
SEHEMU YA SITINI
“Ameichaji tokea asubuhi, sasa imeisha saangapi?, si asemetu kama ataki niende kwao” alisema Suzane kw manung’uniko, “tena nikuambie best wanavyo kutamani kukuona, yani kila siku nikikutana nao, watakuja lini kutusalimia”SASA ENDELEA...
Aliongea Seline akijaribu kumchangamsha mwenzie, nikweli akafanikiwa Suzane akabadirika na safari yao ikaendelea huku wanaongea mambo mbali mbali, ikiwemo nyumba ambayo Seline ali ambiwa imepatikana mitaa ya seed farm, hivyo wataenda kuinagalia watakapokuwa wanatoka kwa kina Edgar, maana ni upande huo huo, pia kuhusu mizigo gri lilikuwa bado njiani, kumbe Suzane akutaka kurudi kumfwata Edgar akiogopa kumweka karibu na Seline ambae alionyesha dalili za kumtamani
Baada ya kumkosa Suzane pale air port Edgar akuwa na namana akaingia kwenye daladala na kuanza kurudi mjini, akipanga aende akanunue simu nyingine ili awasiliane na Suzane ajuwe kama yupo wapi, na kwanini haja safari, “yani huyu jamaa ni mshenzi kabisa, ame sababisha nime shindwa ku kumpigia Suzie, yani niki juwa kama kweli amechukuwa yeye, atanitambua, hakuna cha ushemeji hapa” aliwaza Edgar akiwa njiani anaelekea mjini kutokea air port, nusu saa baadae alikuwa anashuka kwenye daladala kati kati ya mji, akatazama kushoto na kulia, akitazama aanzie wapi kutafuta duka zuri la simu, akakumbuka jana alinunua simu kwenye duka moja mtaa wa pili toka pale alipo, akaanza kutembea taratibu kuelekea mtaa huo, lakini waati anakatiza kwenye duka moja, akamwona shemeji yake bwana kazole akiongea na mzee moja alie kuwa ndani ya duka hilo, huku akiwa ame shika simu kama ile ya kwake iliyo potea na chaja yake ikiwa juu ya meza kubwa ya pale dukani, hapo hasira zika mpanda mala mbili, akawafwata kwa mwendo wa Nyati, .......
“Shem tabiagani hiyo, ya wizi?” aliuliza Edgar baada ya kuwafikia wakina kazole na mzee Kalolo, bwana Kazole akaishikwa na mshangao, huku mzee Kalolo ambae alisha mkumbuka Edgar, maana limwona sikuile ana wekewa bondi ya shamba nyumbani kwa mzee Haule, akajaribu kumtisha Edgar kiutu uzima, “we kijana jaribu kuwa na adabu, nani mwizi” aliongea mzee Kalolo akimkazia macho Edgar, “unaazani hiyo simu uliyoishika ni yanani?” aliongea Edgar kwa sauti kubwa iliyowafikia watu waliokuwepo eneo lile, kuona hivyo mzee Kalolo akataka kuificha ile simu, “unauakika kuwa hii simu ni yako, ondoka kabla sija kuitia mwizi sasa hivi”aliongea mzee kalolo, akipiga atua kuelekea kwenye makabati yaliyopo ndani ya duka lake, “shem naomba simu yangu, Edgar alimgeukia bwana Kazole ambae mda wote alikuwa kimya, “simu, simu gani?” aliuliza bwana Kazole akijifanya kushangaa, ni baada ya kuona mzee Kalolo amesha ificha ile simu, hapo Edgar aka baki kimya akimtazama bwana Kalolo
Huku ana tabasamu, ni tabasamu lililojaa uchungu, “bwana Kalolo hee, tutaonana baadae,” aliongea bwana kalolo akianza kuondoka baada ya kuona Edgar yupo kimya akizani amesha amesha kubari matokeo, kabla hajapiga atua yapili bwana Kazole alistuka akifyetuliwa miguu na kupaa hewani kisha akatuwa chini na kujipigiza kwenye ngazi, akifikia kiuno ‘pwaaaa’ “mamaaaaa kiuno changu” alipiga yowe bwana kazole, huku akimshuhudia Edgar yani mdogo wa mwisho wa mke wake, akimfwata pale chini na kumkamata, shati lake maeneo ya kifuani, kisha akaanza kumshushia mvua za ngumi, usoni kwake, Edgar alimpiga bwana Kazole ngumi mfululizo za usoni, bila kuacha, huku watu wakisogea pale walipo na kushangilia ugomvi wasio hujuwa
