
SEHEMU YA TANO
ILIPOISHIA...
Eva alishangaa maana haikua kawaida ya Cathy kumchunia licha ya kua Cathy alikua mtu wamajivuno...hata hivyo alipuuzia akalala.SONGA NAYO...
Kadri siku zilivyozid kwenda cathy alizidi kumchukia eva...lakin eva wala hakujal wala hakumchukia cathy....Siku moja danny alishikwa na ugonjwa ghafla....alipelekwa hospitali na rafik yake peter akiwa tayar amepoteza faham..
Eva aliposikia habari za ugonjwa wa dabny alichanganyikiwa..akawaza sana.
Jaman, sijui kawaje,alijisemea eva huku machoz yakimlengalenga
Wazazi wa danny waliposikia habari ya ugonjwa wa mtoto wao walifunga safar mda huohuo nakuja hospital alipokua mtoto wao..
Hospitali haikua mbali sana na shule hvyo haikua kaz ngum kwa wanafunz kwenda kuwasalimia wenzao
Siku iliyofuata wazazi wa danny walikua tayari washafika....eva nae aliomba ruhusa ya kuja kumsalimia danny..
Mda huo na cathy alikua anajiandaa kuja baada ya kusikia ugonjwa wa danny
Eva alifika alipokua amelazwa danny.. Akawakuta wazazi wake,,akawasalimia...
Waliitikia kiunyonge sana eva yeye akazan kua ni sababu ya ugonjwa wa danny.....
Danny alikua hajazinduka bado...eva aliingiwa na hofu maana ni muda mrefu tangu danny azimie...
Eva unaweza tu kwenda nje kwanza maana sasaiv danny hajazinduka bado...alisema mama danny maana hakutaka kabisa danny nazinduke amkute eva pale kutokana na alivyoambiwa na mmewe victor
Eva hakupenda ila ilibidi aondoke..
Siunaona sasa mtoto wetu anaanza kupatwa na majanga....nilikwambia familia yao sio watu wazuri....alisema victor
Yaan sijui itakuaje..huenda tayari wameshaanza..yaan huyo bint atanijua kama kweli wamehusika....alisema rachel kwa hasira
Mda kidogo cathy alifika....wazaz wa danny walifurah kumwona cathy...maana wanamfaham kwa kua ni jiran yao halafu kwao ni matajir kuzid wao...kwahyo walifanya kujipendekeza
Cathy aliwasalimia baada ya kufika.
Asante cathy kwa kumjulia hali danny... Unaweza kukaa tu umsubiri danny aamke....alisema ma!a danny (rachel) amabe huyohuyo alimfukuza eva
Cathy alifurah kuambiwa hvyo......mara danny akazinduka.
Mwanagu jaman unajisikiaje...aliuliza rachel kwa shauku..
Najisikia vizur tu mama...danny alifurah kuwaona wazaz wake...
Danny aliangaza kama eva yupo lakin hakumuona....akaulizia kama eva alikuja pale..
Mama yake alidakia.....wala eva hajaja hapa....
Mwanangu yaani ndo kuamka na kumuulizia eva....kwani tuliopo hapa hatukutoshi had huyo eva..? Aliuliza victor..
Danny alikaa kimya.
Eva yupo darasan bize anasoma....alidakia cathy.
Danny alimwangalia kwa hasira akijua ni uchochezi tu.
Sasa rafiki gan huyo?...hakufai mwanangu..yeye anakujua wakat wa uzima tu.. ..mwenyewe nilizan atakuja lakini tangu tuje hajaonekana...alichombeza rachel..
Mara daktari alibisha hodi......Cathy alienda kufungua...daktar akaingia...
Cathy alistuka baada ya kumuona eva pemben kidogo ya mlango...
Eva machoz yalikua yakimtoka kwan aliyasikia yote yaliyoongelewa..eva alishangaa kwanini wazazi wa danny waliongea vile,
Hivi nimewakosea nini mimi hadi wanizuie kumwona danny makusudi?alijiuliza eva
aliamua kwenda zake bwenini baada ya kukata tamaa
Danny alipata nafuu na kuruhusiwa...wazazi wake walimuaga...wakaondoka na yeye akaenda shule
Ila alikua akijiuliza sana kwanin eva hakuja..
Alifika shule na baada ya siku aliingia darasan...
Eva alipomuona alifurahi sana ...akamchangamkia....lakn danny alioneka tofaut siku hyo.....aliwaza kwann eva hakuja kumsalimia alipokua mgonjwa...alimuona kama si rafk mwema..
Cathy aliifurahia ile hali akitumain atapata nafasi kwa danny....
Alimfuata danny na kukaa jiran yake...
Danny unaendeleaje aliulza cathy.....
Naendelea vizuri aliitikia..
Eva alijiskia vibaya maana danny hakumjibu pale eva alipoulza..
Alikaa kimya
Baada ya mda...eva alimuulza danny kwann yuko vile..
Yaan eva naugua nusu kufa hata kuja kunijulia hali hamna....alilalamika danny
Eva alijua fika kilichomfanya asiingie mle ndani....ila hakutaka kumwambia danny maana alijua angemwambia , danny asingeamin kama wazaz wake wanaweza kumsingizia eva...na angemuona mchonganish.
Nisamehe tu danny kuna vitu vilinikwamisha....alisema eva
Vitu gan hvyo eva.......yaan hata dakika tano za kuja kunisalimia hukupata!!!
Wazaz wangu wamekasirika kwa ulichokifanya eva...
Eva alikosa la kuongea ikabid anyamaze....
Danny hakua na furaha na eva tangu sku hyo,,cathy alichukua nafas hyo kama faida kwake lakn hata hvyo danny hakua na mda nae vilevile
Siku zilipita eva alikua na mawazo sana maana danny hakua yule wa zaman tena...
Danny nae alikua na mawazo.....alikasirika kwa alichofanya eva...lakn bado alikua akimwone huruma eva kwa vle alivyokua mpweke..
USIKOSE SEHEMU YA SITA
My eva💖💕💝
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
My eva💖💕💝
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO