RANIA (25)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO ILIPOISHIA... Rania alimwangalia Dom usoni kwa dakika kama tano hivi.. Nini...aliuliza Dom kimasihara . Dom nikwambie kitu... Alisema Rania. Niambie....alisema Dom kwa hamu ya kuambiwa hicho kitu.... SASA ENDELEA.. Rania taratibu alianza kumsogelea Dom.. Dom macho yalikua yamemtoka kama chura mjamzito... Rania alimsogelea zaid Dom akamkazia macho kwa muda wa dakika kama tatu hivi kisha akainua mkono wake kuelekea usoni kwa Dom..Dom ndo alizidi kukodoa macho zaidi Aiiiiii...we Raniaaaa!!!!... Dom alisikika akilalama baada ya Rania kumbonyeza kwa nguvu chunusi yake kubwa iliyokua usoni. Anhaa....kumbe ni li chunusi..nilizani jipu...alisema Rania huku akimwachia Dom. Nilizani umeshakua..kumbe bado una mambo yako ya kitoto..alisema Dom. Hihiihii...alicheka Rania kisha akasema: We ulitaka nifanyeje uone ni mambo ya kikubwa?....najua tu ulichokua unawaza kichwani kwako.. Hahaaa...alisema Rania. Wewe subiri... Nitakukomesha na wewe siku nyingine.…