MREMBO MCHARUKO (19)

Zephiline F Ezekiel
Mtunzi: Latifa

SEHEMU YA KUMI NA TISA
ILIPOISHIA...
Alianza kuongea akipiga kelele zilizowastua madokta ambao walikuja nakushangaa maiti inaongea.

"Eleza nani kakutuma uje kumuua uyu binti?"

Ni Diana ndie aliuliza uku mumewake akiwa bado anaendelea na maombi

KAMA UNAISOMA SIMULIZI HII TOFAUTI NA KWENYE APP YA CnZ Media
IPAKUE ILI KUPATA SIMULIZI KWA WAKATI SAHIHI
👉GUSA INSTALL👈

ENDELEA...
"Ni Neema na Harvey ndio wamenituma nimuue Lisa na mtoto wake"

Ilijibu sauti ya kiume iliyokuwa ikiongea kwenye mwili wa Lisa.

Yalikuwa kama maigizo wote walioshuhudia hawakuamini.

"Mama unawajua hao watu?"

Vitalis aliuliza

"Nawajua ni yule mwanaume aliekuwa mumewake Lisa na uyo Neema ni mamayake mdogo"

Alisema Mama nakumfanya Vitalis hasira zimpande

"Haiwezekani kumbe wao ndio wanamtesa ivi mkewangu lazima walipe kwa aya waliyofanya"

Aliongea kwa uchungu ikabidi wamtulize kwanza waangalie hali yangu.

Maombi yaliendelea zaidi "Ninakuamuru urudi ukamuingilie uyo aliekutuma kuja uku"

"Naogopa wataniua"

Alijibu uyo jini

"Kumbe unaogopa kufa kwanini wewe unaua sasa basi nakuunguza na moto wa yesu uteketee apa "

Alisema Diana maombi yakazidi yule jini alipiga kelele sana mwisho akatoka nakumuacha huru Lisa maombi ya shukrani yakafanyika baada ya muda mfupi Lisa akafumbua macho.

"Mumewangu sijaumia nilivyoanguka chooni?"

Ndio neno la kwanza kuongea bila kujua ni zaidi ya miezi sita nipo kitandani nikiwa chizi.

Kila aliekuwepo humo ndani akuamini kama nimeweza kuamka nakuongea. Mama alinisogelea uku akilia nakunikumbatia

"Lisa mwanangu umepona ooh asante mungu"

Alisema

"Mama usijali sikuumia sana nilidondoka tu chooni"

Nilimjibu uku nikipeleka mkono nakujishika tumbo langu nikashtuka sina mimba.

"Mungu wangu mimba yangu imetoka Mamaaa mwananguuuuuuuu"

Nikaangua kilio kwa nguvu kilichowashtua wengi.

"Lisa mimba haijatoka tayali umejifungua"

Alisema Vitalis nakunieleza yote yaliyotokea sikuamini.

"Haiwezekani mimi nilikuwa chizi? Eeh jamani binadamu wabaya niliwakosea nini mimi?"

Nilizidi kulia nikiudhunika sana sikuweza kuamini nililia kwa uchungu nakuwapa kazi kunibembeleza.

Mwisho nikaletewa mwanangu nimuone nilimuonea huruma tangu azaliwe ajanyonya maziwa ya Mama adi sasa mwezi mzima umepita.

Kwasababu nilikuwa mzima siku iyo iyo nikaruhusiwa kurudi nyumbani.

Ndugu walipata habari wakaja kuniona nakunipa pole kwa yaliyonikuta.

Hatimae nikamaliza wiki moja hali yangu ikiendelea vizuri.

"Lisa muda wakufunga ndoa umefika sasa"

Alisema Vitalis

"Apana bwana bado"

"Nini we usinitanie nimevumilia sana huu ndo wakati wakuishi na familia yangu"

Alisema akaenda kuongea na wazazi wangu waliokubali mipango ikaanza hatimae ndoa ikapita tukaanza kuishi pamoja mume na mke.

Ndoa yetu ilikuwa ya furaha na amani japo kukosana kawaida kupo kwa wanandoa.

Mtoto wetu wa kiume tulimuita Brian hatimae akatimiza miaka miwili ilikuwa furaha sana kwetu. Baada ya miezi michache nikashika ujauzito ambao nilipimwa nakuonekana ni mapacha watatu.

Siku moja tukiwa tunaelekea hospital njiani tukamuona yule mamayake mdogo Neema amekuwa kichaa

"Mungu kamlipa kwa mabaya yake"

Alisema mumewangu mi ata kuongea nilishindwa machozi ya uchungu yalinitoka.

****

Harvey aliendelea na tabia yake yakubadirisha wanawake kilasiku lakini akuna ata mmoja aliewahi kumwambia anamimba yake kibaya zaidi akuwa akitumia kinga. Siku moja Babayake akiwa safarini ndege aliyopanda ilidondoka nakufariki apo apo, Mamayake alipopata taharifa ya kifo cha mumewake alipandwa na presha nakupelekea mauti yake.

Mali zote zikabaki chini ya Harvey aliezidisha ulevi nakulala ovyo na wanawake adi pale hali yake ilipokuwa mbaya alianza kuumwa nakutoka vipele mwilini alipoenda kupima akajulikana ni Muathirika wa ukimwi alilia sana nakujuta kwa yote aliyofanya ila akuweza kubadirisha ukweli akazidisha ulevi nakuacha kutumia dawa hali yake ilizidi kuwa mbaya pesa zote alitumia adi nyumba akauza alikosa sehemu yakuishi nakuanza kuzunguka mitaani kama kichaa akuwa yule Harvey handsome boy alichoka nakuwa kama kinyago mwili mzima alikuwa ananuka watu awakumsogelea karibu yake alitia kinyaa.

Siku moja alivuka barabara bila kuangalia kutokana na msongo wa mawazo alionao gari likamgonga nakufariki apo apo huo ndo ukawa mwisho wa Harvey.

***

Siku ya maombi hospital yule jini aliekuwa kwenye mwili wa Lisa alitolewa nakurudi kwa Neema ambae ndie alienda kwa mganga ili amtie uchizi Lisa mwisho afe na mimba yake. Jini linatumiwa kuua sababu kashindwa kumuua Lisa lazima arudi kwa aliemtaka Neema aliogopa kurudi kwa Mganga kwani angeuliwa yeye alipotolewa akaenda kumvaa Neema ambae alikuwa Lodge na mwanaume wa mtu akiwa uchi uchizi ukamuanza apo akatoka nje uku anapiga kelele nakukimbia ovyo kila aliemfahamu alipomuona alimshangaa amekuwaje ila kuna waliomsikitikia pia wapo walioona ni bora yalivyomkuta.

Uchizi wake uliendelea zaidi ya mwaka mmoja akupata mtu wakumsaidia adi pale siku moja alipokutwa amekufa na mwili wake kutoa harufu kali akazikwa na manispaa ya jiji la Dar es salaam huo ndo ukawa mwisho wa Neema mchina Shangingi aliekubuhu sana ambae akujua dunia ni mapito alizani ataishi milele.

**

Lisa alifanikiwa kujifungua salama watoto wake mapacha ambao wawili wa kike na mmoja wakiume.

Maisha ya furaha yakatawala ndoa yake na kilakitu kikabaki historia.

MWISHO

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni