
SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA
"Shikamooni namuulizA mama rozinta nimemkuta.""Heee mtume basi malaya wangu rozinta ameshaaharibu maana namwambiaga mimi aache Muda mwingine enhee kaka ndio mimi mama yake nambie.......
SASA ENDELEA...
BMwili wangu ukapigwa shoti ya ajabu kwa kile alichokijibu mama yake rozinta ambaye nilipomuangalia vizuri alikuwa sio siri amefanana na rozinta hata alivyokuwa akiongea.Hakika jibu lake lile lakuniambia malaya wangu rozinta ndio lilinifungua na kuamini sasa kwa mbali kuwa rozinta alikuwa ni Malaya wa kutupwa hadi mama yake anamjua nikajikuta nikiishiwa pozi na kukaa kwenye mkeka pasipo hata kuambiwa kuketi maana muda ule kichwa changu kilianza kuuma kupita maelezo."Hee vipi Mwanangu tena umeniambia unamuuliza Mama rozinta ndio mimi sasa niambie una shida gani."Yule mama rozinta akaniuliza na kusababisha nimuangalie huku machozi yakinilenga lenga na kusababisha niwashangaze mama rozinta na wale wanawake wengine walionekana kama ni wamama watu wazima kabisa kama mama yangu.
"Kusema ukweli Mama mimi rozinta ni mpenzi wangu sasa aliniambia kuwa wewe unaumwa na amekuja huku kukuuguza sasa aliondoka kama mwezi hivi uliopita sasa baada ya kuona kimya ndio nikaamua kuja huku baada ya kuulizia sana."Nilimwambia mama rozinta ambaye wenzake wakaangua kicheko cha nguvu kilichozidi kuniumiza moyo lakini mama rozinta akawanyamazisha wale wenzake na kuniangalia mimi kwa huruma akashusha pumzi na kuniangalia kwa makini.
"Mmmmh Wewe ni kijana mtanashati sana mwanangu lakini ulipoingia hapo sipo mimi rozinta ni binti yangu wa kumzaa kabisa lakini mtoto huyu ameshindikana maana nimemwambia sana kama mzazi lakini wapi wazee wazima wamemwambia kuhusu menendo yake lakini hakusikia sitaki kukubali kuwa watu walipoona una uhusiano naye hawakukuambia chochote maana sifa zake zinatambaa ameshawamaliza wengi hapa kijijini.na anaendelea kuwamaliza huko mjini mimi sina cha kukuambia zaidi ya kukushauri Kuachana naye rozinta nenda kapime afya yako mapema ili upate kujua umeathirika au la Samahani sana kwa yoyote aliyokufanyia binti yangu maana wanaume wengi kama wewe wanakuja hapa pale tu rozinta anapoharibu rozinta hajaja hapa kama miezi mitano hivi cha muhimu mtafute huko huko."Maneno ya mama rozinta kwa hakika yaliniingia barabara na niliyasikia vyema sana na kuyachanganua katika ubongo wangu.Sikutaka kuamini moja kwa moja kuwa eti rozinta anaweza kunisaliti mimi kwa sababu alionyesha mapenzi ya dhati kabisa kwangu bila ya kuaga nikanyanyuka na kuondoka huku kichwa changu kikiwa na mawazo mengi.Roho iliniuma sana kwa yale maneno ya mama rozinta ambaye aliniambia tabia ya mwanae ambaye alisema kuwa ameshawamaliza wengi kijijini.
"Daaaaah hivi na mimi kweli eti nitakuwa nimeathirika haaa siamini."Nilijiwazia mwenyewe baada ya kupanda gari na kukaa kwenye siti gari ya kurudi nilipotokea kwa hakika akili yangu ilikuwa imechanganyikiwa kabisa.safari ya kurudi nilipotoka ikaanza na gari ile kwa mwendo kasi ilianza kukimbia kuelekea nyumbani na kweli muda wa masaa matatu gari likafika kituoni ninaposhukia nikashuka na kuelekea nyumbani kwa mwendo wa mdogo mdogo.Nikafika nyumbani na kumkuta mama mwenye nyumba akiwa barazani anapunga upepo na aliponiona alionekana kuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua maana alikuwa ajui nitokako.
