
SEHEMU YA KUMI
ILIPOISHIA...
Cathy alimfuata jasson akamweleza kuhusu ule mpango..Jason alikubal maana alijua hyo ndio njia rahis ya kumpata eva..
SASA ENDELEA..
Cathy alifanikisha kuzipata picha ambazo eva alikua akiongea na mkufunz...alizipata nyingi maana mkufunz alipenda kumwita eva mara kwa mara....almtumia zote jasson ili .....afanye kaz yake..Kesho yake jasson alimpigia sim danny..
Danny...yan eva huku siku iz hashikiki....alisema jasson.
Una maana gan...aliulza danny kwa mshangao....
Yaan mm mwenyew siamin macho yangu...alisema jasson kiunafik..
Mbna sikuelew jasson?...
Najua itakuuma ila inabid nikwambie...mm mwenyw kama rafk yako inaniuma ila bas tu...
Eva anatoka na mkufunz sku iz....
Niniii??????...danny aliuliza kwa mshangao...
Ndo hvyo ndugu.....af unajua hawa wakufunz walivyo malaya....si ajab ana ukimwi...mm nakwambia nikuokoe danny....
Danny aliishiwa nguvu....hakuamin masikio yake...
Au n uongo??....ila jasson atanidanganya ili iweje??...alijiuliza maswal meng sana....alimwamin rafk yake jasson,,,hakutaka kuamin kama angemdanganya
Yan danny eva kabadilika sana...ngoja nikutumie picha zao..
Danny aliposikia picha alistuka sana...mda kidogo baada ya jasson kukata sim...danny aliona picha nying sana za mazingira tofaut tofaut za eva na mkufunz....
Danny hakula siku hyo...alikua analia sku nzima...mara sim ya eva ikaingia...
Danny alishindwa kujua apokee au la..baada ya kujishauri sana aliamua kupokea...
Eva...
Abeee....
Hivi et unatoka na mkufunz???
Eva alishangazwa na sana na swali lile....
Mbna umeuliza hvyo danny??.....
Nijib kwanza....alisisitiza danny...
Eva alikana...
Unakataa nn eva na wakat picha zenu nying ninazo hapa!!?....
Eva alishangaa kusikia habar za picha...
Danny alikata sim na kumtumia zile picha..
Eva alimpigia danny...
Inamaana huo ndo uthibitisho tosha??...kwahyo na ww umeamin???...aliulza eva..
Sasa ntafanya nn eva...eva mbna hvyo lakn??
Eva alishindwa kujua nan kamtumia hizo picha maana alipomuulza danny alikataa kumwambia..
Hata hvyo alihofia kumwambia danny kama mkufunz anamtaka kimapenz...alijua ndo angeharibu kabisa....
Alibak tu kulia mtoto wa watu....asijue cha kufanya..
============================================
Cathy na jasson walipongezana kwa kaz waliyofanya...waliwajulisha victor na rachel ambao nao pia walifurahi..
Waliendelea kumsingizia mambo meng sana eva kwa danny...
Taratibu danny alianza kupoteza iman na eva licha ya kuaalimpenda sana eva na hakua tayar kumwacha...
============================*****
Msongo wa mawazo ulipelekea eva kukonda sana....alimwita miriam na kumweleza (kama ilivyoelezwa katika sehem ya kwanza)..
Miriam alimtuliza rafk yake eva....
Eva alijua kua kwa vyovyote cathy atakua anahusika...hata hvyo hakuweza kumfuata maana hakua ana ushahd wowote..
Cathy alikua na nyodo sana baada ya kujiona kua amemuweza eva..
Sababu ya mawazo,,,eva aliuguua na alikonda pia.....
Miriam alimpeleka hospitali rafk yake..
Licha ya kua hawakua na maelewano,,,, lakn danny aliposikia kuuguakwa eva roho ilimuuma sana...
Alimtafta eva amjulie hali.....lakn kwa wakat huo eva alikua na hali mbaya...miriam rafik yake alipokea sm..
Unasemaje ww..alisema miriam kwa hasira akiamin kwamba danny ndo chanzo cha ugonjwa wa eva......
Umemsababishia haya yote halaf saiv unataka nn zaid...unataka afe kabisa???.....
Danny aliumizwa na kaul za miriam...roho ilimuuma sana.lakn hata hvyo hakukata tamaa...aliendelea kumjulia hali eva.....
Hatimay eva alipata nafuu....danny alimpigia sm...
Eva pole jaman....alisema danny..
Eva machoz yalikua yakimtoka tu mda wote...danny ilibid ambembeleze eva...alimuahid kwaba haitojirudia tena...
Sitaamin maneno yao tena sawa eva...usilie eva wangu...
Eva alifarijika akanyamaza...akawa na furaha tena...
==============================*****===*=**
Victor alimwita mke wake...
Nataka nifanye kitu...hapa itakua janja yetu ya mwisho.....tukishindwa hapa bas sijui kama tutaweza kuwatenganisha sku nyingne....alisema baba danny
Ni nn hcho mme wangu..aliulza rachel kwa shauku...
Naomba unitaftie namba za daktari anaemtibu eva...alisema victor
Mmh za nn???..aliulza mkewe..
USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA MOJA
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO