RANIA (14)

Zephiline F Ezekiel
RANIA (14)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA KUMI NA NNE ILIPOISHIA... Hatimaye siku ya mapambano ilifika..mpambanaji alikuja na kinyago uwanjani..mwanamfalme nae alikua amejiandaa sawa sawa. Muda wa pambano ukafika na Dom akaamuliwa kuweka chini kinyago.. Dom alikitoa kinyago usoni na kukutanisha uso na fasha. Fasha ali..... SASA ENDELEA.. Fasha alishangaa kuona Dom ndo mpinzani wake Lakini hakujali kivile. Kwa ajili ya Rania ndo umeamua kuja kupambana na mimi?..aliuliza Fasha kwa sauti ya chini. Muda wa mapambano umeshafika mwanamfalme,.. Alisema Dom. Najua..lakin hukupaswa kuja..Rania yuko salama.. Humiamini?..aliuliza Fasha. Nakuamini ingawa sio asilimia zote.. Alisema Dom. Haya ngoja na tuone..alisema mwanamfalme na kuanza mapambano muda huo. Walipambana kwa muda mrefu kidogo.. Baada ya muda Dom alionekana kuzidiwa.. Watu walianza kushangilia maana walimpenda Fasha. Kwa dakika chache Dom alikua ameshayasoma madhaifu ya Fasha pamoja na sehemu ambazo alizitumia sana kwenye mapambano. Walikwenda mzun…