"Vipi mwanangu pablo umeenda huko! Umefika umemuona Mama rozinta? Rozinta je." Mama mwenyenyumba akinitandika maswali yaliyozidi kunichanganya kichwa changu na kwa hakika sikulijibu hata moja nikampita kama sikumsikia vile haraka nikaingia chumbani kwangu na kujibwaga kitandani na kuanza kuwaza na kuwazua.
"Sasa rozinta atakuwa ameenda wapi sasa kama nyumbani kwao tu hajaonekana muda mrefu.mmmh inanipa wasiwasi eee rozinta mpenzi upo wapii." Masikio yangu hayakutaka kusikia kabisa nilichoyasikia na sikutaka kabisa kuamini kile nilichokisikia hata kwa mama yake rozinta.Yale mapenzi motomoto tuliyokuwa tunapeana mimi na rozinta kwa hakika yalinipagawisha kupita maelezo na maneno yote niliyoambia kuwa rozinta alikuwa malaya hayakuniingia kwa sababu sikuwahi kumuona akifanya huo umalaya.Nikiwa naendelea kuwaza ghafla mlango wangu ukagongwa jambo ambalo lilinishtua na kunipa shauku ya kutaka kujua nani mgongaji nikakurupuka haraka haraka huku nikitaka kujiaminisha kuwa aliyekuwa anagonga alikuwa rozinta.Nikaenda mpaka kwenye mlango nakuufungua lakini uso kwa uso nikakutana na Mpangaji mwenzangu wa kiume ambaye alionekana kama kuna kitu anataka kuniambia.
"Karibu."
"Hamna kaka sasa nataka unisindikize sehemu muhimu kaka."
"Aaaaaa Mwanangu nimechoka halafu kichwa kinaniuma ile mbaya siwezi kwenda."
"Aaaaa pablo hutojutia wee nisindikize ukaone fahari ya macho maana haifilisi duka." Mpangaji mwenzangu ambaye aliniambia kuwa anataka kunisindikia sehemu alinishawishi kumsindika sehemu ambayo mimi sikuwa naijuia haraka bila ya kubadilisha nguo nikatoka na kuvaa viatu kisha nikafunga na mlango wangu kwa funguo nikatoka na yule mpangaji ambaye alionekana sana kufarihia kutembea na mimi kwa muda ule.Hatukutumbea sana yule mpangaji akasimamisha bajaj kisha akaniomba tupande bajaj na wala sikubisha nikapanda ile bajaj na safari ikaanza kwenda hiyo sehemu ambayo alitaka nimsindikize sehemu ambayo wala
Sikujua tunaelekea wapi.Safari yetu ikafika katika moja ya club kubwa ambayo niliitambua baada ya kusikia makelele Mengi na kuona watu wengi walikuwa wakiingia sehemu ile ambayo sehemu ya kuingilia kulikuwa na mlinzi aliyekuwa akiruhusu watu kuingia na kutoka.
"Aaaaa Sasa mwanangu si ungenambia kama tunakuja club mimi sina pesa ya kiingilio ujue." nikamwambia mpangaji mwenzangu ambaye alicheka sana baada ya kumwambia vile.
"Hahahaha nimekwambia unisindikize yani kila kitu mshua Mimi tatizo lipo wapi."
"Aaaaa mimi sikai sana nina mawazo kibao me nikajua nikusindikize labda sehemu unaenda kuchukua hela mshaba kweli wewe."
"Aaaaa pablo bwana tuingie na samahani nilitaka kukuprise ni nikuonyeshe mitaa maana utembei tembei wewe."Nilikasirika sana baada ya kugundua yule mpangaji kunipeleka klabu sehemu ambayo watu huwa wanacheza mziki na kunywa vinywaji na kustarehe na wapenzi wao.Sikuwa na ujanja tena baada ya mpangaji wenzangu kuniahidi tutakaa kidogo tu na pia nilifurahia moyoni baada ya kuona kuwa pia ilikuwa ni nafasi ya mimi kubadilisha mawazo yaliyokuwa yakiniandama sana.Mpangaji mwenzangu akalipa pesa wote tukaingia ndani na kuaanza kusikia ule mziki vizuri mamia ya watu walikuwa wakicheza na kuruka ruka huku kila mtu akionekana kufurahia hali ile.Ilikuwa sehemu nzuri kwa sababu wote walikuwa wanacheza kiustaraabu na hata mziki uliokuwa unapigwa na dj uliwaburudisha wengi mpaka mimi baada ya kuingia nikaanza na kujilazimisha kucheza na kutaka kumuomba dada mmoja nicheze naye lakini mpangaji akanizuia na kunishika mkono na kunipeleka mpaka sehemu ya vinywaji ambapo akaniambia niagize chochote na yeye akaagiza maji na mimi nikaagiza soda kutokana na kutopenda kutumia kilevi chochote.
"Pablooooo Mwanangu sehemu pazuriii eeeee."
"Sanaa mwanangu mziki mzuri kwa hakika unabadilisha sana Mawazo."
"Hahahahaha sana Hiii hebu cheki yule jamaa anavyopigana mabusu na bwana wake." Mpangaji Mwenzangu ambaye ndio mtu wa kwanza kuniambia kuwa rozinta alikuwa malaya akaniambia huku akininyooshea kidole ili niangalie kile ambacho aliniambia Haraka nikageuka huku mkononi nikiwa nimeshika chupa ya soda na kuangalia ni nani huyo aliyekuwa anapigana mabusu na bwana wake.Ghafla nikapata mshtuko wa ghafla moyo ukaanza kudunda na macho kunitoka na kujikuta nikitumbua macho kwa nguvu ili nione nilichoambiwa chupa mkononi ikanidondoka baada ya kumuona mwanamke aliyekuwa akipigwa Mabusu hadharani na kusikwa shikwa na jamaa huku wakiwa wamesimama wakicheza mziki huku wakishangilia na watu.Mwanamke huyo mrembo ambaye aliwavutia wengi waliokuwa wakimuangalia alivyokuwa akinyonyana denda na yule jamaa kiufundi alikuwa si mwingine bali ni rozinta........
Hasira za ghafla zikanipanda sikutaka kukubali kabisa kile ninachokiona taratibu nikaanza kujisogeza huku nikiwa nimekunja ngumi kwa hasira.Mpangaji mwenzangu akaanza kunizuia ili nisiende pale.
"Aaaa mwanangu pablo sasa kausha kausha bwana wewe kidume mademu wapo kibao mademu wapo wengi sasa unataka kufanya nini pablo pablo."Mpangaji mwenzangu akajaribu kunizuia lakini wala sikutaka kuzuilika nilipoona ananizingua kwa kunizuia mkono ukanitoka na kujikuta nikimtwanga ngumi kali mpangaji mwenzangu ngumi iliyompata sawasawa kifuani na kupelekea adondoke chini.ila hali watu hawakuona watu wengi walikuwa bize na kuwashangilia rozinta na yule jamaa ambao walikuwa wanataka sifa pale walikuwa wananyonyana denda na kutomasana sehemu mbali mbali na kuzidi kuwakosha watu ambao walizidi kupagawishwa pia na dj ambaye alikuwa akipiga mziki na kuongea kwa kuimba kwa kutumia maiki yake na kunogesha kabisa hali ile.Nikapishana na watu na kila aliyekuwa mbele yangu nilimsukumiza kwa nguvu na kumtoa mbele yangu hasira zilizidi kuongezeka kila dakila nilikuwa nahema juu.kwa kutumia nguvu nikafanikiwa kupenya na kuwafikia mpaka pale ambapo sikuuliza kwanza nikawatenganisha rozinta na yule bwana wake kwa kuingia kati na kumsukumiza kila mmoja na kusababisha watu waliokuwa wanawashangilia kunyamaza.Nilipofanikiwa kuwatoa walivyokuwa wamekombatia nikapeleka kibao kikali kwa rozinta ambaye alionekana kama amelewa lakini kibao kile kikavuruga pombe kichwani mwake.
"Weee rozinta unafanya nini Hapaa hapaa ndio kwa mama nakuuliza hapa ndio kwa Mama."Nilimwambia rozinta kwa hasira huku nikimtingisha kwa hasira yeye baada ya kugundua ndio mimi akaanza kunishika mkono yangu na kutaka kunitoa nisiendelee kumtingisha.
"Weee kaka vipi mshamba nini uwiii niache bwana niache Erik mtoe huyu simjua ananiumiza."Rozinta alilamika huku akilia na kuzidi kunipa hasira na kujikuta nikinyoosha mkono nimzabe kibao cha pili lakini ile nataka kumtandika mkono wangu ukadakwa na nilipogeuka mzima mzima nikachotwa mtama mzito uliosababisha niende chini nifikie mgongo na kusababisha niachie mguno wa maumivu kutoka na mtama ule kuniingia kisawasawa.
"Weee kama nani unamtandika kibao demu wangu fala wewe rozintaaaaaaa!"
"Abeeee baby."
"Huyu Panya ndio naniiiiii huyu mpaka anakutandika kofi mke wangu."
"Namshangaaa baby yani kaniumizaaa usoni mpaka nimevimbaa hata simjui baby kama vipi waite na wenzako mumdunde maana kaniumiza na wala simjui."Sikuamini kabisa maneno ya rozinta yalitoka mdomoni mwake hasira zikanipanda tena nikajizozoa na kuamka na kutaka kumvamia lakini nikapewa pigo la ngumi kali ya kifua na yule jamaa ambaye nilimsikia rozinta akisema anaitwa erick pigo ambalo lilinifanya nipepesuke lakini nikasimama imara na kukunja ngumi kisha nikamrushia makonde mawili ya uso na kumpata yule jamaa ambaye aliinima chini kwa maumivu.Mziki ukazimwa baada ya hali ile kutokea watu wakawa kimya kuangalia mtanange ule wa ghafla na hali ile ikanipa bichwa na kujikuta nikikata tena kumvamia yule jamaa erick na kusahau kuwa mimi nilikuwa mgeni na maeneno yale yalikuwa ni ya wenyewe.
"Mvamieni Huyooooooo!!" Kabla hata sijamtandika erick yule erick akawaita wenzake ambao walikuwepo mule na kusababisha mtafuruku kutibuka na kuniandama kwangu.baada ya erick kusema vile nikajikuta nikipigwa na butwaa na kutaka kujihami na kuangalia huku na huko kuangalia nani anakuja baada ya kusikia maneno mvamieni huyo.hali ya kuangalia ilikuwa ni kuchelewa kwangu kushangaa kushangaa nikajikuta nikitandikwa ngumi kali ya uso na kabla hata sijakaaa sana teke kali ilikatua mgongoni na kusababisha niyumbe huku nikitoa miguno ya maumivu na kabla hata sijakaa sawa mtama mkali mwingine ukanipeleka chini na wote waliokuwa wananipiga nilikuwa wala siwajui.nilijikwamua kutaka kunyanyuka lakini hali ilikuwa tofauti kama nilivyotegemea watu waliokuwa wananipiga ambao baada ya kuwaangalia walikuwa watatu wakaongezeka wengine watatu ambao walikuja pale kunishindilia kwa kunipa mateke na kunikanyaga kanyaga sehemu mbalimbali mwilini na kunisababishia maumivu.
"Maaaaaaaaamaaaaaaaa! Ananikanyaga kwenye korodaaaaaani !." Hakika kipigo changu kiligeuka furaha kwa wengine waliokuwa kimya ambao baada ya kuniona napigwa wakawa wanashangilia kupelekea mpaka dj kuanza kupiga mziki tena na kusababisha watu waanze tena kucheza cheza.
"Apigweeeeee huyo mpigeeeeeee mpigineeni." Katika sauti nilizosikia kuamasisha watu waendelee kunipiga alikuwepo pia na rozinta ambaye aliendelea kuchochea nipigwe.Harakati zangu za kujinasahau kwa hakika zilionekana kugonga mwamba lakini mpangaji mwenzangu akiongozana na jamaa mmoja ambaye alikuwa baunsa na shati yake aliyovaa iliandikwa security wakaja kutawanyisha watu waliokuwa wananipiga na sisi tukatolewa nje kama wezi.
"Oyaaa mwambie Fala huyo hiyo Morogoro." Yule mlinzi alisisitiza baada ya kutotoa nje mimi nilikuwa hoi kwa kuchoka na kipigo shati yangu niliyovaa ilichafuka kwa kuloa damu kutokana na kipigo kile.Kilichonisaidia ni kwamba wale majamaa waliokuwa wamenipiga hawakutumia silaha yoyote kunipigia walitumia ngumi tu na mateke na kusababisha wanitoe damu kidogo maeneo ya paji la uso na mdomoni kutokana na ngumi kadhaa zilizonipata huku nikiwa na maumivu maeneo ya tumboni na mbavuni na maeneno ya sehemu zangu za siri kutokana na mateke.tulipotoka mpangaji mwenzangu akachukua bajaj kuelekea Nyumbani na ndani ya bajaj mpangaji mwenzangu alikuwa kimya kabisa na kuniangalia kwa kuogopa ogopa.
"Yani mimi rozinta wa kunifanyia vile wa kunifanya napigwa mbele ya watu ambao walikuwa wanashadadia kupigwa tu kisa tu nimemfumania na Mwanaume mwingine daaah nilimpa kila kitu anachotaka na mara ya mwisho nilimpa laki nne jamani leo wa kunifanyia vile daaa sasa najuta kwanini sikusikiliza kila mtu aliyekuwa ananiambia kuhusu rozinta daaah kweli usilolijua kumbe usiku wa giza."Niliongea kwa uchungu tukiwa ndani ya bajaj ile tunaelekea nyumbani hakika sikuamini kabisa kama rozinta ndio kanifanyia vile.
"Mwanangu pablo haina haja kulalamika cha msingi nenda ukapime au nitakupelek..." Kabla hata mpangaji mwenzangu ajamalizia nikajikuta nikimkunja na kutaka kuanza kumtandika jambo ambalo lilisababisha mpaka mwenye bajaj kusimamisha bajaj.
"Weeee ndio umesababisha tena nyamaza nitakupasua."
"Aaaaaa pablo kausha bwana mimi nilikupeleka kule ili kujua Kwamba rozinta ni kweli malaya na wala hasingiziwi kama unavyofikiria pia kama kijana mwenzangu nilitaka ili uwai mapema labda uende ukapime kabla mambo hayajabadilika."
"Ila kweli kesho lazima niende nikapime." Nilikubali maneno ya mpangaji mwenzangu na kutulia kabisa na hapo safari ya kurudi nyumbani ikachukua hatamu machozi yalikuwa yananitiririka mashavuni na hapo ndio maneno ya mama yangu mzazi yaliponirudia kichwani mwanangu na kusababisha nikumbuke ya nyuma.........
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA THELATHINI
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com