RANIA (38)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA THELATHINI NA NANE ILIPOISHIA... Walishinda ingawa walibakia na huzuni maana hata Mfalme wa Lazi alikua amepoteza watu wake wa karibu sana aliowaamini pamoja na asilimia kubwa ya jeshi lake. Hatimae vita ilibakia kati ya Suya na Rania. SASA ENDELEA.. Licha ya kua vita kubwa iliyobakia ilikua kati ya Rania na Suya lakini wanajeshi hawakujua. Wanajeshi wa Tharia na lazi walizania vita imeisha..lakini ukweli ni kwamba suya alikua na uwezo wa kuwaangamiza kwa kutumia jeshi dogo alilonalo kwakua ni mtu wa miujiza sana. Mfalme wa Tharia alilijua hilo ingawa bado alikua hajaliweka wazi kwa Mfalme wa Lazi. Suya akiwa peke yake chumbani alikua akifanya ibaada ya kumwongeza nguvu. Baada ya ibaada yake kukamilika alitoka ndani kwenda kuonana na Faritha ili amwambie hali halisi na mipango na ukuu wake wote alionao. Alimwita Faritha pamoja na mganga sehemu ya faragha na kuwaeleza yote. Mganga alistaajabu sana..hakuamini alichokisikia. Kwanini ulinificha Siku zote hi…