SEHEMU YA HAMSINI
Muda si mrefu atakuja kushituka kutoka usingizini hakutaka kuamini kama kile kiumbe kilichopo mbele yake ni Jini si akachukuwa maamuzi ya kumfyatulia risasi yani risasi mfurulizo zikatoka na kwenda kutuwa kifuani kwa Makata ajabu risasi zote zilidunda huku kiumbe kikizidi kumfata.NIOMBE SAPOTI, BONYEZA TANGAZO LINALOKUJA NA KUJAA KWENYE SIMU YAKO WAKATI UKIFUNGUA SIMULIZI AU LILE LINALOKUWA KATIKATI YA SIMULIZI ZETUKABLA HAUJAIFUNGUA NDANI, PIA KUNA LILE LINAKUJA NA KUNG'ANG'ANIA HAPO CHINI, BONYEZA WALAU MARA 3-4 HIVI HIYO NDIO SAPOTI YAKO KWANGU, TAFADHALI NIPE NGUVU NAKUTEGEMEA SANA MSOMAJI WANGU
SASA ENDELEA...
Mariam akarudi nyuma kwa uwoga. Makata kwanza alikuwa na hasira juu ya kifo cha mwanae na kitendo cha bibiye kumtwanga Risasi ilikuwa kama vile kajipalia makaa ya moto ikaonekana kama yeye ndio kahusika na mauwaji ya mwanae. Bibiye akazidi kubofya targert ya kufyatulia risasi na kuishia kusikika katahaa katahaa!!! Hamna kitu, ile Makata anamkaribia bibiye tu na kuandaa mikucha yake sijui kwa nia ya kutaka kumchinja akashtukia akipigwa mateke ya double kick tena lilikuwa pigo moja takatifu mpaka akayumba na kutupwa nnje , Mariam hakuweza kuamini aisee kidume cha shoka amefika hakuwa mwingine ni Hafidhi mi nilijuwa anaenda kule mtaa wa tatu kumbe kaja huku Sinza. Akageuka kumtizama bibiye na kumuuliza “vipi mama watoto umzima?’’ Mariam akaitikia “ndio baby niko salama’’ “ok! Kama umzima ingia chumbani ukalale nisubiri nakuja sasa hivi. Kumbe ilikuwa sebuleni baada bibiye kushtuka kutoka usingizini akatoka mpaka sebuleni na kukutana na Makata kiumbe hatari sana.
Mwanaume baada kumwambia hivyo bibiye akatoka nnje na kumkuta Makata ndio ananyanyuka akajitikisa kichwa kujiweka sawa binafsi ilikuwa kama vile kapigwa na kontena kichwani “Vizuri sana tena sana kwa kuweza kukutana nawe kwa mara nyingine teena,’’ ilikuwa kauli ya Hafidhi akimwambia Makata, Baada Makata akili yake kukaa sawa na kutambuwa kumbe yule aliyoko mbele yake ni Hafidhi, akaanza kucheka hicho kicheko sasa shida tupu, “kha!kha!kha!.. yani alicheka sijui nini kimemchekesha, Hafidhi akatamka kauli moja tu. “Wee nyau nifate’’,,,kisha akachumpa na kupotelea upande wa pili wa ukuta aliweza kufahamu ndani ya eneo hilo kwa mapambano yao patakuwa hapatoshi basi akakimbia huku Makata akimkimbiza na kujikuta wakitokea, kwenye uwanja mkubwa wa mpira ulioko maeneo ya shule ya msingi Sinza, mwanaume akasimama na kuvuta pumzi nzito kwa ndani. Makata nae akasimama na kubaki kutizamana utasema majogoo yanayo tamaniana kupigana, ghafla bini vuu Hafidhi akafutuka na kuwa kiumbe cha ajabu mfano wa Dragon, kwanza Makata mwenyewe richa ya umbo lake la kutisha akaingiwa na hofu juu ya umbo la Hafidhi akajiuliza “huyu kiumbe gani ? mbona kawa mkubwa wa kutisha hivi, wakati akijiuliza hivyo akajikuta anakumbwa kwa kudakwa shingoni kisha akatikiswa na kutupwa kule damu nyeusi zikaanza kumtoka kwa fujo sehemu ya shingo yake hakuchelewa kujiunganisha na kujipanga kwaajili ya kujibu mapigo wakavamiana na kuanza kuzichapa hakika Makata alizidiwa kila Nyanja na kuamuwa kukimbia akapaa juu, akimuacha Hafidhi akimkodolea macho yeye hakuweza kupaa sauti ikamuuliza kama umeweza kuwa Dragoni unashindwaje kupaa embu jaribu kufanya hivyo si akafanya kutest akaenda juu na kuanza kumfatilia mbaya wake, Katika aKili za Makata alijuwa Hafidhi hatoweza kumfatilia wala nini nae akasahau kama aliweza kuwa kiumbe cha ajabu tena mwenye nguvu kushinda yeye wakati akizidi kusonga mbele akahisi kitu kama upepo ukivuma kutokea nyuma yake wala si mbele tena.
Akageuka kutizama hakuweza kuamini baada kuona kumbe jamaa anamfata, tena akija kwa kasi ya kimbunga mwili mzima ukiwaka moto. Ikambidi Makata azidishe speed,
Tukija huku mtaa wa tatu hali haikuwa hali kabisa kumbe bibiye Salma kampigia simu basha wake ambaye ni Kessy baada Mwanaume kufika akaanza kupambana basi akawekwa mtu kati, kikosi kikamzunguka na kuhitaji kumvamia kwa pamoja, sema Kessy akasimama imara na kujibu mapigo, kabla ya kuzidiwa ujanja na kupigwa na kitu kizito kichwani, hakuweza kutegemea na kujishika kichwani akayumba na kudondoka chini akazimia,
“Sasa huyu bwege tukamle kiboga tumnyonye mavi kudadeki zake yani kanitowa jino mimi mamaye zake’’
“oyaa Sheby embu tulia ndugu kutolewa jino ni moja kati ya ajali kazini so kausha,’’
“wee bwege nini yani unataka nikaushe vipi wakati kanitowa jino huyu mwehu nishakuwa pengo kudadeki embu niache nikamle kiboga’’ binafsi Sheby alikuwa na hasira baada kupigwa ngumi ya mdomo mpaka jino lake moja likang’oka. “wee Sheby unataka kufanya nini embu muache huyo mtu nenda kachukuwe maji usukutuwe hizo damu’’ alikuwa kiongozi wao, basi Sheby akafanya kama alivyo ambiwa japokuwa kwa shingo upande, Kesho yake asubuhi na mapema nyumbani kwa bibiye Mariam Wananchi walijazana na kutaka kushuhudia jinsi geti na mlango ulivyo bomolewa kila mmoja akasema nyumba hiyo ilivamiwa na majambazi maana milio ya risasi iliweza kusikika usiku polisi wakachukuwa maelezo na kuondoka watu nao wakaanza kutawanyika,
Kumbe ile jana usiku baada Makata kukimbia akakimbilia kwenye utawala wao, Hafidhi nae akaingia huko huko kikundi cha Majini wakajipanga kutaka kumdhibiti Hafidhi ajabu kiongozi wao akawaambia “msifanye hivyo tambuweni kitu kimoja Makata katumiwa na binadamu kumchokoza huyu kiumbe sasa basi hii kesi ni yakwake peke yake hakuna kuingilia kaeni pembeni tuangalie mpambano ‘’ Unajuwa mpaka hapo Makata akachoka hoi yani kukimbia kote amekuja huku akitegemea kupata msaada matokeo yake kauli inatolewa hiyo kesi yake peke yake aimalize mwenyewe, kitendo bila kuchelewa Hafidhi akachenji umbo na kuwa kiumbe wa kawaida maana aliweza kufahamu katika umbo la Dragon atamuonea sana kidogo Makata akapumua na kuona kidogo afadhali kitu kingine kilicho mvunja moyo Makata kitendo cha kushangiliwa kwa mpinzani wake utasema yupo kwenye himaya yao. Akachukia si kidogo kumbe tayari Makata hakuwa sawa kisaikorojia na kujikuta akipigwa kama mtoto mdogo sekunde si nyingi akachinjwa damu zikaruka huku na kule Majini wakaanza kugombania nyama ya mwenzao kumbe furaha yote hiyo kutaka nyama,
“Ongera sana kijana kwa kuweza kutuondolea huyu chizi maana alikuwa mbishi asietaka kusikia chochote kile,’’ Hafidhi hakutaka kupoteza muda akaondoka zake, Wakati akikata mitaa kurudi nyumbani kwa Vivian akaitowa simu yake na kuitizama akashtuka baada kukuta sms ya Ankor wake ikimwambia
(HAFIDHI KIJANA WANGU NAKUOMBA KITU KIMOJA IWAPO MTU YEYOTE AKIKUPIGIA SIMU NA KUKWAMBIA HALI YETU KUWA TUMETEKWA NAKUOMBA USIJE KWANI HAWA VIUMBE HAWANA ROHO YA HURUMA HAT…) Kabla ajamalizia kusoma akaiweka mfukoni na kutoka mbio, ilikuwa kitendo cha kufumba na kufumbuwa akai kwapuwa moja kati ya pikipiki ambayo mwenyewe ndio alikuwa anaipaki akapigwa kiwiko na kutupwa kule kisha mwanaume akasepa na mchuma wenzake wakaona wee usitutanie yani uibe bodaboda mchana kweupe tena kijiweni wizi wawapi huo. Wakamuungia sema kufika maeneo ya Magomeni pale njia panda akawapiga chenga ya mwili wakabaki kuzubaa na kuulizia wakashindwa kupata jibu kamili, Mwanaume baada kuwatoka wale madereva bodaboda akaingia maeneo ya Tandale akifanya kama kuzunguka hivi aweze kutokea Mtaa wa Tatu,
“Yani inapendeza sana hii kitu yani kwa ubwege wenu mmeshindwa kumpigia simu huyo shujaa wenu sio embu Peter kusanya simu zao zote kisha kazitie chooni,’’ Jamaa akaanza kuzikusanya simu upepo si ukaanza kuvuma ukiona hivyo tu basi kimbia mapema vinginevyo utakuja kufa kizembe SIKU ZOTE UNAAMBIWA DALILI YA VUA MAWINGU SIJUI MANYUNYU SEMA MWANAUME NDIO KATIA TEAM. AKAANZA SIJUI NA Peter au pira kwa kuwa yeye alikuwa akizikusanya simu, akajikuta akipigwa na kiti cha uso baada Hafidhi kukibetuwa na kukipiga teke. Peter akatupwa kule kuja kutahamaki Mwanaume kawekwa mtu kati yani walitaka kufanya kama ilivyotokea kwa Kessy wakumbuke huyo sio Kessy wala fenesi ni Hafidhi a.k.a mzee wa nyapu.
Mwanaume alikuwa akipiga style ambazo hakuna hapa duniani kwanza unaweza kusema ana macho manne wakati yule mwenye gongo akimvizia kwa nyuma ili amtwange nalo, ile anapiga tu Hafidhi kama vile sumaku inavyo kinasa chuma nae akalidaka hilo gongo na kumkita kichwa kimoja tu jamaa akayumba ndani ya Mtaa wa Tatu shukhuri ilikuwa pevu Kessy nae akajiunga kupambana ikawa kata funuwa sijui nyonya mavi wananyonywa wao maana mziki wa hafidhi ni hatari tupu
“Halloo Mzee ndio mwanao amekuja anatuuwa huku’’ ghafla simu ya kijana Yule ikakatika sauti nzito yenye kuambatana na yowe ikasikika kijana akilia, “ohoo shit! Mama Hafidhi mwanao ananiulia vijana wangu wa kazi huko hivi huyu mtoto yukoje kwani?’’ Mzee J Ikram akaongea hivyo akiambatanisha na swali,
“Lakini mume wangu mambo mengine unajitakia mwenyewe,
Unafahamu fika kuwa mwanao hawezi kushikika hata kwa Supergrou leo unawaagiza watoto wawatu wajipeleke kwenye mdomo wa mamba kweli"....
Wakati mtu na mkewe wakiongea simu ya
Mkewe ikaita akipokea na kusikia sauti ya mwanae kipenzi akisema
“Assalam alaykum ewe mama yangu?"
Kabla hujaitikia salamu yangu naomba umwambie kitu kimoja mumeo
Akaweka loudspeaker kabisa haina cha kumwambia asikie mwenyewe
Mwambie namuheshimu kama Baba si vinginevyo tabia ya kunifatilia ipo siku itakuja kumgharimu maisha yake
Sasa mwambie aje kuokota mizoga ya watu wake
Nishachinja wote atajuwa mwenyewe kama atapika mchuzi au atawabanika hiyo mi sijui"...
“Hafidhi mwanangu kwanini unafanya hivyo ujui kama kuuwa ni dhambi kubwa sana.
Hafidhi achana na hayo mambo
Rudi nyumbani
Simu ikakatwa"......
Baada simu kukatwa Mama yake akajaribu kumpigia sema hakuweza kupatikana, akabaki kusikitika tu. Na kujisemea “sijui nimezaa binadamu au Jini maana mtoto gani asietaka kusikia la muadhini wala mkimu swala. “Mume wangu mtoto ndio tushampoteza huyu embu fikilia kizazi chenyewe ni yeye tu, sijui itakuwaje’’ Hakika mama Hafidhi aliongea kwa hisia huku mchozi ukimtoka, “hapana mke wangu usiongee hivyo tambuwa kitu kimoja mwanetu bado yupo hai na haiwezekani kumpoteza kizembe tumuache aifanye kazi ya serikali (One day) atarudi nyumbani,’’ basi wakakumbatiana kwa maneno ya kujipa faraja tu.
Mzee J Ikram hakutaka kupoteza muda si kaambiwa na mwanae aende kuichukuwa mizoga yake basi akajiandaa kwa safari na kuelekea jijini Dar es salaam, “Sasa bosi hapa zinahitajika kokoto kama debe kumi na cement mifuko mitatu kuhusu mchanga ule pale unafaa kingine nondo zenye sentimita nne’’ alikuwa fundi ujenzi akiongea na bibiye Mariam kuhusu matengenezo ya geti ambalo jana yake usiku lilivunjwa na Makata kiumbe cha ajabu. “Sawa nimekuelewa kwahiyo matengenezo yote haya mpaka yakamilike itakuwa shillingi ngapi?’’
“Ni elfu themanini tu’’ Mariam akafunguwa pochi na kutowa kiasi cha pesa na kumkabidhi huku akimwambia
NAOMBA SAPOTI, KUNA MATANGAZO(ADS) YANAJITOKEZA KWENYE APP YETU, LIMOJA LINAJAA KWENYE KIOO CHAKO JINGINE LINANG'ANG'ANIA HAPO CHINI KABISA, BONYEZA JAPO MARA 2 AU 3 KILA UKIFUNGUA SIMULIZI HIYO ITANIPA NGUVU YA KUENDELEA ZAIDI NA SIMULIZI ZETU🙏🙏
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA HAMSINI NA MOJA
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com