Mtunzi: Latifa
SEHEMU YA KUMI NA NANE
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
"Daktari Daktari amefumbua macho"
Nilisikia sauti ya mwanamke ikisema ivyo sikuelewa anamaanisha nini.
Mara nikamuona mwanaume amevaa koti kubwa akaja nakunisogelea.
KAMA UNAISOMA SIMULIZI HII TOFAUTI NA KWENYE APP YA CnZ Media
IPAKUE ILI KUPATA SIMULIZI KWA WAKATI SAHIHI
IPAKUE ILI KUPATA SIMULIZI KWA WAKATI SAHIHI
👉GUSA INSTALL👈
ENDELEA...
"Vipi unaendeleaje upo salama?"
Aliniuliza
"Yani wewe unaacha kuuza nyama unanifata mimi unataka kunichinja eeeh si nakuuliza?"
Nilinyanyuka mzima mzima nikamvuta shati uyo mwanaume nakumkunja nimpige.
Yule mwanamke mwengine kuona ivyo akatoka mbio nje kuita watu waje kumsaidia.
Muda huo huo wakaja Vitalis na wazazi wangu ambao walishangaa purukushani inayoendelea ikabidi wasaidiane kunituliza kulikuwa na machuma kwenye iko kitanda nikafungwa mikono na miguu nisisumbue baada ya apo nikachomwa sindano ya usingizi nipumzike.
Kila alieniona alinihurumia na mimba yangu nilikuwa kichaa ambacho akikujulikana imekuwaje nimekipata walijua labda kichaa cha mimba lakini haikuwa ivyo, Mamangu alilia sana asiamini mwanae akili zimeruka.
"Lisa mwanangu umekuwaje mama jamani na mjukuu wangu atapona kweli?"
Alilia sana mama akinionea huruma.
Macho ya Vitalis yalikuwa mekundu kwa kulia nilikuwa na wiki mbili sijaamka kitandani Leo ndo nimeamka nakuwa kichaa hudhuni iliwajaa wote ndugu zangu walipata taarifa nakuja hospital kila alieniona machozi yalimtoka kilicho wahudhunisha ni mimba yangu nilitia huruma sana.
Wiki ikaisha bado hali yangu ni mbaya akili azijarudi madaktari walijitaidi kunitibia lakini ikawa ni bure sikuweza kuwa sawa mwisho wakashauri nirudishwe nyumbani sababu wao walishindwa.
Akukuwa na laziada ikabidi nirudishwe tu nyumbani kwa wazazi wangu baba ndio alitaka ivyo nisiende kwa Mumewangu.
Nyumba haikukalika vurugu tupu mikawa nafungiwa mlango nisiweze kutoka nje.
Hakuna alieweza kukaa karibu namimi nilikuwa mkorofi sana anaenisogelea nampiga.
Miezi ilizidi kusonga ikafika mimba ikikua tu adi miezi tisa ikafika sijapona bado kichaa
"Mungu wangu atajifunguaje mwanangu jamani?
Mama alisema kwa hudhuni akilia
"Usijali mama Mungu atasaidia tu"
Aliongea Vitalis japo nayeye moyo wake ulikuwa unamuuma sana.
"Ata siamini mwanangu alikuwa mzima leo hii ni kichaa kawakosea nini mwanangu adi mumfanye ivi jamani?"
Alizidi kulalamika Mama
"Mama Lisa basi nyamaza yote ni mitihani ya dunia"
"Sio kweli wamemloga mwanangu"
"Acha imani zakishirikina"
Walikuwa wanaongea Baba na Mama
"Lakini mnaonaje tukampeleka kanisani aombewe"
Alishauri Vitalis
"Bora kanisani kuliko kuwaza mambo ya kishirikina"
Baba akasema lakini tatizo likaja watanipelekaje uko kanisani ikabidi watafute mchungaji aje kuniombea nyumbani.
***
Baba ndie alitafuta mchungaji nakulemleta nyumbani ambapo maombi yalifanyika mlangoni uku mimi nikiwa chumbani nimelala sababu ya vurugu zangu akuna alieweza kuingia ndani nilikuwa na nguvu za ajabu, Mchungaji aliomba apo adi akachoka nakuondoka akuna kilichobadirika uchizi ndo uliongezeka.
Huo ulikuwa mwanzo wa watumishi wa mungu kuja nyumbani wengi wakawa wanakuja nakuniombea lakini hali yangu haikubadirika.
Vitalis aliamia nyumbani kazini alimuacha Secretary aliekuwa anasimamia, Mara chache alikuwa akienda ila muda mwingi aliutumia kuwa nyumbani kwetu alikosa raha hali yangu ilimfanya akose usingizi aliangaika sana kuleta wachungaji kuja kuniombea lakini haikusaidia kitu bado akukata tamaa aliamini ipo siku Mungu atasikia kilio chake mkewake atapona ndugu walichachamaa kumpeleka kwa Mganga lakini Baba alikataa ataki nipelekwe.
"Mwanangu anateseka tumpelekeni tu jamani labda watasaidia hao waganga"
Alisema Mama
"Ivi unakumbuka Lisa alivyoangaika kwa waganga kutafuta mtoto iyo mimba aliipata au waganga ni binadamu kama sisi ila mwenye uwezo ni Mwenyezi Mungu pekeyake msiniletee ujinga apa hii mimba Mungu ndo kafanya aipate nayeye ndie anajua Lisa atajifunguaje acheni imani potofu mwanangu sitaki apelekwe kwa waganga"
Alisema Baba na huo ndo ukawa msimamo wake nilibaki nyumbani uku wakija wachungaji kuniombea kilasiku japo mafanikio ayakuonekana lakini Vitalis akuchoka kunisaidia kila mtu alimsifu kwa moyowake akufunga ndoa namimi lakini alinipenda nakuniona tayari ni mkewake zaidi akutaka kunitelekeza aliniitaji sana ni mwanaume wa pekee.
Siku zilizidi kusonga uku mimba ikiwa kubwa.
Hatimae siku yakujifungua ikafika sasa uchungu ulinishika usiku sikulala adi kunakucha alivyo Mungu wa ajabu sasa sikufanya fujo kabisa siku iyo kila mtu alishangaa
Usiku tumbo lilianza kuniuma nikapiga kelele kumuita Mama ambae akuogopa alikuja chumbani kwangu uku wengine wakibaki mlangoni kuangalia kunanini.
"Mama tumbo linauma"
Nilimwambia
"Pole mwanangu linauma sana na kiuno je akiumi?"
Aliniuliza uku anajifuta machozi
"Kinauma alafu uku kunatoka nini sijui"
Nilimwambia nikimaanisha sehemu za siri waliojifungua wanajua dalili za mwanamke anaeumwa uchungu inakuwaje basi Mama akaaniangalia nakujua nipo karibu kujifungua ilikuwa usiku saa tano akabaki namimi adi kunakucha Asubuhi wakaniwaisha hospital binafsi. Kila mtu alikuwa kimya kwenye gari kasoro mimi niliekuwa naugulia maumivu adi tulipofika hospital nikaingizwa ndani nakupewa kitanda Daktari akanipima nakuonekana mtoto yupo karibu akaanza kunielekeza nisukume
"Naumia inauma Mamaaa njoo muone uyu ananifanyaje"
Nikaanza kulia nikimuita mama ambae ilimbidi aingie ndani nakumueleza Daktari Mimi akili zimeruka ulikuwa mtihani kwenye kusukuma uchizi ulianza upya
"Tanua miguu utaua mtoto"
Alisema Daktari
"Sitakii niache sitaki mimi"
Nilikuwa napiga kelele miguu nimebana na mtoto yupo karibu ilikuwa kazi sana wakaja na manesi kunishikilia Mama alikosa ujasiri wakujizuia aliangua kilio nakutoka nje ambapo alikutana na ndugu wengine adi Vitalis alikuwepo
"Kunanini mbona unalia?"
Aliuliza Baba
"Uchizi umemludia nilijua mwanangu amepona ataki kusukuma mtoto yupo karibu anabana miguu"
Alisema Mama akilia sana.
"Mama basi wamfanyie upasuaji"
Vitalis alisema
"Haiwezekani tumechelewa mtoto yupo mlangoni kabisa"
Mama aliongea kila mtu alichoka wakabaki na mawazo wakisubiri miujiza itendeke.
Mara ghafla wakasikia mtoto mchanga akilia humo ndani alipokuwepo Lisa hawakuamini ikabidi Mama aingie nakumkuta Lisa amelala uku kitoto kinasafishwa alipiga magoti chini nakumshukuru Mungu sana kumsaidia mwanae ameweza kujifungua salama.
"Daktari mtoto gan uyo?"
"Wa kiume Mama"
"Ooh asante Mungu"
Alisema Mama baada ya kumsafisha mtoto alipewa amshike na wengine pia wakaruhusiwa kuingia ndani nakumuona mtoto Vitalis akijikuta machozi yanamtoka alipomshika mwanae alifanana nae kilakitu zaidi nywele mtoto alikuwa na nywele nyingi nyeusi kama Babayake alifarijika sana kupata mrithi wake.
"Nakupenda sana mkewangu"
Alinisogelea nilipolala nakunibusu.
"Daktari vipi kuhusu uyu mama mtoto?
Aliuliza Baba
"Mmmh ni mtihani sana tumepata kazi kubwa adi amejifungua tumshukuru Mungu pia amepoteza fahamu akuwa na nguvu nyingi msijali baada ya masaa machache ataamka tu lakini akili yake bado Mungu amsaidie"
Alisema Daktari akitoa leso nakujifuta machozi ata yeye hali yangu ilimgusa sana.
Mtoto wakaruhusiwa kumchukua warudi nae nyumbani sababu kumuacha na Mamayake ambae si mzima angeweza kumsababishia matatizo ivyo wakarudi nae nyumbani nakumpa Maziwa ya Nido.
Wiki moja ikapita bila kuamka kitandani hudhuni ikatawala kwa kila mtu matumaini yakupona ayakuonekana watu walilia mwisho wakachoka nakusubiri miujiza nipone au nife wanizike.
"Naamini Mungu atakusaidia utapona mkewangu"
Alisema Vitalis japo dalili azikuonekana zakupona lakini alijipa imani.
Mwezi mmoja ukakatika uku mtoto akiendelea vizuri mwenye afya yake lakini Mama bado yupo kitandani nusu mfu.
****
Marko Raphael ni mchungaji wa kanisa la Ushindi lililokuwepo magomeni ni kijana mdogo mwenye miaka Therathini alianza kumtumikia Mungu tangu akiwa na miaka kumi na tano alikuwa na imani sana akiomba nakufunga maisha yake yote aliishi kwenye wokovu.
Alibahatika kuoa mwanamke mzuri ambae ni mtumishi wa Mungu aitwae Diana maisha yao yalikuwa yakumcha Mungu nakumpendeza kwa kila jambo.
Siku moja walienda hospital kumpeleka mamayake Diana ambae alikuwa mgonjwa anasumbuliwa na miguu pia ni mtu mzima umri umeenda sana.
Walifika St Mathieu Hospital iliyokuwa maeneo ya Segerea sababu wao wanaishi kinyerezi waliingia ndani mgonjwa akapokelewa nakuingizwa kwenye chumba akipata matibabu.
Marko na mkewe Diana walikuwa kwenye viti wamekaa ambapo ghafla wakamuona mamayangu akiwa anatoka kwenye chumba nilichokuwepo uku akilia kwa uchungu
"Mwanangu weee umekufa unaniacha na nani mimi mamaa oooohhh"
Alikuwa ajiwezi alilia sana adi kukaa chini Mara akatoka Baba nakjmshika mkewe akimtuliza lakini ilikuwa bure Mama alizidi kulia.
Vitalis alikaa kwenye kiti uku kajiinamia macho yote ni mekundu.
Diana aliwahi kuinuka nakuja alipo Mama kumbembeleza ambapo Marko yeye alimfuata Baba akamsalimia nakumuuliza kunanini
"Binti yangu ambae alikuwa kichaa amefariki"
Alisema Baba kwa hudhuni
"Poleni sana naomba niingie ndani kumuona"
Alisema Marko wote wakashangaa ila mwisho wakamruhusu kuingia ambapo alisogea adi kitandani nilipokuwa nimelazwa nakufunikwa shuka la kijani.
"Uyu binti ni mzima ajafariki"
Alisema wote wakashtuka nakumshangaa
"Daktari katoka apa sasa ivi kumpima amefariki we unasemaje ni mzima au umevuta bangi naomba ondoka acha maiti ya mwanangu"
Baba alichukia nakusema kwa hasira ata Mama aliacha kulia nakustaajabu kusikia mwanae mzima ajafa kama alivyoseka Daktari.
"Naitwa Mchungaji Marko Raphael na uyo apo ni mkewangu roho wa Mungu amenileta apa hospital ili nimsaidie uyu binti nilionyeshwa
maono usiku nilipolala kuhusu uyu Msichana naamini Mungu atamponya ni mzima ajafariki."
Alisema akutaka kusikia maneno tena alichokifanya ni kumsogelea Lisa kitandani nakuanza maombi akuwa kama watumishi wengine wanaopiga makelele yeye alikuwa kimya midomo tu ndo inacheza ambayo uwezi kujua neno analosema ata kwa vitendo alikuwa akinena kwa lugha.
Dakika chache tu Lisa akaanza kutingishika akirusha mikono na miguu
"Niacheee naunguaaa sitakiii niacheee"
Alianza kuongea akipiga kelele zilizowastua madokta ambao walikuja nakushangaa maiti inaongea.
"Eleza nani kakutuma uje kumuua uyu binti?"
Ni Diana ndie aliuliza uku mumewake akiwa bado anaendelea na maombi
USIKOSE MWENDELEZO
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi