MTAA WA TATU (22)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
Dhumuni la barua hii ni kutaka kukwambia ya kwamba mimi siitwi Chanduka kama nilivyo jitamburisha kwako mimi
Ndio Hafidhi j Ikram.
NIOMBE SAPOTI, BONYEZA TANGAZO LINALOKUJA NA KUJAA KWENYE SIMU YAKO WAKATI UKIFUNGUA SIMULIZI AU LILE LINALOKUWA KATIKATI YA SIMULIZI ZETUKABLA HAUJAIFUNGUA NDANI, PIA KUNA LILE LINAKUJA NA KUNG'ANG'ANIA HAPO CHINI, BONYEZA WALAU MARA 3-4 HIVI HIYO NDIO SAPOTI YAKO KWANGU, TAFADHALI NIPE NGUVU NAKUTEGEMEA SANA MSOMAJI WANGU
SASA ENDELEA...
Ninae tafutwa na kwa kosa la mauwaji sijui ilikuwaje mkashindwa kunitambua na jana usiku nimeuwa polisi watano kisha nikatoroka na kuja kutimiza ahadi yangu.
Mapenzi tuliyofanya ilikuwa kama mwisho wa penzi letu.
Ndani ya kiganja changu kuna rist la watu hamsini. Lazima wauwawe
idadi itaongezeka iwapo yeyote
atakaye thubutu kuingilia
Ishu hii.
Zuwena pole sana nafanya yote haya kwa ajili ya kufuta machozi ya
Habiba, ndani ya watu hao
Baba watoto wako nae yumo.
Kama polisi wakifika hapo kunitafuta wape hiyo barua by Hafidhi j Ikram sekunde si nyingi Zuwena akashtuka baada
mlango wa chumba chake kupigwa teke
Polisi wakavamia mikononi wakiwa wamekamata mitutu. Mwenye
Bastora mwenye SMG
na kumuamrisha upo chini ya ulinzi
hakupewa nafasi hata ya kuvaa kitu.
Wakamtoa nnje akiwa kajifunga lile shuka tu,
“Afande Ngogo embu soma hii barua"
mmoja kati ya maafande alimwambia mwenzie na kumkabidhi hiyo
Barua, nae akaipokea akaanza kuisoma kwa sauti kubwa kila mmoja asikie
baada kumaliza kuisoma
polisi wakachoka hoi maana dahaa kumbe mtu wanaemtafuta wamemkamata
kauwa tena mbona balaa
“Mbona hafananii
Hafidhi ni muafrika huyu mbona yupo kama mpemba inakuwaje hapa"..
Afande Ngogo akauliza hivyo.
“itakuwa alivaa sura ya bandia tu"
“sasa kama hivyo kijana atakuja kuuwa watu wengi Aisee cha umuhimu tuweke ulinzi wa kutosha atafutwe kila kona ya nchi hii.
Akipatikana sheria ichukuwe mkondo
wake haijalishi kama ni mtoto
wa general, au bridged
hapa kazi tu twendeni vijana"...
Mkuu wa msafala aliongea hivyo kwa hasira.
“sasa mkuu huyu Mama tumfanye nini?"
Ngogo akauliza huku akimtikisa
Zuwena sijui nia yake shuka ijiachie aone
Mautamu.
“huyo achana nae hausiki kwa
lolote lile"....
Basi polisi wakaondoka zao
Kidevu akamsogelea mama Asia na kumwambia
“nakupa heshima kubwa sana mama yangu
hakika ulikuwa ukiishi na kiumbe hatari sana"...
Zuwena hakutaka kuongea chochote
akaingia zake ndani
kuingia tu akakuta simu yake inaita akaichukuwa haraka kuitizama mpigaji
My love ndio jina alilo msevu
Hafidhi akaipoke huku akiwa na kitete akauliza
“halloo baby uko wapi? polisi wamekuja sasa hivi na mitutu"....
Zuwena akauliza kwa shahuku ya kutaka kufahamu kipenzi chake yuko wapi.
Sauti ya kicheko ikasikika
“ha!ha!ha!ha!"
“khaa baby unacheka unajuwa maskhara ehee ni kweli sikutanii wamekuja,"
“njoo hapa makaburini utanikuta baby"
Kisha simu ikakatwa
Zuwena hakutaka kuchelewa akavaa haraka na kutoka huku akikimbia mbiombio kufika eneo la makaburi
hakuweza kuamini kwa kile
Alichokiona
Aiseee".....
Zuwena hakuweza kuamini macho yakamtoka pima
Baada kukuta miili ya maafande imelaliana hovyo
wakiwa hawana tena uhai
si afande Ngogo wala nani wote wamechinjwa,
Wananchi walijazana na kuanza kuulizana
“hii imekuwaje polisi wote hawa wameuwawa"...
“yani sijui nisemeje
Polisi walikuwa sijui wanatokea wapi,
Sasa wakati wanapita hapa kuna kijana mmoja hivi shalobaro tu akapishana nao
Ghafla bin vuu yule sharo akaanza kutembeza kichapo kwa maafande wale. Mi nilijuwa bongo movie kumbe wanapigana kweli yule sharo alikuwa na visu kama viwili.
Basi akatumia hivyo kuwachinja,
Nikaitoa simu yangu kushort video nikashort,
”embu tuone hiyo video"
Mimi nitumie whatsapp kaka"
Baada jamaa kusema kashort tukio zima kila mmoja akata aone mwingine atumiwe
Jamaa akasema
“ningewatumia tena mngeona tatizo yule sharo kasepa na simu yangu
kudadeki zake kanipiga zinga la mtama, na kuniambia
“lete simu lasivyo nitakuuwa.
Nikaona mmh!
Nisije kuchinjwa bure nikampa mwenyewe"
Zuwena hakuwa na jinsi zaidi ya kuitoa simu yake na kumpigia
Hafidhi majibu yakaja simu ya
mteja unaempigia haipatikani kwa sasa
jalibu tena baadae.
Zuwena akachoka hoi akamuuliza yule kijana aliyekuwa akisimulia tukio zima
“wee kaka umesema huyo
muuwaji kaondoka na simu yako?"
“ndio Dada yangu yani dahaa
simu nimeinunua juzi tu shilling laki
nane jamaa kaibeba"
jamaa akaongea hivyo huku machozi yakianza kumtoka,
“basi usilie nipe number ya simu yako
niweze kumpigia"
Jamaa akataja number za simu
Zuwena akapiga kwa bahati nzuri simu inaita.
Zuwena akaenda mbali kidogo na pale
huku akisikilizia kama simu itapokelewa
ni kweli simu ikapokelewa
na wakati huohuo defender za polisi
kama sita hivi zinaingia polisi
wakaruka kutoka kwenye magari yao
na kulizunguka eneo zima,
Afande mmoja akainama ulipolala mwili wa afande Ngogo na kuokota kitu kama
kikaratasi hivi,
Akakifungua kilikuwa kidogo sana sema kikawa kikubwa baada kukikunjua
“nafahamu fika ni jinsi gani
mtakuwa na simanzi baada kuwauwa panya wenzenu. Naomba mtambuwe kitu kimoja
mwisho wa mchezo huu
mtakuja kupata matokeo. Nyie endeleeni
kukamata vibaka wezi
pigeni watu wenye kufanya maandamano
Msitake kuingia kwenye mkono
wa Mtaa wa tatu mimi ni zaidi ya chatu
nang'ata natafuna nameza.
Yeyote atakae nifatilia lazima auwawe"...
Barua ikaisha hivyo
“Aisee afande Agnes
inaonekana huyu jamaa anajiamini sana mpaka anafikia hatua ya kuitisha serikali"
“ndio maana yake sema muache aneng'eneke (One day) ipo siku moja tutamnasa tu ndio atajuwa kuwa serikali ina mkono mrefu
pumbavu zake"
Afande Agnes akaongea kwa hasira.
Zuwena nae akaisikilizia simu mpaka ikakata.
Na kuamua kupiga tena hatimae ikapokelewa
“Zuwena nini shida? nini tatizo?
Unataka kitu gani kwangu please tulia nyumbani usinipigie simu wala usitake kufahamu wapi nilipo
ukidadisi sana nawe utauwawa!"
Hafidhi aliongea hivyo kwa sauti ya ukali kisha akakata simu,
Habari zikatangazwa kila kona ya nchi
baada muuwaji kufanya
mauwaji mengine tena safari hii ya kutisha
Zaidi kauwa maafande kumi
watano kituoni
watano waliotoka kumtafuta wakakutana nae njiani akawachinja wote
kijana mwenyewe picha yake ni hii.
Ni kijana mdogo sana sema mambo yake ni hatari tupu"
“Toba"...nini hiki (Why)?
mama Hafidhi nini mwanao anafanya, hii ndio kazi aliyopewa na Ankor wake sio?
Niambie mke wangu kwanini mwanetu anauwa kipi kimemsibu?"
Mzee J Ikram aliongea kwa jazba kubwa baada kuona taarifa ya habari kuwa mwanae ameuwa tena polisi kumi.
Mkewe hakujibu kitu akabaki kulia tu
maana Hafidhi ndio mtoto
wa pekee leo hii kageuka kuwa muuwaji
itakuwaje kama akikamatwa hukumu yake ni kunyongwa au kufungwa kifungo cha
Maisha jela.
“hapana siwezi kumuacha mwanangu
ateketee kwa mambo kama haya
lazima nifanye kitu aisee"...
Akaitoa simu yake na kumpigia sijui nani
sauti upande wa pili ikasikika
“halloo mzee shikamoo vipi wazima huko?"
“marhabaa kijana wangu
Dennis kiupande wetu si wazima ila kwa upande wa kijana wako
Mambo si mambo kabisa"
“nani? Hafidhi au"....
Dennis akauliza hivyo,
“ndio ni Hafidhi binafsi amegeuka kuwa gaidi mpaka sasa kauwa polisi kumi na moja.
Dennis nakuomba please naitaji msaada wako uje kumzuia mwanafunzi
Wako asiendelee kufanya ugaidi"
“usijali baba yangu kesho
Nitakuja na vijana kama watatu ni wakali zaidi yake tutamzuia tu,
Ondoa shaka kabisa kila kitu kitakwisha"
“nitashukuru sana kijana wangu
kama kazi ikienda vizuri nitakupa cheo kikubwa sana"
Mzee J Ikram akakata simu
kabla hajaiweka mfukoni simu ikaita
akaipokea
“halloo Assalamu alaykum?
“waaleykum ssalamu
Ewe baba yangu"
Mzee J Ikram akashtuka na kuuliza
“wewe ni Hafidhi? please mwanangu rudi nyumbani uje kuniambia hao watu wamekufanyia kitu gani, tutawakamata kwa mbinu za Kijeshi
kisha wajaze pipa kwa kisoda
au wale embe na kokwa lake,
Hafidhi mwanangu si unazifahamu vyema adhabu zetu ehee
basi njoo nyumbani Baba",,,,
yani aliongea huku kijasho kikimtoka kuonyesha ni jinsi gani anaitaji mwanae
arudi nyumbani.
Anampenda kuliko kitu chochote.
Mkewe akamnyang'anya simu
na kuongea yeye,
“Hafidhi baba uko wapi mwanangu?
Mama yako kila sekunde nalia nashindwa kula wala kulala"
“pole sana mama yangu"
Kisha akakata simu huku wakaishia kusema
halloo,,,,halloo,,,
Simu ishakatwa kibaya zaidi katumia simu ya mezani.
Ndani ya Yombo vituka tunamuona
Hafidhi akiwa anaongea na mama mmoja hivi.
“sawa kijana chumba umepata sema
ndani ya nyumba hii kuna mashart machache tu.
Utakiwi kutumia kilevi cha aina yeyote ile yani kuvuta bange sijui sigara"..
“usijali mama yangu yani hivyo vitu situmii kabisa"
“basi sawa subiri nikuandikie mkataba wako si umesema unahamia leo ehee?
“ndio nahamia leo maana ndio kwanza nimetoka kijijini nisije kulala stendi bure"
“inamaana hapa mjini huna ndugu
kabisa?"
“ndio sina ndugu
Nimekuja mjini kusaka maisha si naweza kupata kazi mama yangu ehee"..
“ndio kazi unaweza kupata ni uwezo wako tu na elimu yako, ehee unaitwa nani?"
Mwanaume akachekecha akili haraka akajibu
“naitwa Eddy Smith"
Basi yule mama akaandika
baadhi ya maneno kwenye karatasi ya mkataba kisha akamkabidhi
na funguo
“hizi ndio funguo za chumba chako
Kuhusu ratiba ya kufagia uwanja au kudeki choo utaenda kusoma pale chooni.
Kila chumba kina number imeandikwa kwenye mkataba"...
“sawa mama yangu nitafanya hivyo"
Hafidhi akaitikia na kuondoka zake,
Mwanaume akakodi pikipiki mpaka Ubungo kisha akaingia kwenye buss ya mwendo kasi
“kusema kweli dunia imekwisha zama zilizotabiriwa kuja ndio hizi yani kuna watu wanajiita manabii sijui mitume
Wakati mtume wa mwisho ameshakufa na hakuna tena mwinginewe mzuri kama yeye"...
Ni mzee mmoja hivi alikuwa akiongea maneno hayo ndani ya buss
“wee mzee embu tunyamazie bwana naona unatupigia kelele tu",,,,
Ndani ya gari ikawa fujo mzee akatoka kwenye kuhubiri dini kaingia kwenye
Siasa
“unajuwa watanzaina walio wengi ni mambumbu inawezekana vipi kutaka kuwapa nchi wachaga,
Kwanza wachaga kwa hela wee wakipewa hii nchi hampati hata shilling kumi
Utasikia mama mia taka hogo"
Kuna kijana mmoja ambae ni mchaga akanyanyuka na kumkunja yule mzee
“wee mzee kama ulitaka kuvunjiwa heshima
Mimi nakuvunjia
heshima kudadeki zako unaleta dharau na makabira ya watu sio?"
Hakika kijana yule aliongea povu likimtoka ikionyesha kachukia kuambiwa wao wachaga wanapenda pesa.
“tafadhali kijana niachie kabla sijaakurukia kichwa ohoo niachie nasema"..
Askari wa usalama aliyoko ndani ya gari hiyo akaja na kutuliza ghasia zile
Askari akamsihi yule kijana kwa kumwambia,
“wewe embu muachie kwanza huyu mzee"
Kijana hakukubari
“nitamuachaje bwana wakati kanitusi"
gari ikafika kituo kimoja ikasimama ikabidi wote wapigwe pingu na kushushwa safari kituoni wataenda kujibu mashitaka yao.
Ndani ya gari kukawa kimyaa mpaka inafika Kariakoo
Hafidhi akashuka na kuanza kukatiza mitaa
sijui kapajuwaje yani kila mtaa kila kichochoro akaingia,
Ndani ya gorofa moja hivi mwanaume akaingia na kupandisha ngazi
ndani ya chumba kimoja kulikuwa na watu wawili wakibishana
mmoja ni mzee wa makamo kwa kukadilia umri wake miaka kama hamsini au stini.
NAOMBA SAPOTI, KUNA MATANGAZO(ADS) YANAJITOKEZA KWENYE APP YETU, LIMOJA LINAJAA KWENYE KIOO CHAKO JINGINE LINANG'ANG'ANIA HAPO CHINI KABISA, BONYEZA JAPO MARA 2 AU 3 KILA UKIFUNGUA SIMULIZI HIYO ITANIPA NGUVU YA KUENDELEA ZAIDI NA SIMULIZI ZETU🙏🙏
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni