RANIA (23)

Zephiline F Ezekiel
RANIA (23)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU ILIPOISHIA... Kiukweli waliokua wamebakia alikua ni yeye na Fasha tu ingawa Rai hakujua kuhusu Fasha. Rai alitambua kua Dom ndo aliebakia maana wengine hawakujua habari za ikulu wala NADISH.. Dom peke yake ndie alifaa. Rai alipata kigugumizi juu ya lile jambo.. Alijiuliza aseme au la... SASA ENDELEA.. Mama...aliita Dom baada ya kuona kua mama amekaa kimya muda mrefu. Mwanangu...wewe ni damu ya ukoo wa mfalme kelkuni....alisema Rai. Mimi?..alisema Dom macho yamemtoka. Ndio mwanangu... Wewe ni damu ya kelkuni.. Mimi na baba yako wote ni ukoo wa mfalme aliepinduliwa..alisema Rai Ulipokua mdogo nilikuwekea kinga juu ya dawa iliyowekwa ikulu ya kuwaua uzao wa kelkuni pindi tu wanapokanyaga ikulu..... Kwahyo Ndio maana hata ulipoenda ikulu hakuna kibaya kilichokukuta..alisema Rai. Dom na Rania wote walibaki wanashangaa.. Mama..kwangu mimi haitawezekana kwamba niwe kiongozi maana siwezi kukosana na Fasha sababu tu ya madaraka...alisema Dom. Sasa…