“Utaniua shemeji, kama simu yako nenda kachukuwe” alilalamika bwana Kazole huku bado mvua za ngumi ziliendelea kushuka usoni kwake, “shenzi kabisa, ume sabbibisha mpaka sasa sijuwi Suzie yupo wapi” aliongea Edgar akiendelea kushusha ngumi zilizo tuwa sawia usoni kwa shemeji yake, na kusababisha damu kuanza kuchuruzika sehemu mbali mbali za bwana Kazole, ikiwepo mdomoni na puani, pia kuna bahadhi ya sehemu alipasuka nakutoka damu nyingi zilizo tapakaa usoni kwake na nyingine ziki mrukia Edgar kwenye tishert yake, Edgar alipoona amelizika akainuka na kumzibua teke la ubavuni bwana kazole
“Mwizi mkubwa wewe, tafuta kwakwenda” aliongea Edgar akimwacha bwana Kazole, na kumfwata mzee Kalolo ambae aliuwa bado ndani ya duka, akimwacha shemeji yake bwana kazole akiwa chini huku watu wakianza kumzonga, “mwizi ! mwizi! piga mwizi huyo... piga” kelele hizo za watu ziliambatana na kipigo cha taratibu kwa bwana Kazole,.. edgaqr hakujali aliendelea kumfwata mzee Kazole “we kijana usini sogelee mimi siyo lofa kama huyo ndugu yako...” mzee Kalolo akuwai kumalizia maneno yake alistuka ngumi nzito ikituwa kwenye shavu lake, nakumpeerusha mpaka kwenye ma shelfu yakupangia bidhaa nayo yaka mdondokea huku baadhi ya vitu viki mwangukia sehemu mbali mbali za mwili wake, mzee kalolo huku akivuja damu mdomoni sambamba na kutema jino lake moja, alimwona Edgar akimfwata pale alipo
“Chukuwa kwenye lile kabati” alisema mzee Kalolo akionyesha kabati aliloweka simu, Edgar akataka kwenda kumwongezea angalau ata ngumi mbili mzee yule, lakini akaingiwa na huruma, akamwacha na kuliendea kabati, akafungua na kutoa simu yake ile anageuka kutoka nje akashangaa kuona vurugu kuwa ikiendelea pale nje, hujku bwana kazole akiendelea kupewa kupigo, “msala huu” alijisemea Edgar, akijiandaa kuondoka zake, lakini aikuwa jambo lahisi kwake, mala akasikia ving’ola vya gari la polisiambalo lilisimama pale huku watu wakitawanyika na kuwa kimbia polisi sita walio shua kwenye gari hili aina ya land rover one ten, Edgar alibaki ame duwaa hasijuwe la kufany, aka shuhudia polisi wakimkama tayeye pamoja na wakina Kazole na mzee Kalolo, wakaingizwa kwenye defender, huku bwana Kazole akiwa hoi bin taaban kwa kipigo alicho kipata toka kwa wananchi
“Jamani sisi wawili siyo waalifu mwalifu ni huyu hapa” aliongea mzee Kalolo, akimwonyesha Edgar kuwa ndie mkolofi, “kelele wewe, utaenda kujieleza kituoni” dakika chache alikuwa wenye kituo cha wilaya, jilani kabisa na uwanja wa mpila wa miguu wa majimaji, wakaingizwa ndani na kukabiziwa kwa polis constebo wawili wakiume na wakike ambao walianza kuwa chukuwa maelezo, huku bwana kazole akiandikiw pf 3 nakupelekwa hospitali ya mkoa, kwa matibabu, katika maelezo yake bwana kazole akaeleza kuwa, akiwa na dkani kwake na mteja wake (yani bwana Kazole) walivamiwa na kijana huyo (yani Edgar) nakuanza kuwa shambulia akifanya ualibifu mkubwa sana pale dukani, napia hakujuwa kama kuna hasala aliyo msababishia mwenzie yaani mteja wake bwana Kazole
Kwa upande wa Edgar yeye hakueleze kwa kilefu, alieleza kuwa watu awawawili ni wezi na pale alikuwa amewakamata, wale polisi wawili walimshikilia Edgar huku wakimwandikia pf 3 mzee Kalolo aende akatibiwe na kesho airport pale kituoni, wale polisi waka msweka Edgar mahabusu, “huyu aingie mahabusu, na report hii tumpatie afisa wa zamu nazani atakuja mida ya saa moja” aliongea yule polisi wa kiume, huku waki mtoa vitu muhimu kama simu fedha na mkanada pia viatu na shati, “samahani braza, naomba niwasiliane na nduguzangu niwajulishekilicho tokea” aliongea Edgar kwa sauti ya upole sana, wakati akifungiwa mahabusu, mpaka mida hiyo tayari ilisha timia saa kumi na moja na nusu
“Ok sawa utawasiliana na mtu mmoja tu muhimu, tena dakikamoja tu!” aliongea yule polisi wa kiume huku akimpatia simu yake Edgar, Edgar akaiwasha na sms zikaanza kumiminika kwenye simu yake zikitokea kwa Suzie, lakini hakuwa na muda wakuzisoma, mtu ambae angeweza kumpigia simu ni baba yake ambae alikuwa na uakika kuwa yupo hapa Songea, maana Suzane akujuwa yupo wapi kwa sasa, akaitafuta namba ya baba yake na kuipiga, bahati nzuri simu aikuita sana ikapokelewa na baba yake, “baba naomba mje hapa kituo cha polisi uwanja wa maji maji, haraka sana nime pata tatizo” aliongea Edgar bila ata salamu, kisha akakata simu, nakumpatia yule polisi ambae alimtazama sana Edgar, ambae sasa alikuwa ndani ya mahabusu akiwa amefungiwa kwenye geti kubwa la nondo, pamoja na watu wengine kama saba hivi
“Mbona hufanani na ualifu we dogo, tena ombea ndugu zako waje kukutoa kabla report aija chukuliwa maana ikisha chukuliwa kesi mahakamani” aliongea yule polisi huku akigeuka na kuondoka zake kuelekea mapokezi, lilipita lisaa limoja Edgar akiwa ndani ya mahabusu bila baba yake kuja pale polisi, atimae likapita lisaa la pili llika kaktika ikawa saa moja usiku, akawasikia wale polisi wakiambizana “nenda kawahesabu wa kiume mimi nawahesabu wakike, ofisa wa zamu karibu anakuja, kuchukuwa riport” aliongea yule polisi wakike, kisha Edgar akamwona yule polisi wakiume akija na kuaanza kuwa hesabu, idadi yao walikuwa nane, “samahani brother, naomba niongee nao tena” aliongea Edgar akimwambia yule polisi, ambae alimtazama kwa sekunde kazaa kama kuna jambo anawaza, kisha akamwambia “subiri kwanza afande aje uchukuwa report, kisha taongea nao” alisema yule polisi na kuondoka zake, Edgar aliona mahakama inamwita, aikipita mda refu akasikia muungurumo wa gari likisimama nje ya kituo cha polisi
“Mungu wangu nime kwisha” aliwaza Edgar huku akisikia mlango wa gari ukifunguliwa na kufungwa ikafwatia salamu za kijeshi, “Jambo afande” kishaakasikia afande alie salimiwa akiitikia, alikuwa mwanamke, aligundua baada ya kusikia sauti yake, kisha akasikia maongezi ya kupewa riport, wakati wanaendelea kupeana riport Edgar alisikia muungurumo wagari linguine liki simama pale kituoni, baada ya dakika chache akasikia sauti za wanawake zikisalimia, “habari zakazi jamani,” ilisalimia sauti moja ya kike, “nzuri wakina dada tuwasaidie nini?” alijibu yule polisi wa kiume huku yule wakike akiendelea kutoa riport kwa afande wao
“Tumepigiwa simu kuwa kuna shemeji yangu yupo hapa amepatwa na matatizo” ilisikika ile sauti ya kike iliyo salimia, anaitwa nani na shemeji yako kivipi” aliuliza yule polisi wakiume akionekana kama anaandika maali, “anaitwa Edgar ni mchumba wa huyu rafiki yangu anaitwa Suzie” hapo moyo wa Edgar ukalipuka kwa shangwe na msisimko wa hajabu, akaachia bonge la tabasamu, “anaitwa nani?” ilisikika sauti ya polisi wkike ambae ni afande wao alie kuwa anapokea polisi, anaitwa Edgar ni huyo wamwisho kuletwa?” alijibu yule polisi wakiume, kikapita kimya kidogo, “Umesema ni mchumba wa nanini?” aliuliza tena yule afande mkubwa wakike, “nimchumbawangu mimi, amekuja jana toka dar, namimi nimekuja leo kwandege,ata sijamwona, ndio baba mkwe ame nipigia simu kuwa yupo...”
NAOMBA SAPOTI, KUNA MATANGAZO(ADS) YANAJITOKEZA KWENYE APP YETU, LIMOJA LINAJAA KWENYE KIOO CHAKO JINGINE LINANG'ANG'ANIA HAPO CHINI KABISA, BONYEZA JAPO MARA 2 AU 3 KILA UKIFUNGUA SIMULIZI HIYO ITANIPA NGUVU YA KUENDELEA ZAIDI NA SIMULIZI ZETU🙏🙏
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA SITINI NA MOJA
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com