
SEHEMU YA NANE
ILIPOISHIA...
Shangaz mbona una unawaza sana?..aliuliza evaHamna kitu mwanangu....alijibu maria.
SASA ENDELEA..
maria alipobaki peke yake liwaza sana...alitaman kumuuliza Eva kua hao aliowaona kwenye pocha ni akina nanin ila alipanga kumuulza sku nyingne maana kwa siku hiyo angemshtua Eva.. huenda Eva angehisi.Baada ya siku kazaa kupita...maria aliona amuulze Eva kuhusu ile picha.akiona atumir mbinu ya utaniutani ili Eva asihisi kitu..
Eva hawa ni akina nan?...maana unapenda kuiangalia hii picha sana.....hebu nambie mwanangu au ndo tayari...aliulza maria kama kiutani vile..
mmmh...shangazi na wewe jamani...et tayari.
eee... kama ni tayari tuambizane ukweli buana..alisema shangazi na wote wakacheka.
Hamna bwana....huyu ni rafiki yangu tu na hawa ni wazaz wake,tulipiga picha siku ya visting day.....alisema Eva.
Maria alishtuka..ila ilibidi ajikaze...akajichekesa tu..
haya mwanangu alisema maria.
maria alipobaki peke yake aliwaza sana..
hivi nimwambie Eva?.. nitaanzaje..hivi ni sahihi kweli au ndo nitayakoroga?..alijiuliza maria akiwa peke yake.
maskini ww Mungu Eva, ndo mtihani gani huu anapitia tena..ee Mungu msaidie huyu mtoto jamani..alijisemea maria.
Mda ulipita hatimaye matokeo ya kidato cha sita yalitoka na wote walikua wamefaulu.
Danny alimpigia Eva wapange watakwenda chuo kipi ili watume maombi...
Walikubaliana,, wakatuma maombi na wakachaguliwa chuo kimoja...
Kwa bahat mbaya hata cathy alituma hukohuko..
Maisha ya chuo yalianza ...Eva alikua na furaha maana ilikua rahisi kumuona danny mda wowote.
Lakn danny alikua na furaha iliyochanganyikana na mashaka sababu ya msimamo wa wazazi wake kwa eva..... ila alijipa moyo tu..
=====
Mama wa danny alipojua kua Eva yupo chuo kimoja na danny alikasirika si kidogo.
Mama danny alimpigia simu danny..
eeeh..Kwahyo umeona sisi ni wajinga unatudanganya kua mko vyuo tofauti wakat mko chuo kimoja??alifoka rachel...unataka nini wewe mtoto lakini?
Danny alishangaa mama yake kajuaje...alikana kua sio kweli
Kwahyo cathy ni mjinga?? Au hamjui Eva?..au unataka nikutumie na picha aliyowapiga??..alisema rachel kwa hasira...
Danny alishangaa kusikia hvyo...alikasirika kusikia ety cathy ndo kasema...alikaa kimya,hakumjib mama yake..
Mama yake alifoka sana ila danny alikaa kimya..
Mda wote huo kumbe Eva alikua nje mlangon kwa danny akisikiliza maana alikuja,,lakin alipotaka kuingia...alishtuka kusikia maongez yale....akabana kusikiliza..... Alisikia yote maana danny alikua na tabia ya kuweka loud speaker.
maskini Eva alianza kutokwa na machoz....
Kumbe wazaz wa danny hawatak mimi nisiwe karibu na danny!!!....aaah...sasa naanza kupata picha ta kwanini walinifukuza pale hospitali Alijisemea eva...
alikumbuka siku ile pale hospitali roho ikamuuma sana...
Kwanini lakn????....kwan nimefanya nn...au kwakua mm maskin..
Yote hayo alijiuliza akiwa mlangon kwa danny..
Eva aliamua kuondoka bila danny kujua kama alikuja...ila kabla
hajaondoka mara ghafla danny alifungua mlango...
Alishangaa kumuona eva pale akiwa analia...
Eva umekuaje??.....aliuliza danny huku akimuingiza eva ndani...
Danny mimi niliwakosea wazazi wako??....au kwakua mimi maskin??nasoma kwa msaada?
Eva...nyamaza kwanza...usilie mimi nakupenda eva..danny alimbembeleza eva..
Siku zote mbona ulikua ukinificha?....aliuliza eva.
Danny alikosa jibu..
Haya niambie....kwanini hawataki uwe na mimi?... mimi nimefanya nini kwani?...aliulza eva akilia
Hata hawajaniambia sababu ya msingi...alidanganya danny..alihofia kumuumiza zaid eva...
Eva we usijali mimi nipo na wewe...alisema danny huku akimkumbatia eva..
Baadae danny alimfuata cathy kule alipokua
Cathy....aliita danny
Abeee..aliitika cathy kwa tabasamu akizani labda danny amekuja kwa heri.
Hauna kazi za kufanya siku hizi??...aliuliza danny
cathy alishtushwa na swali lile maana hakulitegemea.
kwanini unaniuliza hivyo?.. aliuliza cathy akiwa ameishiwa pozi.
Sikiliza cathy...wewe endelea kushtaki kwa mama...ikibidi uwe unarekod Kila ninachofanya na Eva...unatuma kwa mama..ila kaa ukijua kwamba hautabadil chochote....
Hata nikimkosa eva siwez kua na wewe..alisema danny kwa hasira na kuondoka....
cathy aliumia sana moyoni.. nguvu zilimwishia..aliona kua Eva ndo chanzo cha yeye kukataliwa na danny, aliapa kumkomesha eva..
Rachel alimwabia victor kwamba danny aliwadanganya na yuko anasoma na Eva....victor alikasirika sana...
baada ya kuwaza sana victor akasema:
Sasa mama danny...
Nambie mme wangu...alisema Rachel.
Danny nitamuhamisha chuo akasomee nje ya nchi....hyo itapunguza ukaribu...alisema victor.
Ni wazo zuri mme wangu...alijibu rachel.
USIKOSE SEHEMU YA TISA
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO