
SEHEMU YA HAMSINI NA TANO
Rose alipo sikia hivyo akaachia tabasamu kamili, “kwahiyo tume kubaliana?” aliuliza kwa shahuku Rose, pigia mstari tena tuwai mapema tuka faidi baridi”SASA ENDELEA...
Alisema Edgar, huku Rose akionyesha kuchangamka alichukuwa simu yake kwenye mkoba, na kuanza kuandika ujumbe, ‘yani sijuwi kama nita weza kuingia Songea leo, maana gari lime zima ghafla hapa iringa wakati nakula, ndio natafuta mafundi’ aliituma sms hiyo nakuirudisha simu kwenye mkoba wake, wakaendelea kula mpaka walipo tosheka, kisha safari ikaendelea kuitafuta mafinga
Ophia na mama yake walirudi ndani na kumsimulia mzee Mashaka jinsi maongezi yao na Suzane yalivyo kuwa, wakimweleza jinsi Suzane alivyo pania kulifikisha lile swala polisi kwa kutegemea ushaidi wa mtu aliewaona wakimteka Edgar, na camera za benk, hapo mzee Mashaka ambae alikuwa hawezi kuongea, akaandika kwenye karatasi maneno marefu hivi, kisha akamkabidhi mke wake, mama Sophia akaisoma ile karatsi, iliyo mwelekeza kuwa, apekuwe kwenye ssuluali yake yliyo kuwa ame ivaa jana achukuwe simu yake na pia kuna kinote book, kwenye mfuko wa shati akiviona amletee, lakini mama Sophi akamwambia vitu vile vipo kwenye meza iliyopo pembeni yake, maana vilitolewa jana wakati walipokuwa wanamtibu, na simu ilizimwa baada ya yeye mama sophia kufika Hospital, basi hapo mzee Mashaa akamwonyesha ishala ya kuomba simu na note book
Wakati huo Suzane alikuwa anaingia nyumbani huku simu na ya Edgar ameshazizima kabisa, na hakutaka mawasiliano na wakina sophia na mama yake, maana alijuwa fika Edgar atakama ni mzima hakuwa na mawasiliano kabisa, japo alitamani sana asikie neno ata moja toka kwa mpangaji wake huyu wa zamani, ili ajuwe kama bado anampenda au la, maana alijuwa wazi kuwa, lazima mzee Mashaka amesha ambiwa, juu ya uhusiano wake na Edgar, na ndio maana alimteka kwa nia ya kumduru mpenzi wake huyo, sasa wasi wasi wake nikuwa, kama Edgar amenusulika, je atakubari kuendelea na yeye kama wapenzi?, naukweli nikwamba hakuna kipindi alichokuwa anmwitaji Edgar kama hiki, ukiachilia kuimisi dudu, lakini pia alitamani kumweleza kuwa anaujauzito wake, Suzan aliingia ndani mwake na kuangalia mle ndani, akaona nguo zote za Edgar zipo vile vile, ikimaanisha Edgar akuingia kuchukuwa chochote mle ndani, akiwa mwenye mawazo mengi na mkosefu wa hamu ya kula Suzan alijilaza kitandani nakupitiana usingizi mzito sana
Huko Songea mzee Haule yani baba Edgar, alishangaa kuona mwanae toka jana hakuwa ame pigia simu, naata mkwe wake ambae bado hajawai kumwona atamala moja, naye pia aikuwa kawaida yake kuto kupiga simu japo mala moja kwa siku ili kumjulia hali, yeye na mamayao, akaona hisiwe shida akachukuwa simu yake na kuipiga, kwa lengo la kumsalimia na pia kumjulisha uwepo wa shemeji yake bwana kazole pale nyumbani, lakini simu ya Edgar aikuita ilkuwa aipatikani, akajaribu simu ya mkwe wake nayo hivyo vyo, mzee Haule akaamua kuachana na mawasiliano kwa muda hule, nakupanga kuwa tafuta tena baadae, japo ule ndio ulikuwa muda mwafaka wayeye kuongea na mwanae ili amsimulie ubuyu ulio tokea kwa dada yakre na shemeji yake
Bwana kazole alikuwa ameenda mjini na mke wake ambae alikuwa amejifunga kilemba kichwani kuficha jelaha lililo bandwa bandage, lengo la safari hiyo ni kwenda kufanya manunuzi ya nguo ambazo zinge wa saidia, maana hawa kuwa na nguo baada ya kuibiwa, kama anavyosema bwana Kazole, uku kificha yakuwa alikamatwa ugoni fake, “yani jitahidi uongee na baba, naimani atatusaidia , anaonekana anafedha nyingi sana, ona alivyo kusanya mazo, ona duka lake lilivyo kuwa kubwa, au tuongee na Edgar ndio itakuwa vizuri” aliongea bwana kazole akionyesha anania ya dhati kabisa kuomba fedha kwa baba mkwe wake, ambae licha ya kumkaba usiku, pia hakuwa anamjari kabisa mzee huyu ambae malanyingi sana, wame chukuwa chakula kwa mzee Haule, na awakuwai kuchangia ata shilingi kwenye kilimo cha jembe la kono cha mzee huyu
“Hilo la kuongea na Edgar ndio gumu sana, maana...” alishindwa kumalizia mke wa bwana Kazole, kiukwelidada yake mkubwa Edgr kila alipo kumbuka jinsi alivyokuwa anamsemea mbovu mdogo wake huyo, “labda wewe uliewai kumtumia ela” aliongea mke wa bwana kazole akijuwa kabisa mume wake alimdanganya, ni kweli bwana kazole nafsi ilimsuta, akajichekesha kinafiki bila kujibu, safari yao ilifanikiwa wakiwa wame nunua nguo na viat, pia waka pitia shule ya mfaranyaki ambayo bwana kazole alikuwa anafundisha, japo mauzurio yake hayakuwa mazuri huku mwalimu mkuu wa shule hiyo, akijitaidi kummfichia madhambi bwana Kazole, hapo shuleni bwana kazole alisimulia mkasa liompata uku akificha baadhi yamambo, nakusema kuwa alivamiwa na wezi, na siyo fumanizi fake, basi mwalimu mkuu akampatia mapumziko ya wiki mbili, ili aweze kutatua matatizo yake, hapo safari ya nyumbani kwa mzee Haule ilianza, huku njia nzima bwana Kazole akiwaza namna ya kufanikwa kujipatia fedha kwa mzee Haule
Ili kuwa saa moja usiku, ndiyo mda ambao suzane alistuka toka usingizini, ni tangia alale mchana mda aliotoka Tumbi kuongea na wakina mama Sophia, akiwa ametawaliwa na unyonge Suzane aliinuka toka kitandani na kuelekea sebuleni, ambako akukaa sana, maana aliione ile sebule ni kubwa sana, “Eddy baba utakuwa wapi?” alijisemea Suzan wa sauti ya chini, huku akielekea jikoni, akasimama dkwenye sink la kuoshea vyombo, akitazma nje, kupitia dirishani, ghafla suzan aliachia tabasamu la matumaini, huku akitoka mbio kuufwata mlango wa kutokea mle jikoni na kisha mlango wa kutokea nje, ilikuwa ni baada ya kuona taa ina waka chumbani kwa Edgar, chumba kile alicho mpangishia, alipo ufika mlango wa chumba kile akaufngua, nao ukafunguka kuashiria kuwa upo wazi
Suzan akiwa na imani kuwa Edgar yupo mle chumbani, aliingia ndani ya chumba kile kwa speed na vurugu, lakini alicho kitgemea akikuwepo, zaidi Suzan alikuta kuna karatasi yenye maandishi kitangani, akaisogelea taratibu na kuiokota huku mapigo ya moyo wake yakimwenda kasi, Suzan alianza kusoma kilicho andikwa, huku hofu ikiwa ime mtawala, lakini kadili alivyo kuwa akisoma, ndipo uso wake ulipo anza kubadilika na kuwa wenye furaha, ‘suzan mpenzi naimani utauona huu ujumbe, mala tu utakapoingia humu chumbani, ndio maana nili acha taa inawaka, usiwe na wasi wasi na mimi, kwani mimi ni mzima, najuwa uutakuwa umesikia kilicho mtokea mzee Mashaka’ suzan alisoma ule kwa umakini sana, akaelewa kuwa mzee Mashaka alimteka Edgar kwa leno la kwenda kumpoteza maisha, lakini Edgar akafaniiwa kuwa toroka,pia ule jumbe wa Edgar uli msisi tiza Szane kuendelea kufanya mipango ya kuhama dar, akiamini aikuwa sehemu salama kwao
‘Hii sasa unapousoma huu ujumbe naimani nitakuwa nimesha pata gari, kwani naelekea kudandia magali ya izigo yaendayo songea’ nikifika nitakujulisha, nakupenda sana Suzane’ ujumbe uliishia hapo, wakati Suzane anamalizia kusoma ujumbe huo, akasikia sauti ya mwanamke kwambali ikibisha hodi, akatoka haraka nakuufwata mlango wa nyumba kubwa anayo kaa yeye, kweli mbele ya mlango huo aalikuwepo Joyce, “hoooo Joyce karibu ndani, karibu sana umenikumbuka leo” aliongea Suzane huku akiingia ndani akifwatiwa na Joyce, ambae alimtambua kama wanafunzi mwenzie wa Edgar, sekunde chache walikuwa wamekaa kwenye makochi, “niambie Joyce utakunywa nini” aliuliza Suzane, huku akimtazma Joyce ambae alionekana kukosa amani, “hapana da’suzie mimi nime kuja kumwona mala moja Edgar, nina shida nae,” alisema Joyce akionyesha hali flani ya uoga na unyoge, “hoooo jamani Edgar ameondoka toka jana mchana kuelekea Songea, kwani vipi kuna tatizo?” aliongea Suzane akimtazama Joyce, ambae alionyesha kuzidi kubadirika sura akikaribia kuangua kilio
“Sijuwi nita fanya nini mimi masikini” aliongea Joyce nakumfanya Suzan azidi kushangaa, “kunatatizo Joyce, au ulikuwa una mdai?” aliuliza Suzan kwa sauti ya upole na yakubembeleza, hapo Joyce akazungusha akili, maana tatizo lake ni kuwa, juzi asubuhi alijisikia utofauti kidogo, akaenda kwenye dispensal ya jilani na chuo chao kupima malelia pamoja na UTI, lakini vipimo vikasoma tofauti, ndipo walipo mpima ujauzito, ni kweli Joyce alikuwa anaujauzito, ndipo alipo anza kumtafuta Edgar iliamweleze swala lile lakini tatizo lake likawa moja atampataje, maana chuo alisha maliza, na simu ya Joyce ilikuwa mbovu
Sasa jana alibaatika kumwona Edgar akiendesha gari la Suzan ambae ni mpenzi wake, na Joyce alikuwa anafahamu swala hilo, ndio maana alishindwa kumfwata nyumbani na kumweleza, lakini pia ata alipo mwona awakuweza kuongea maana Edgar alikuwa na haraka zake, akamwahidi kumtafuta baadae, lakini mpaka giza linaingia akumwona, akapiga moyo kode akipanga kutumia hakili kumfikishia ujumbe Edgar , pindi atakapo mkuta yupo na Suzane, akaamua kwenda nyumbani kwao, lakinihakukuta mtu, licha ya kurudia mala mbili, lakini ilikuwa vile vile, siku ya pili Joyce akukata tamaa, alikuja asubuhi na mapema lakini hakukuta mtu, ata mchana pia na jioni akabaatisha kumkuta Suzane
“Simdai chochote ...ila .. ila nina tatizo naitaji msaada wake” aliongea Joyce kwa kusita sita, kama kuna jambo zto anashindwa kulieleza, hali hiyo ili mtisha Suzane, “nijambo ambalo lazima litatuliwe na mwanaume, au atamimi naweza kuitatua?” aliuliza Suzane akionyesha nia ya dhati ya kutaka kumsaidia Joyce, hapo Joyce akaanza kueleza shida yake, lakini akificha ukweli halisi, alielez kuwa yeye amepewa ujauzito na rafiki yake Edgar, ambae alikuwa anasoma darasa moja na Edgar, na huyo mtu alie mpa uja uzito ameondoka kabla yeye kujuwa kuwa anaujauzito, tatizo ni kwamba huyo mtu akujuwi kwao nayeye simu yake imearibika
“Yani hapa sina ata shilingi, yani ninge itoa,” alimaliza Joyce kusimulia, “pole sana,” alisema Suzane nakutulia sekunde kadhaa hapo suzan akakumbuka kitu, “tena nime kumbuka ebu ngoja nikachukuwe simu ya Edgar tuitafute namba yake,” hapo Joyce akajuwa kuumbuka inausika, “unazani anasimu, ameibiwa kabla hajaondoka” alisema Joyce haraka sana akimwai uzan alie kuwa anainuka kuelekea chumbani, hapo Suzane akaanza kuona mapicha picha, nakuhisi kuwa uenda anadanganywa, akawaza mawili matatu na kupat5a picha flani, kwanza kabisa alikumbuka jinsi huyu binti alivyo kuwa anamshobokea Edgar, kila mala anapo wakuta, pia anafahamu kuwa Edgar hakuwa na Rafiki wa kiume zaidi ya rafiki wa kike tena ni huyu Joyce pekee
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA HAMSINI NA SITA
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com