RANIA (37)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA THELATHINI NA SABA ILIPOISHIA... Haraka alirudi ndani na kuangalia kwenye kioo chake na kumwona Rania anatembea porini mwenyewe bila uelekeo wowote huku akiangaza huku na kule huku ameshikikia kile kisu cha kumshambulia Suya. Rai alichoka.....alihisi mambo yameharibika zaidi SASA ENDELEA.. Mama naomba unisamehe sana...nimeshafanya kosa Mara ya kwanza.. Siwezi kuacha mabaya yamkute Dom kwa ajili ya ujinga wangu... Alijisemea Rania huku akiendelea na safari. Akiwa anatembea mara aliona askari wawili wakitembea..aliwafahamu kua ni watu wa Suya maana alikua akizijua sare zao. Kwa kujificha alianza kuwafuata nyumanyuma wale watu ili afike alipo Dom na kumwokoa. Muda huo suya na Faritha walikua wameingia ndani ili kumwona mpelelezi.. Dom alishituka kumwona suya.. Alijua ameisha maana alizani kua suya bado anamkumbuka. Lakini kwa upande wa Suya yeye wala hakua amemkariri Dom.. Wala hakumkumbuka..ulikua wasiwasi wa Dom tu. Suya na Faritha walisogeza viti wakak…