RANIA (26)

Zephiline F Ezekiel
RANIA (26)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA ILIPOISHIA... Dom apoona vile aliwahi alipokua Fasha. Mwanamfalme... Mwanamfalme... Aliita Dom lakini Fasha hakuamka..Dom alihisi kuchanganyikiwa.... Hali ya Fasha ilikua mbaya sana.... SASA ENDELEA.. Dom alihisi kuchanganyikiwa.. Hakujua nini hasa chanzo cha Fasha kua vile na hakujua afanye nini... Ndani ya muda mfupi tayari matabibu wa ikulu walikua wameshafika.. Haraka walimchukua Fasha na kuondoka nae..Dom aliwafuata kwa nyuma. Walipofika tu kwenye chumba cha tabibu mkuu walimwingiza Fasha haraka..Dom nae pia alitaka kuingia lakini alizuiliwa. Kwa huzuni alirudi alikotoka... Akiwa amekaa mara Rania alikuja huku anahema. Dom... Eti nini kimemkuta Fasha?.. Aliuliza Rania. Sifahamu...mwenyewe nimemwona ameanguka tu hata sielewi...alisema Dom.. Mmmmh..sasa atakua amefanyaje..alisema Rania huku akikaa. Mara ghafla Dom alishtuka. Nini?...mbona umeshtuka hivyo?.. Aliuliza Rania. Dom aizidi kukodoa macho... Dom..tatizo nini?...aliuliza Rania. Dom …