LISEME JINA LANGU (8)

Zephiline F Ezekiel
0
Mwandishi: Pablo

SEHEMU YA NANE
"WEWE NI MWANANGU NA KAMWE HAUWEZI KUNIKIMBIA MIMI NAPENDA KUKWAMBIA NIKUKAMATA WEWE NA HUYO MBWA WAKO VICHWA VYENU HALALI YANGU".......

SASA ENDELEA...
Baada ya kusema maneno hayo yaliokuwa yakitoka kinywani kwa baba moureen kupitia kwenye simu wote tukajikuta kwa hofu tukiangaliana huku kila mmoja akiwa ana waza lake tukiwa ndani gari hilo huku mimi nikiendelea kukiangalia kidonda changu ya sehemu niliyopigwa risasi.tukiwa katika hali hiyo ghafla simu ya moureen ikaita tena na kwa shauku kubwa wote tukajikuta tukiweka mkazo wa umakini kuangalia simu hiyo iliyokuwa ikiita.

"Moureen unaendeleaje huko."
"Baba amenipigia simu na kuongea maneno ya kutisha huku akisisitizia akitukamata basi vichwa vyetu halali yake"
"Dooo vp Pablo anaendeleaje hapo."
"Kidogo anaendelea vizuri."
"Pouwa basi ondokeni haraka sana kutokana sasa hivi wameichukua simu yako na kuanza kuingiza katika computer kwa lengo la kujua upo wapi."
"sasa tuelekee wapi doctor"
"Bagamoyo nendeni mpaka makumbusho ya taifa kisha kachukueni vile vyumba vya kule ufukweni muutulie kisha tupa hiyo laini na sajili nyingine halafu nicheki hakika unampa dawa pablo anywe." simu ilikatika na kumfanya moureen ashushe Pumzi ndefu na kuniangalia mimi niliyekuwa namuangalia kwa makini moureen.hakusita kunisimulia habari ya doctor aliyekuwa akiongea naye huku akisema kwamba ndiye yeye alinisaidia kunitoa risasi niliyopigwa na kunitibia vidonda vyangu vya mguu nilivyojichoma na vyupa na tena akiendelea kunisisitizia kwamba kwa sasa ni yeye tu ndiye mkombozi wetu kutokana na kutupa kile kinachojiri kutokana na yeye kuwa daktari akina moureen nyumbani kwao.Bila ya kupoteza muda moureen akawasha gari kwa mwendo wa haraka na kuliingiza katika barabarani kutoka katika msitu mnene niliokuwa siufahamu kwa muda huo kutokana na kutotaka kuuliza.kwa mwendo wenye spidi ya hali ya juu moureen akafanikiwa kufika mwenge mapema tu na kukuta foleni katika mataa ya pale mwenge kuelekea lugalo foleni ambayo ukubwa wake ulitufanya tuingie hofu.tukiwa katika hali ya foleni katika barabara hiyo la mwenge ghafla kundi kubwa la watu waliokuwa katika pikipiki huku wakivaa suti nyeusi wakiambatana na miwani wakaanza kuzunguka katika foleni hiyo huku wakikagua kila gari watu waliokuwepo humo.hali ya hofu ikatanda dhidi yetu huku na kuanza kuomba mungu.Lakini kabla hata ya kufika kwetu taa za kuruhusu magari ya upande wetu ikawaka na moja kwa moja moureen akachomoza gari haraka na kuwapita baadhi ya magari kwa kuovertake haraka haraka jambo ambalo halikuonekana na matraffic na wale watu waliovaa suti na kuwaacha wakibaki wakikagua magari mengine.Hakika baada ya kupita pale hatukupata vizingiti vingine huku kwa saa kama saa tatu usiku tukafanikiwa kufika bagamoyo Na kutokana na moureen kuwa na pesa akachukua chumba ambacho kwa usiku huo tukalala wote kwa mara ya kwanza na kutofanya chochote na kulala mzungu wa nne katika kitanda kimoja.hakika siku zilizidi kuchomoka huku moureen akizidi kuwasiliana na doctor huku akizidi kutupa habari zilizozidi kunichanganya kwa sababu aliniambie wanataka kupandika picha za wanted kuwa mimi nimteka moureen.tulikaa siku kama Nne katika chumba hicho huku hali yangu vidonda vyangu vikiendelea vizuri na kunifanya nijisikie mzima huku vidonda vyangu vikipona kabisa.ilipofika siku ya tano usiku tukiwa ndani ya chumba cha hoteli ambayo tumepanga Tukiwa tunaangalia Movie iliyokuwa ikionyesha kwenye dstv ndani ya television iliyokuwepo chumbani humo ghafla scene ya mapenzi ikaanza kuonyesha kwenye movie hiyo na kusababisha moureen aniangalie kwa macho maregevu kisha akanisogelea

"Baby tangia uwe na mimi hatujawahi kusex niliku...."kabla hata moureen hajamaliza akaanza kunishika koki yangu iliyokua ina hamasika kidogo kidogo kwa kuangalia movie hiyo iliyokuwa inanisisimua.hakika sikumjubi chochote nikapeleka mdomo wangu katika mdomo wake na kuanza kunyonyana naye denda huku mkono wangu ukianza kuchezea matiti yake na mwingine nikipapasa ikulu yake hali iliyomfanya moureen akiruka ruka huku akihema kwa kutuo miguno ya raha iliyokuwa inanisisimua kwa hali ya juu.hakika ilipita kitambo sana sijafanya mapenzi kwa hiyo chance ile aliyonipa moureen niliona kama lulu huku nikijikuta nikipania mechi na kuanza kumvua nguo moja moja moureen aliyekuwa analegea pole pole.lakini baada ya kumvua nguo kabla hata hatujaendelea simu yake ikaita na kunifanya nisite kuendelea kumchezea moureen huku moureen mwenyewe akitaka kuipuuzia simu hiyo.nilijikukota kiuvivu na kuangalia ni nani aliyekuwa akipiga.si mwingine bali alikuwa ni dokta nikaipokea kwa tahadhari kubwa na kuanza kumsikiliza.
"Hakikisheni mnaondoka Haraka Washafika b.........." simu ile ikanichanganya baada ya kukatika na kumuambia moureen ambaye baada ya kusikia taarifa hilo alikurupuka kwa haraka na kuanza kuvaa kisha wote tukatoka na kwenda kulipia haraka haraka na kwenda kuchukua gari letu lakini ile tunaingia barabarani kwa lengo la kuondoka baada ya kuingia Katika gari.
"Paaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa"Mlio wa kupasuka katika kioo cha gari yetu ukasikika ukifuatiwa na ukelele mkali kutoka moureen aliyeokena kudhurika kwa kiasi kikubwa kutokana na kioo kuvunjikia karibu yake kutokana na yeye kuwa dereva..

Baada ya kutoa ukelele huo moureen akazimia na kushababisha gari ianze kuyamba yumba jambo lililonifanya nianze kwenda kukaa sehemu hiyo ya udereva kwa shida ili niendeshe mimi kutokana na gari hiyo kutaka kupoteza uelekeo kutokana na mshtuko alioupata moureen aliyekuwa akiendesha gari na kumfanya azimie baada ya risasi kuvunja kioo hicho.kabla hata sijaanza kukanyaga breki ili kupata uelekeo mzuri wa gari hiyo lilokuwa likiyumba yumba ghafla gari letu likapigwa kikumbo kikali na gari nyingine na kushababisha gari letu kuvamia genge la vitu vya sokoni lililokuwa limefungwa usiku huo na kufanya nipate maumivu makali kutokana na kugongwa gongwa na mbao zilizoambata na mabati ambayo hayakusita kunikata pale yalipogusa mwili wangu.Ila licha ya kuingia katika mkumbo huo wa kuvamia genge lakini gari letu halikuzimika huku mimi nikiwa bado naliendesha na kukanyaga gia namba sita ambayo ilikuwa inasaidia gari letu kwenda kwa kasi ya ajabu.Nyuma yetu tulikuwa tunafatwa na magari kama sita ambayo kila gari lilikuwa linatugonga pale yanapotufikia huku wakitumiminia risasi ambazo ziliendelea kutoboa vioo vya gari katika upande wa nyuma huku kioo cha mbele kikiwa kimetoka kabisa.moureen alikuwa kazimia jambo lililomfanya ayumbe yumbe ndani ya gari lililokuwa nikiliendesha mimi kwa kasi kwa lengo la kuwakimbia wanaotufukuza ambao walikuwa si wengine bali ni kundi la robert mugalula.kutokana na speed yangu kuwa kali nikajikuta nikiingia katika korongo la msitu ambao hata nilikuwa sipajui ni sehemu gani lakini ilikuwa maeneo ya bagamoyo.nilijitahidi sana kukanyaga breki ili lisimame lakini lilikataa kutokana na mteremko mkali ambao ulinifanya nikate shauri yakutoka huku nikimshikilia moureen aliyekuwa ajitambua na kuangaika kuufungua mlango kwa lengo la kutoka nje kutokana na mteremko huo kuonekana mbele yake kuwa na miti mikubwa ambayo kama gari hilo likigonga na sisi kuwepo katika gari hilo lingetusababishia maafa.nikiwa katika kufanikiwa kuufungua mlango huo wa gari nikaanza kusogea haraka haraka huku nikiwa nimemshikilia moureen ambaye sikutaka kumuacha licha ya kuwa katika hatari kubwa ambayo kama ningelitoka mimi basi ningekuwa tayari nishatoka.kwa hali ya kujiandaa kabisa baada ya kuufika mlango ile nataka kutoka tu gari lisilojulikana lilipotokea likaja kugonga mlango huo ambao ukajibamiza na kunibana mimi kwenye maeneo ya mbavu na kunifanya nitoe ukelele mkali sana wa maumivu huku damu nyingi zikianza kunitoka kutoka na mlango huo kunibana sawa sawa.nikiwa katika hali ya kuugulia sehemu hiyo niliojibana macho yangu yakagonga katika mti mkubwa uliokuwa mbele yetu ambapo gari letu lilikuwa likielekea palepale.Nikajikuta nikifumba macho na kuanza kumuomba Mungu aniokoe katika balaa lile na kwa hofu kubwa nikajikuta nikizimia kwa hofu kabla hata ya gari letu kugonga mti huo na kunifanya nisielewe kilichokuwa kinaendelea...

"Mmmm..ooooh..aaaa mama..nakufa..naumia yalaaa.oooh"ilikuwa ni miguno ya kulalamika niliyoitoa baada ya kuamka na kujikuta nikiwa nimefungwa kichwa chini miguu juu katika mti mkubwa ambao ni kamba tu ndio ilikuwa imefungwa katika miguu yangu na kupitia katika mti na kunifanya nibembee kichwa chini miguu juu.maumivu nilikuwa nayasikia kila sehemu huku damu nyingi zikiwa zinanitoka katika sehemu mbalimbali za mwili zilikuwa zikichuruzika chini huku nikishuhudia mwenyewe katika macho.maumivu niliokuwa nayapata nahisi ilikuwa bora nife kutokana na majeraha hayo kuuma.nikiwa na hali ya kushangaa shanga nikamuona mtu mwingine akiwa amepigishwa magoti huku akiwa uchi na mwili wake mzima ukiwa umetapakaa damu ambaye alikuwa kafungwa kamba mikononi na miguuni.niliangalia sura yake kwa makini kutokana na yeye kuniangalia mimi kwa huruma jambo lililonifanya nimtambue kuwa alikuwa ni dokta ambaye alitusaidia katika mikasa iliyopita.nikiwa katika hali ya kumuangalia kwa huruma ghafla mlio wa risasi uliopenya katika kichwa cha yule dokta ukasikika na kupasua kichwa chake na kufa papo hapo na kunifanya nitoe macho kama nimebanwa na mlango.Ghafla nikamuona robert mugalula aliyekuwa amefungwa bandeji kichwani kwake akasogea huku akipuliza bunduki ambayo alionekana ndio yeye alimlipua dokta kisha mkono wake mwingine akiwa ameshika mkia ambao baada ya kuuangalia kwa makini ulikuwa ni mkia wa taa.akanisogelea kidogo na bila ya kunisemesha akaanza kurusha rusha mkia huo na kuweka sawa kwa lengo la kunitandika nao mimi ambao kabla hata sijapigwa nikahisi mkojo kutokana na sifa kubwa ya mkia wa taa ambao niliusikia tu kwa juu juu ni jinsi gani unavyoumiza.
"YAAAALAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA...

Nilijikuta nikipiga ukelele wa nguvu wenye maumivu makali ambayo hayakuweza kuvumilika hii ni baada ya Robert kufyatua mkia ule wataa aliokuwa ameushika na kunichapa nao kwenye kidonda changu nilichokua kinaniuma hii ni baada ya kujibana na mlango wa gari na baada ya kuchapwa na mkia ule wa taa maumivu yalianza kurudi upya huku nikiishuhudia mvumuko wa damu nyingi zilizokuwa zikimwagika kama maji katika kidonda changu hicho.sikuweza hata kushika kidonda changu kutokana na kushindwa kukifikia kwa sababu nilikuwa nabembea baada ya kufungwa kichwa chini miguu juu.Baada ya kunichapa mkia ule robertson alitulia kwa muda huku akiniangalia kwa hali ya kukunja sura yake.Akiwa katika hali ya kuniangalia ujio mwingine ukaja walikuwa ni baba yake moureen aliyeambatana na wafuasi wake ambapo bila hata ya kumuongelesha robertson kwa ishara tu akaomba mkia wa taa baada ya kupewa akanisogea kisha akaimaliza kuichana shati yangu iliyokuwa imeshachanika na kuimalizia kabisa na kunibakisha tumbo wazi kabisa.akaanza kunitemea mate yasiokuwa na idadi kisha bila ya kunionea huruma akaanza kunikojelea huku akinishindilia matusi yasiokuwa nampangilio baada ya kumalizia kunitukana na kunitemea mate akarudi nyuma kidogo na kuaanza kuuzungusha mkia wa taa na bila ya kukosa na yeye akanilenga pale pale na kunifanya nipige kelele mpaka sauti ikakauka na kutoa machozi ambayo kwa mara ya kwanza nililia mpaka machozi kukauka.baba yake moureen akaishia hapo aliendelea kunitandika baadhi ya sehemu huku kila sehemu mkia huo ulikuwa unanichana na kuniweka Alama kubwa kutokana na mkia huo kuwa na mibamiba.

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO



USIKOSE SEHEMU YA TISA

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)