RANIA (16)

Zephiline F Ezekiel
RANIA (16)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA KUMI NA SITA ILIPOISHIA... Namadi tatizo nini? Aliuliza Rania kwa pupa... Namadi alieleza kila kitu hadi mwisho kisha akanyamaza. Nini?.. Alisema Rania macho amemtoka.. Fasha nae alishtuka sana.. SASA ENDELEA.. Nani ametoa hii amri?.. Ni mfalme au..alijiuliza Fasha. Haya unaweza kwenda sasa...alisema Fasha akimwambia Namadi. Mwanamfalme, bila shaka hii ni kazi ya baba yako...alisema Rania. Hivi Mfalme anaweza kutoa amri ya namna hii kweli!!..alisema Fasha. Huenda na mimi ni wa huo ukoo unaowindwa...watanutafuta muda sio mrefu... Alisema Rania. Wewe sio wa huo ukoo...la sivyo siku ya kwanza tu kukanyaga ikulu ungeshakufa tayari...Alisema Fasha. Na hiyo dawa ipo?..aliuliza Rania kwa mshtuko. Ndio ipo...alisema Fasha. Mungu wangu.. Mimi kukosekana ndo kunafanya watu wasio na hatia kufa!!!...alisema Rania. Usiseme hivyo Rania..alisema Fasha. Wakati Namadi anaondoka alikutana na Dom.. Namadi...mbona uko hapa?..aliuliza Dom. Namadi alimsimulia yote.. Haaaa.....alishtu…