MY EVA (6)

0
JINA: MY EVA
SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA...
Eva alikua na huzuni na alikia hana raha muda mwingi sana maana danny alikua amebadilika.
maskini Eva alikua mnyonge sana..

Danny alikua amevunjika moyo kwa alichofanya eva lakin bado alimuonea huruma kwa kua alikua mnyonge sana.

SONGA NAYO..
Danny alimwendea rafiki yake peter...akamwelezea hali ilivyo kati yake yeye na Eva.

peter alimiulza..kwan nini tatzo?

Unajua sku ile nilipokua nimelazwa nlikua nafikiria kua eva angekuja
lakini nilipomuuliza mama alisema eva hajaja pale hospitali..yaani hadi naondoka pale alikua hakujatu..liniuma bas tu..nilizani Eva ndo angekua mtu ww kwanza kuja pale..lakini hakuja et....alisema danny

Mmm mbona Eva alikuja...na mimi ndo nilimuona...??

Alikuja hadi akaingia ndan na wazazi wako walikuemo ila mda huohuo nlimuona ametoka akiwa amenyong'onyea sikujua kwanin alitoka mapema kias kile....alisema peter.

Mmmh...we peter wewe...mbona mm walinambia hajaja.? Aliuliza peter kwa mshangao..

walikuambia hajaja?..aliulza peter kww mshangao.

ee waliniambia hajaja..yaani tena wakasema hata wao wanashangaa kwanini hajaja na wamekasirika sana...alisema Danny.

Alikuja bwana....tena alikaa nje ya wodi uliyokuemo mda mrefu tu...ila kipindi anaondoka alikua kama analia vile...nlimuulza nini tatizo akaniambia hamna kitu...alikazia peter.

Wewe ulikua wapi mda huo...aliulza danny

Nilikua natoka kukunulia chakula...niliwakuta wazaz wako na cathy wakiwa wanaongea..nikaweka chakula wakaniambia niende nje kwanza.....alisema peter.

Danny alishagaa sana kwanini wazazi wake wamfanyie vile Eva. .aliwaza kwa nn wazazi wake walimwongopa.

sasa mama na baba walikua na sababu gani ya kuniongopea?..au cathy atakua alimchongelea Eva.. maaana huyo nae kwa mdomo mdomo tu ni hatari..alijisemea Danny

Itakua cathy alimchongelea eva..alijisemea danny
******

Baada ya mda danny alienda darasan akamkuta Eva amekaa peke yake akiwa hana raha.

Eva...aliita danny.

Bee...aliitika Eva

Et ulikuja pale hospitali..aliuliza danny huku alimwangalia eva kwa kujishtukia..

Hamna sikuja...alijibu Eva kwa mkato.

Eva..kama ulikuja niambie tu. usinikasirikie hivyo bwana... alisema danny huku akiaa karibu na Eva.

Mbna unaulza hvyo....aliuliza eva.
Peter amenambia ulikuja...halafu ulitoka kama unalia vile,kwani baba na mama walikwambiaje?...mbona ulikua unalia..aliuliza Danny.

Eva alipata kigugumizi kuyajibu yale maswali....usijal danny we yapotezee tu..alisema Eva.

Eva nambie basi,au cathy alikuchongelea?..aliuliza danny

Hamna cathy wala hahusiki....alisema Eva.

Eva alijua fika kua cathy sio chanzo maana walimfukuza hata kabla cathy hajaja..

Sawa umekataa kuniambia.....ila nisamehe basi,sikujua kama ulikuja...nisamehe sawa Eva.

Eva alikaa kimya kidogo,na yeye zamu ya kuringa ilikua imefika

Eva jamani...nisamehe basi... alisema Danny huku akimwangalia Eva machoni bila kupepesa akijua kabisa Eva ni muoga

Sawa, nimekusamehe..alisema Eva.

Danny alibaki amemkodolea Eva macho Kama dakika tano hivi.

Mbona unanikodolea....umenifananisha au...aliulza Eva.
Danny alimsogelea akamnong'oneza "we mrembo"

Eva alicheka tu baada ya kunong'onezwa na Danny

Siku zikaenda hatimaye walihitimu kidato cha sita na kila mtu kuelekea kwao.

Eva na danny waliagana huku wakitokwa ma machozi
.
Hivi Eva tutaonana lini tena...aliuliza danny

Tutaonana tu mungu akijalia..alijibu eva kwa unyonge.. Wakaagana tena na tena.
******
Danny alipokelewa kwao kwa furaha kubwa

wazazi wake walimfanyia sherehe ya kifahari kwa kuhitimu kidato cha sita...walikula,wakanywa na kufurahi pamoja.

baada ya siku chache wazazi wake walimwita...

Mwanagu tumekuita hapa kukwambia jambo fulani....alisema victor.

jambo gani hilo baba?...aliuliza danny kwa shauku akizani ni la heri.

kwanza kabla ya hapo nikuulize....bado unaurafk na eva?? Aliuliza victor..

Danny alishangazwa na lile swali,akaa mda kidogo kisha akasema...ndio baba.

anhaa..kumbe.. sasa mwanangu, sijui jambo hili utaliookeaje,lakini nakuomba huo urafiki na Eva uishe mara moja...alisema victor na kumkazia Danny macho.

Danny moyo alishtuka na mapigo ya moyo uakaenda kasi sana.
Kwanini baba??.. aliuliza danny kwa mshangao....

USIKOSE SEHEMU YA SABA

TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)