RANIA (22)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI ILIPOISHIA... Fasha alipogeuza macho yake alikutanisha macho ana kwa ana na Rania akiwa kama mmoja wapo wa watumishi wa binti mfalme... Nini???...alijisemea Fasha kimoyomoyo kwa mshangao mkubwa... SASA ENDELEA.. Rania alipoona Fasha anamwangalia sana aliangalia chini. Mwanamfalme... Mbona unashangaa sana?..aliuliza jao kwa sauti ya chini. Aaa..hamna kitu.. Alisema Fasha huku akionekanankabisa kuna jambo linalomsumbua. Walifanya mapokezi vizuri bila tatizo lolote.. Kuanzi siku hiyo Rania aliishi ikulu kama mtumishi wa Mars binti mfalme na mke mtarajiwa wa Fasha. Kesho yake asubuhi mwanamfalme akienda kumsalimia mchumba alikutana na Rania mlangoni. Baadae unione...alisema Fasha na kuingia ndani. Rania hakujibu kitu..aliendelea na kazi zake. Baadae kama walivyokubaliana walionana kwenye sehem ya faragha ya mwanamfalme. Rania... Kwanini umenifanyia hivi?.. Aliuliza Fasha. Nimekufanyia nini kibaya sana mwanamfalme?... Aliuliza Rania. Tuseme kwam…