
SEHEMU YA SABA
ILIPOISHIA...
Mwanangu huo urafiki na Eva itabidi usitishe mara moja...alisema victor.Kwanini baba??... aliulza danny kwa mshangao..
SASA ENDELEA..
Mwanangu sisi wazazi wako tunapokukataza kitu ujue tunakutakia mema...hebu naomba utusikie...alikazia mama danny.Ndio najua kua mnanitakia mema....lakn ningependa kujua sababu ya hayo yote...alisema danny.
Huyo eva mm namfaham vizuri ...kwao sio watu wa kawaida....ni wachawi wakubwa,nisingependa kuona unadhurika kwa sababu ya kua karibu nae...alisema baba yake.
Lakini baba mimi nina urafiki na eva sio ndugu zake,sasa kama wao wakiwa wachawi inaathiri nini urafiki wetu?...aliuliza danny.
Sasa wewe huoni kua wanaweza kumtumia kukuzuru kwqkua wewe ni rafiki yake??..aliuliza victor.
Sasa wanizuru kwa lipi wakati hata hawanifahamu?....aliuliza danny.
We mtoto wewe usijifanye unajua mno kutuzidi sisi....kwani wachawi hua wanawazuru waliowakosea tu??alifoka mama danny..
Halafu istoshe wale kwao ni masikini sana....watakutumia uwe kitega uchumi...kwan hakuna waschana wa hadhi yako had ung'ang'anie huyo maskin?? Aliulza rachel...
Danny alikasrisika sana kwa maneno aliyosema mama yake..
Mama!!!!.....aliita danny kwa hasira..
Wewe.... uwe na adabu unamfokea nani hapa?!! Aliulza victor kwa hasira.
Kwani baba we mbona ulimpenda mama akiwa maskin kwao...nani alikuzuia!??.
Wew danny umekua sana ee...unajibizana hvyo na baba yako!??....alifoka mama danny
Danny ilibidi akae kimya maana wazazi wake walikua wamewaka kweli kweli...
Sasa nakwambia stak kusikia habar za eva hapa....alisema mama danny kwa hasira..
Kaul ya danny ilimuuma rachel maana hata yeye alikua maskini alipoolewa na victor..
hili toto jinga sana..alijisemea rachel kila akiikumbuka kauli ile.
Danny alikua na huzuni sana baada yale mazungumzo...maneno ya wazazi wake hayakumwingia kichwani hata kidogo.....alimpenda sana Eva.
kwani baba yeye amejuaje kama ni wachawi!?..uongo mtupu!!...hapa kwakweli watanisamehe tu kwakweli maana haitawezekana mimi kumwacha Eva..
Mda si mrefu Eva alimpigia simu danny..danny alikua akiongea kwa unyonge sana hadi eva akashtuka na kumuuliza:
Danny unaumwa??...aliulza eva..
Hamna eva..wala siumwi..alisema danny
Sasa mbona mnyonge hvyo??..aliulza eva.
Danny alikosa jibu,akakaa kimya kwa muda mfupi kisha akasema:
Eva...
Abee...aliitika Eva.
Nakupenda Eva sawa ee...
Eva alishangazwa na hali ya danny... Alikua akionge akwa unyonge sana..
Nakupenda pia danny.... Lakin mbona uko hvyo...
Mama yangu anaumwa sana Eva...alidanganya danny..
Pole jaman....ashaenda hospitali?
Kabla danny hajajibu..mara mama yake huyu apa....danny ikabidi akate simu
Hivi wewe mtoto husikii ee...nshakwambia hunielewi...alisema rachel na kuweka kituo kikubwa.
"et mama yangu anaumwa ndo maana niko hivi"... alisema rachel huku akibinua pua kwa kidole chake..hivi wewe mbona una kichwa kigumu kuelewa?...aliuliza rachel kwa hasira
Danny alikaa kimya huku ameinamisha kichwa..
rachel alimwangalia jicho baya kisha akaondoka kwa hasira.
Eva hakuelewa nini maana ya mambo yote hayo.
hivi danny kawaje kwani?..mbona simwelewi?...alijiuliza eva ila akapotezea.
Usiku huo eva aliota ndoto iliyokua ikimsumbua mara kwa mara....siku ya kwanza kuiota ni siku ile aliporipoti shule na ndo sku hyo alipokutana na danny... Aliipuuza maana hakuielewa.
Ni mara ya sita sasa ndoto ile inajirudia..
Alimwa!ba shangazi yake kwamba hua kuna ndoto inayomsumbua kila mara...
Ni ndoto gani hiyo mwanangu...aliuliza shangazi yake
Yaani kuna mtu amekaa kwenye kiti fulani hivi kama cha kifalme....walinzi weng wakimlinda....alisema Eva kisha akaweka kituo.
Enheeee...alichombeza shangaz maria
Ila huyo mtu alikua anatokwa machoz huku akiniambia...alisema eva
Enheeee...
Unasafari ngum mbele yako...imejaa machoz....ila itabidi uvumilie..maana baada ya mda mref yataisha na utakua na furaha hadi kifo...ukweli wa maisha yako ni mgum kuukubali....utakuathiri sana...lakini sasa utafanyaje...utavumilia tu...alisema Mtu yule halaf akanikumbatia mara nguo na alizovaa nikajikuta nimevaa mimi....nikashtuka ....sasa shangaz mimisielewi kwakweli...alisema eva.
Shangazi alishtuka sana...sasa itakua na maana gani?
Ila alikumbuka sku moja aliona picha Eva akiwa amepiga na kijana mmoja na mwanaume fulani hivi na mwanamke....(ni picha waliyopiga sku ya visting day).
Kilichomstua shangaz ni yule mwanaume kwenye ile picha....anamjua sana kua ni yule aliyehusika na kifo cha wazazi wa Eva..
Yule mtu alikula njama moja na mme wa shangazi maria kuwauwa wazazi wa Eva...na baada ya shangazi kujua hili jambo aliamua kutengana na huyo Mme ingawa huyo Mme wake anamtafuta amuue kufuta ushahidi.....
Shangaz alishtuka sana ila akajikausha...alihofia labda mwanae anaweza kua na urafiki na huyo kijana kwenye picha ambae huenda ni mtotonwa muuaji yule..aliogopa jinsi baba wa danny angemfanya eva...
Ila alihofia kumuulza eva kuhusu ile picha..maana angemshtua..
Shangazi unawaza nini? Eva alimuuliza shangazi...
Aaaaaaah.......hamna kitu....nlikua nawaza pengne hiyo ndoto ina maana gani...alidangaya shangazi
USIKOSE SEHEMU YA NANE
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO