
SEHEMU YA KUMI NA TANO
ILIPOISHIA...
Usiku wa manane Dom alianza kunyata na kuatafuta kilipo kile chungu...Alitafuta sana mwisho akafika kilipo chungu ingawa alikua hajajua kama ni hapo..
Muda huo huo mganga alikua anakuja kwa ajili ya kuongeza viungo kwenye dawa yake kuiboresha zaidi ili kumkamata Rania..
SASA ENDELEA..
Wakati Dom anaendelea kushangaashangaa mara kwa mbali Alimwona mganga yulee anakuja..ilikua ni kama bahati tu alimwona mapema.Dom ilibidi avunge kua alikua anapita tu..hata hivyo Dom alikua hajajua kama alipokua ndio penyewe
Haraka alitoka na kujificha sehemu aone mganga ataweka mambo yake kwenye kona gani.
Mganga bila kujua kama kunamtu anamfuatilia nyuma alifika na kuangaza huku na kule hakuona yeyote yule... Akahakikisha ni salama.
Taratibu aliweka dawa yake na kunuia maneno fulani ambayo Dom hakuyasikia...
Baada ya kumaliza kazi yake Mganga aliamua kwenda zake..
Wakati huo Dom aliasubiria hadi mganga akafika mbali na yeye akaja.
Alinyata taratiiibu hadi akafikia kile chungu... Aliangaza huku na huku hakuona mtu... Kabla hajaendelea kufanya mambo mara alihisi kama kuna mtu nyuma yake anamvizia..
Ni nani huyu?...alijiuliza Dom..
Dom aliamua kubadili mwelekeo na kuvunga kama anakifunikia chungu vizuri na kufunika kitambaa maana mganga alikua ameacha vibaya vibaya tu.
Baada ya kukifunika akaamua aende zake.
Dom alivunga kuondoka lakini alijificha ili aone kama huyo mtu alikua na kazi zake tu au alikua anamfuatilia yeye.
Dom akiwa amejificha mara alimwona mtu huyo akikaribia chungu kile.. Mtu huyo alikua amevalia kinyago cheusi Kama tu Dom alivyokua amevaa.
Mtu huyo alipokifikia chungu alikiinua na kutaka kukipigiza chini kipasuke...
Dom alishtuka.. Alikumbuka mama yake alivyomwambia kua mtu atakaejaribu kuharibu hizo dawa bila kukata kile kijiti cha mwanzi lazima awe kichaa..
Bila kuchelewa Dom alimuwahi mtu huyo na kumzuia asikivunje...
Mtu huyo alishtuka sana baada ya kuzuiliwa...
Nani wewe?..aliuliza mtu huyo..
Weka hiki chungu chini kwanza ndo tuendelee..alisema Dom.
Mtu yule akaweka chungu chini kwa wasiwasi.
Mwanamfalme... Unataka kufanya nini?.. Aliuliza Dom.
Dom!!..aliita Fasha kwa mshangao baada ya kuitambua sauti ya Dom.
Wote iliwabidi wavue vinyago vyao
Dom..sijajua umefikaje hapa lakini ngoja nikwambie....hiki chungu ndicho kina dawa...alisema Fasha kabla Dom hajamkatisha.
Najua mwanamfalme...najua kua hiki ndo kinafanya Rania akiingia humu wanatambua mara moja.. Lakini hivyo ulivyotaka kufanya sio sahihi.. Alisema Dom.
Sio sahihi kiaje?...Aliuliza Fasha.
Ungekua kichaa...alisema Dom.
Heee... Kichaaa?..aliuliza Fasha kwa mshituko.
Dom alichuchumaa na kutoa kisu kile na kukikata kijiti cha mwanzi.
Muda huo hio dawa zote kwenye chungu ziliyeyuka na baada ya muda zikarudia hali yake.
Ndio nini hicho?..aliuliza Fasha.
Hapa tayari haiwezi kufanya kazi tena...hata Rania akikanyaga ikulu haitafahamika...alisema Dom.
Heee.. Umeitoa wapi?..Aliuliza Fasha.
Ni Hadithi ndefu...alisema Dom.
Sawa...ngoja nikumini kwa sasa.. Alisema Fasha.
Walitoka pale kwa haraka na wakaenda mbali...
Dom.. Tujaribu kumleta halafu nione kama itagundulika...ikiwa dawa yako sio ya kweli sitakusamehe kwakweli... Alisema Fasha..
Sawa.. Alisema Dom kisha akaondoka...
Huku Rania alikua akiwaza sana.
Hivi mimi eti nitaufanyeje ufalme!!?....mbona tuhuma wanazonipa haziendani na mimi jamani?.. Alijiuliza Rania.
Akiwa anawaza mara alikuja Fasha.
Rania alisimama na kutoa heshima kwa mwanamfalme kama kawaida..
Rania,... Sasa hivi uko huru kutoka humu..alisema Fasha
Heeee.... Asante sana mwanamfalme,nakushukuru sana..alisema Rania kwa furaha.
Ila utaishi ikulu..alisema Fasha.
Ikulu?.. Kwanini tena?.. Aliuliza Rania akiwa ameishiwa pozi.
Siwezi nikakuacha ukaenda kwa Dom.
Mwanamfalme, wewe uliwahi kuniambia kua nikikanyaga tu ikulu nitakamatwa..na sasa hivi unachosema ni nini basi?..aliuliza Rania.
Hiyo dawa ilishavunjwa tayari... Hauwezi kujulikana..alisema Fasha.
Nani kaivunja?..aliuliza Rania.
Dom...alisema Fasha.
Dom??!!....aliuliza Rania kwa mshangao...
Sasa bado unahitaji kwenda nje ya ikulu...aliuliza Fasha.
Rania alikosa ujanja...akakaa kimya.
Nitatafuta sababu ya kukufanya ukae ikulu kwa uhuru..lakini hutakua karibu na Dom.
Lakini mwanamfalme.. Kwanini unakua hivyo lakini?.. Sasa kwanini nisiwe karibu nae?..aliuliza Rania.
Rania... Nifanyeje sasa ili ujue jinsi ninavyoumia?...basi na wewe kwanini unakua hivyo.. Kwani mimi nina kasoro gani hadi unione wa kazi gani?.. Aliuliza Fasha kwa uchungu..
Nisamehe sana mwanamfalme.. Lakini mimi simaanishi wewe ni wa kazi gani...ila nyie nyote ni watu wangu wa karibu.. Kwanini nimtenge Dom basi?.aliulza Rania.
Fasha alikaa kimya huku akiumia moyoni mwake.
Rania alimwangalia kwa huruma sana Fasha... Alijua kiasi gani anaumia lakini hakua na jinsi maana alikua ashampenda Dom.
Mwanamfalme... Nisamehe sana..natamani ningeweza kukufanya ufurahi....alijisemea Rania kimoyomoyo.
Haya nifuate..alisema Fasha.
Rania alimfuata Fasha nyuma akiwa hajui hata anakoenda..
Walipanda juu ya farasi na kwenda sehemu fulani..
Walipofika Fasha alimwagiza mtumishi wake mmoja kufanya jambo fulani ingawa Rania hakusikia.
Mwanamfalme.. Nimekuja....alisema Dom.
Ingia humo..Alisema Fasha.
Dom aliingia kwa wasiwasi..alipoingia hakuamini kuonana na Rania tena.
Rania alilipuka kwa furaha.. Bila kuchelewa alikwenda na kumdandia Dom kama ngedere anadandia mti..
Dom alimkumbatia Rania kwa nguvu bila hata kujali kama ni mzito wala nini...
Rania... Unakula sana tatizo... Alisema Dom.
Na ndio utakoma leo..hata sina mpango wa kushuka sasa...nitakudandia hadi jioni..?alisema Rania.
Dom alitabasam tu..
Eti Dom.. Umeitegua ile dawa?..aliuliza Rania
Tumeitegua mimi na Mwanamfalme...alisema Dom.
Mwanamfalme kaniambia ni wewe..alisema Rania.
Ni wote sio peke yangu... Alisema Dom.
Umewezaje?..aliuliza Rania.
Nitakusimlia baadae...ni Hadithi ndefu.. Alisema Rania.
Fasha aliamua kukaa mbali asiwasikilize maaan angeumia maskini😢
Huku ikulu ikulu mfalme aliwaita watu wake.. Omandi na mganga.
Kwa sasa naona imeshindikana kumpata huyu binti kwa wakati mwafaka...sasa natoa amri.. Fanyeni upelelezi na kila atakae bainika kua ni ukoo wa Mfalme aliepinduliwa auawe kwa siri....na hakikisheni Fasha hajui maana navyomjua hawezi kukubaliana na sisi katika hili...alisema Mfalme.
Ndio mtukufu Mfalme..tutafanya kama ulivyoagiza..alisema mganga na omandi.
Baada ya hapo mganga aliondoka moja kwa moja akaenda kwa malikia suya na kumwambia mpango wao.
Sawa...we hakikisha unaniletea kila taarifa hapa kwanza tummalize huyo mtoto anaetusumbua halafu tukimaliza na mfalme basi tutammaliza..alisema malikia suya.
Omandi na Mganga walikusanya vijana wao wanaowaamini na kuanza kazi ya uchunguzi.
Baada ya siku kadhaa walikua wameshawapata baadhi yao.vijana wale walitoa taarifa na wakapewa mamlaka ya kuwaua..
Wale vijana majira ya usiku walikwenda hadi sehemu walipowaona wale watu wa uzao wa mfalme aliepita..
Pale walipokua wanaishi hanna na Namadi palikua jirani kabisa na hao watu...
Usiku namadi akiwa amelala alisikia mtu akigonga mlango... Kwa hofu alikwenda kufungua mlango..
We mtoto.. Tatizo nini?..mbona unagonga mlango usiku huu jaman?.. Aliuliza Namadi
Kaka Namadi.. Mama na baba yangu wanakufa huko..kuna watu wameingia humo ndani wakiwa na silaha..mimi nimejikaza nikatoroka..naomba msaada wako tafazali.. Alisema mtoto yule.
Namadi alishangaa sana kusikia hivyo.. Haraka aliondoka hadi kwa jirani huku akimwambia yule mtoto abaki ndani kwa namadi.
Namadi alipofika mlangoni alisikia saut za watu waliokua kama wamefungwa midomo kwa vitambaa wasiongee wakilia.
Namadi aliingia ndani kuwatafuta wauaji...
Akiwa anatembea kwa kunyata mara walimona na wakamuweka kati.
Umefuata nini wewe?. Aliuliza mmoja wa wale wauaji lakini namadi hakujibu swali lile.
Muueni huyu haraka sana..alitoa amri muuaji yule.
Namadi muda wote huo alikua akiwasomea ramani..kabla hawajamkamata walitembezewa kichapo cha haraka haraka..
Ndani ya dakika chache walikua washaumizwa vibaya sana..waliamua kukimbia.
Namadi aliwahi chumbani kwa wale wazazi wa yule mtoto.alipoingia tu aliwaona wamelala chini wakiwa wamejeruhiwa vibaya sana.
Baba wa mtoto yule alikua tayari ameshakufa ..aliekua anaelekea kukata roho alikua mama.
Namadi aliwahi amchukue yule mama ili amtibu..
Mwanangu.. Niache tu hapa mimi si wa kupona...tafazali kama ukimwona mwanangu nitunzie..alisema mama yule kwa tabu sana.
Mama.. Usiseme hivyo hautakufa. Alisema Namadi..
Hapana mwanangu...sitapona..wameniua hawa watu..kisa mimi ni ndugu wa mfalme kelkuni...walimtoa madarakani kwa nguvu..na sasa wanawatafuta wazawa wake wawaue...alisema mama yule..
Namadi alikua anashangaa sana maana yeye alikua hajui cha Mfalme kupinduliwa wala nini.
Mama yule alifariki wakati Namadi akishangaa bado.
Namadi alipogundua kua yule mama ameshafariki aliumia sana moyoni.. Alirudi kwa yule mtoto akiwa amenyong'onyea sana.
Maskini mtoto yule alipomwona Namadi kwenye ile hali alijua tu kua wazazi wake ndo basi tena...alianza kulia sana.
Namadi alijitahidi kumbembeleza lakini haikusaidia..
Kesho yake asubuhi sana namadi alimwita hanna na kumweleza yaliyotokea..
Haaaa... Jamani.. Hii nchi mbona inatisha?..aliuliza hanna.
Hanna huyu mtoto inabidi tumtoroshe maana wanamtafuta na yeye wamuue...alisema Namadi.
Walikubaliana kwenda kumficha mtoto kijiji jirani.....baada ya kufika huko Namadi alisema,
Hanna baki na huyu mtoto mimi nitaenda kumtaarifu Rania kilichotokea..
Sawa.. We nenda.. Alisema hanna.
Rania akiwa na Fasha mara alikuja mtumishi mmoja na kumwambia Fasha:
Mwanamfalme.. Kuna mtu anataka kuonana na wewe hata hatumjui..amesema kua eti anaitwa Namadi.
Namadi?. Hebu mruhusu aje..alisema Fasha.
Namadi kawaje?..aliuliza Rania.
Muda huo Namadi alifika akiwa na hofu kubwa..
Namadi tatizo nini? Aliuliza Rania kwa pupa...
Namadi alieleza kila kitu hadi mwisho kisha akanyamaza.
Nini?.. Alisema Rania macho amemtoka..
Fasha nae alishtuka sana..NINI KINAFUATA?.
USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA SITA
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO