RANIA (28)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE ILIPOISHIA... Kumbuka kitu kimoja....nitakusaidia kwenye kua mfalme lakini kwa shariti moja...alisema suya. Lipi hilo?... Utanifanya malikia wako...alisema suya.. Hilo halina shida... Alisema mkuu wa majeshi. Waliagana na mkuu wa majeshi akaondoka. Njia nzima mkuu wa majeshi alikua akiwaza juu ya kumuua Fasha.... SASA ENDELEA.. Baba..naomba ruhusa nifanye kitu kimoja... Alisema Fasha akimwambia mfalme. Sema mwanangu... Alisema Mfalme. Naomba nikaonane na mama mmoja huko nje ya ikulu.. Alisema Fasha. Kwanini?..aliuliza mfalme. Kwa sasa ninataka niwafahamu wazazi wangu..wawe wako hai au wamekufa...sasa huyo mama anaonekana kua na ujuzi na mambo mengi hapa ikulu... Alisema Fasha. Ni nani huyo?.. Aliuliza Mfalme. Simfahamu jina ila kuna mtoto wake yuko hapa ikulu anafanya kazi...ndo nimemfahamu huyo mama kupitia kwake....alisema Fasha. Mmh...haya nenda... Alisema Mfalme. Nashukuru baba kwa ruhusa yako...alisema Fasha. Baada ya hapo Fasha alikwenda…