyaacha maegesho yale kuingia barabarani kuelekea upande wa Westland. Koplo Otho’ naye aliiondosha gari yao aina ya Peugeot 308, gari ya kisasa kutoka Uingereza, baada ya dakika kadhaa waikuwa kwenye foleni kubwa za Nairobi lakini macho yao yalikuwa makini kuitazama gari aliyopanda mwanadada yule isipotee. Kwa mwendo wa taratibu walikuwa katika barabara ya Mombasa kisha wakaiacha ile iendayo Nairobi central na wao kuifuata ile gari aliyokuwa sasa imekamata barabara ya Waiyaki kuelekea Westland, baada ya mwendo kidogo ile gari ilikunja kulia na kufuata barabara ya vumbi iliyoingia katikati ya nyumba zilizojengwa kwa mpangilio mahsusi kama quarter za shirika Fulani, Otho’ nae aliingia na gari yake kuifuata, sasa ailibaki gari mbili tu mbele aliyopanda yule dada na nyuma ya kina koplo Otho’ na sajenti Maria…
Otho’ aliegesha gari yake mbele kidogo karibu na duka kubwa lililokuwa likiuza bidhaa muhimu kwa binadamu. Sajenti Maria alishuka kutoka katika gari na kutembea taratibu kuelekea kule aliko yule mwanadada, Otho’ alibaki kwenye gari akiangalia kwa mbali tukio hilo. Yule mwanadada aliongeza mwendo kidogo alipogundua kuwa anafuatwa, alitembea huku akitoa simu yake ya mkononi na kuongea na mtu Fulani, sajenti Maria aliona tayari kagundulika kama anamfuata huyo mwanadada, na yeye alitoa simu yake na kwasiliana na Otho’ ili amlinde katika hilo. Otho’ aliiacha gari pale dukani na kufuata ule mtaa kama mtu aliye na shughuli nyingine kabisa, kwa mbali alimuona sajenti Maria kasimama akitazamana na yule mwanadada, kati yao kulikuwa na nafasi kama ya mita mia moja hivi, Otho’ alimpita sajent Maria na kumsalimu kama hamjui huku akiendelea upande ule aliko yule mwanadada na alipomfikia alimsalimu vilevile na kuendelea na safari yake na kumpita yule mwanadada, baada ya mwendo kama wa mita hamsini alikunja kona na kusimama kuona nini kinaendelea.
Sajenti Maria alibaki akitazamana na yule mwanadada kila mmoja akiwa na simu mkononi, mara nyuma ya Sajenti Maria ulisikika mlio wa pikipiki, Sajenti Maria alipogeuka nyuma kuipisha pikipiki ile alichelewa, dereva wa ile pikipiki alimgonga Maria na kumuangusha chini, sajenti Maria alijaribu kujiinua lakini kabla hajakamilisha zoezi hilo aligongwa tena eneo la mbavu na kuanguka chini, kisha yule muendesha pikipiki aliteremka na kuiegesha ile pikipiki huku ikiwa inanguruma na taratibu alimfuata sajenti Maria pale chini, alimtazama kwa dharau na kupandisha juu kile kioo cha kofia ngumu aliyoivaa.
“Wewe ndiyo unajua kufatilia nyendo za watu siyo?” alimuuliza huku akimsogele karibu zaidi. Sajenti Maria alimwangalia kwa hasira mpaka uso wake ulipoteza kabisa ile haiba ya uanamke, yule jamaa alipomkaribia alichuchumaa ili kumsaili vizuri sajenti Maria, kwa kushtukiza sajenti Maria alirusha teke la nguvu lililotua katikati ya mapaja ya yule jamaa na kupiga sawasawa sehemu zake za siri, yule jamaa kabla hajajielewa teke lingine lilitua upande wa kulia wa shingo yake na kumpeleka chini, sajenti Maria alijiinua kwa haraka na kusimama kidete na kumuacha yule jamaa akiwa chini. Yule mwanadada alipoona mchezo ule wa kiufundi kutoka kwa sajenti Maria aligeuka ili apotee eneo lile, lakini hamad alijikuta akitazamana uso kwa uso na bastola ya Othorong’ong’o, alisimama ghafla na kujikuta hana la kufanya, Otho’ akatoa pingu zilizokuwa mifukoni mwake ili kumfunga yule mwanadada.
“Weka mikono yako nyuma!” alimuamuru ili amfunge pingu hizo, yule mwanadada akaishikanisha mikono yake nyuma ya mgongo akiwa anatazamana na Otho.
“Geuka” Otho alimuamuru, na yule mwanadada aligeuka na mkononi mwake tayari alikuwa na bastola amabayo aliificha upande wa nyuma kwenye sketi yake, aligeuka na kufyatua risasi iliyoenda na kupiga mguu wa Otho, yowe la maumivu lilimtoka Otho huku akiiachia bastola yake ikidondoka chini, sajenti Maria alichanganyikiwa afanye nini akiwa bado katika kuhamaki pikipiki nyingine ilitokea nyuma ya Otho na yule mwanadada akaidandia katika kiti cha nyuma, sajenti Maria alirusha risasi kwa bastola yake lakini hakuweza kupata shabaha nzuri kwani ile pikipiki ilikuwa imekwishakunja kona na kumuacha Otho akiwa chini mguu ukivuja damu, aligeuka kumwangalia yule mwenye pikipiki ya kwanza lakini hakumuona pale badala yake watu walianza kujaa eneo lile, sajenti Maria akavua shati lake alilovaa juu na kumfunga koplo Otho jeraha lake ili kuzifanya damu zisiendelee kumwagika kisha akajitahidi kumyanyua kutoka pale chini akisaidiwa na watu wachache walifanikiwa kumfikisha kwenye gari, sajenti Maria aliwasha gari na kuondoka eneo lile.
Siku mbili
kabla ya mauaji ya Fr Gichuru
Mtawa wa kike alikuwa amesimama katika kituo cha matatu akisubiri usafiri kuelekea mjini, kila mara alionekana akiiangalia simu yake, huku akiwa na kikapu mkononi alionekana kama anayekwenda sokoni. Mara gari moja Land Rover Defender ilikuwa ikitoka katika geti la kanisa hilo na kukunja kulia kuelekea mjini, ikasimama jirani kabisa na mtawa yule.
“Sista, twende nikusaidie” ilikuwa ni sauti ya Fr Gichuru akimpa lifti yule mtawa, alipokwishakuketi sawia kitini waliondoka kuelekea upande wa mjini na Fr gichuru alianzisha maongezi.
“Sista safari ya wapi saa hii?”
“Nakwenda Kileleshwa estate, kusalimia jamaa kwani leo nina ruhusa kutoka kwa mama mkuu” yule mtawa alijibu.
“Ooh, vizuri kuwatembelea ndugu siku mojamoja” Fr Gichuru alimueleza huku akiwa anakaribia katikati ya jiji la Nairobi
“Ila kwanza nataka kwenda pale shule ya msingi Nairobi, ningeshukuru kama unganisaidia kufika pale maana usafiri wa kwenda kule ni mgumu” yule mtawa aliomba huku akimlegezea macho Fr Gichuru. Siku zote kumnyima mwanamke ombi lake siyo rahisi sana, Fr Gichuru aliiacha barabara kubwa na kuufuata barabara ndogo inayopita katika majumba ya watu kuelekea huko shule ya msingi, alipoyamaliza majumba na kuteremka kibonde kidogo kuliendea daraja ili kuvuka na kutokea upande wa pili, alikuta mtu aliyeanguka na pikipiki.
“Oh God!” yule sista alihamaki, Fr Gichuru akasimamisha gari akataka kushuka kwenda kumsaidia yule jamaa aliyeanguka.
“No usiende Fr ni hatari, huwezi jua nini kilichopo huko chini” Sista alimbembeleza Fr Gichuru, lakini haikuwa rahisi kwani moyo wa huruma wa kikasisi ulimsukuma kushuka.
“Hapo hapo ulipo tulia” sauti ilitoka nyuma ya gari yake, alipogeuka alikutana na mtu aliyeshika bastola akimnyooshea yeye.
“Nini tena jamani? Mbona sielewi kinachoendelea?” Fr Gichuru alilalamika
“Tulikuwa tunakusubiri wewe na tunashukuru huyo sista wako amekuleta mahali pema peponi” yule jambazi alizungumza, “Haya haraka ingia katika gari iyohiyo siti ya nyuma” aliamuriwa, na bila kubisha alijipakia ndani yake na nyuma ya usukani yule mtawa aliyepewa lifti alikuwa tayari nyuma ya usukani kwa kuondoka.
“Ha! Sista!” Fr Gichuru alipigwa na mshangao alipomkuta yule sista tayari ameketi kwenye usukani.
“Aliyekwambia mi sista ni nani!?” alijibu yule mtawa huku akitoa kilemba chake kichwani na kuruhusu rasta zake ndefu kumwagika mabegani “Mimi nilikuwa nakutafuta wewe, naitwa kahaba Rose” alijitambulisha. Fr Gichuru alivalishwa soksi usoni ili asione anapopelekwa na safari ilianza. Mwendo wa muda kadhaa waliisimamisha ile gari na kumshusha Fr Gichuru kisha wakachukua gari nyingine na kuitelekeza ile ya mission palepale eneo la Madaraka estate pembeni mwa barabara ya Mbagathy, kisha wao wakaendelea na safari yao kuelekea barabara ya Mombasa na mpaka karibu na kiwanda cha saruji cha Bamburi na kupinda kushoto kuelekea kwenye eneo la viwanda, moja kwa moja waliingia kwenye godown kubwa na kumteremsha Fr Gichuru.
Ndani ya chumba kidogo chenye vikorokoro vingi walimuhifadhi akiwa amefungwa kamba kwa nyuma.
Yule mwanamke aliyejifanya mtawa alimvua ile soksi usoni na kumuacha huru akiweza kuona kwa mbali kutokana na giza lililotanda ndani humo.
* * *
“Kazi uliyonituma nimeimaliza, nipe changu” Rose alimwambia mtu mnene walipokutana tena katika chumba chao kilekile katika Plazza Hotel.
“Usijali, mzigo wako upon a asante kwa kazi nzuri, lakini ole wako uitoe siri hii, nakuua” Bill mtu mnene alimpatia pesa nyingi kahaba Rose na kuagana nae.
“Asante Bill” alishukuru huku akitoa machozi, machozi yenye pande mbili, furaha ya kukamata pesa nyingi ambazo hajawahi kuzishika maishani, na uchungu wa kumsaliti kasisi asiye na hatia. Alitoka na kubamiza mlango nyuma yake, moja kwa moja akaiendea lifti na kuteremka chini kabla ya kupotelea mitaani.
Bill akiwa na swahiba zake waliingia katika gari aina ya hammer na kuelekea kumuona mateka wao mioyoni mwao wakijua kazi imekwisha.
Ukimya ulitawala katika lile godown isipokuwa kweny kijichumba kimoja kimoja tu ambako Fr Gichuru alikuwa akisali kwa kilatini kwa sauti tulivu ambayo kama ungekuwa karibu na dirisha lake ungeisikia vizuri tu.
Mara mlango ulifunguliwa kwa ghafla na watu sita waliingia ndani ya kijichumba kile. Fr Gichuru aliendelea na sala yake kana kwamba hakuna mtu aliyeingia humo ndani.
“Mmmh Sali sana tu mpaka milango ifunguke!” sauti hiyo ilimshtua Fr Gichuru na kuinua macho yake juu na kugongana na yale ya ya Bill mtu mnene
“Bill!” aliita kwa mshangao
“Unashangaa nini? Habari za Roma?” Bill alimuuliza Fr Gichuru
“Nzuri tu, habari za ulikokwenda”
“Salama tu Fr, leo tumeonana tena, sina mazungumzo mengi na wewe leo ila ninachohitaji ni ile Monstrance, tuambie ilipo tukaichukue usiku huu kisha tutakuachia huru, mimi sipendi kumwaga damu isiyo na hatia kama yako Reverent Father Frederick Gichuru”
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi