TANGA RAHA (16)

0
SEHEMU YA KUMI NA SITA
ILIPOISHIA...
Nikazidi kuongeza mwendo huku akilini wazo la bibi kuwa amefariki dunia likaanza kunitesa,Kabla sijafika karibu na sehemu ilipo nyumba ya bibi nikastuka mtu akinishika mkonno kwa nyuma huku akinivuta kwa nguvu
SASA ENDELEA...
Nikageuka na kukutana na sura yam zee wa makamo akiwa amavalia kanzu nyeupe na bara-kashea huku mkononi mwake akiwa ameshika mkongojo wa kumsiadia katika kutembelea
“Shikamoo mzee”
“Shikamoo yako haina msaada wowote kwangu”

Mzee alizungumza kwa hasira huku akiachia msunyo mkali hadi nikabaki ninamshangaa huku nikijiuliza nilicho mkosea ni nini
“Wewe kijana ni mbaya sana…..Kijana huna adabu shiii nkumi,kijana huna busara.Yaani umeona haitoshi umeamua kutuma majini yako kuja kumdhuru mke wangu”
“Mzee mbona sikuelewe umechanganyikiwa nini?”
“Mimi nimechanganyikiwa.PUMBAVU SANA WEWE”

Mzee akanichapa bakora moja na kunifanya nimponyoke mkononi mwake na kusimama pem-beni nikiwa ninamshanga huku watu wengine walio karibu yetu wakitushangaa kwa tukio alilo lifanyia babu
“Vijana wa siku hizi hamuuna adabu sana unaniambia nimechanganyikiwa mimi?”
“Oya brother Eddy huyo mzee ni kichaa asikupotezee muda wako wewe achana naye”

Alipita jamaa mmoja na kuniambia kuhusiana na huyo mzee ambaye kwenye macho yangu sikuwahi kumuona siku hata moja katika mtaa nilio kuwa nimekaa.

Nikaamini mzee hana akili vizuri baada ya kuanza kumkimbiza kijana aliye niambia kuwa mzee huyo ni kichaa.

Nikajiweka vizuri shati langu na kuanza kupiga hatua kuelekea kwenye nyumba ya bibi iliyo jaa watu nje wenye kanzu nyeupe.

Bibi akaniona na kuja kunifwata na kunikaribisha na kunionyesha stuli isiyo kaliwa na mtunkisha nikaichukua na tukasogea kidogo na kukaa pembeni na walipo watu wenye kanzu nyeupe huku bibi akikaa juu ya gogo la muembe ulio katwa siku nyingi
“Bibihapa kuna nini?”
“Ni maulidi ya mwanangu mmoja wa kike anayafanya kwa mtoto wake alieye zaliwa miezi kad-haa ya nyuma”
“Ahaaa mbona kumetulia sana?”
“Ahha ndio wanamalizia malizia…”
“Inamaana watu tayari wameshamaliza kula ubwabwa?”
“Ubwabwa wamekula tangua amchana hapa wanasubiri kufunga maulidi”
“Bibi bwana mimi nimekuja nina tatizo tena sio dogo nitatizo kubwa kiasi kwamba ninajikuta nimechoka kwenye tatizo lenyewe”

Bibi akaanza kucheka na kwajinsi ya meno yake kuwa pungufu mdomoni mwake na kuweka mapengo makubwa ikanilazimu na mimi kuanza kumcheka
“Eddy mjukuu wangu ile jana ulivyo kuwa unahama unakumbuka nilikupa nini?”
“Ulinipa maji kwenye kichupa?”
“Uliyatumia?”
“Bibi nisikudanganye nilisahau?”
“Hapo ndipo ulipo kosea na yule msichana uliye hama naye ndio aliye kusababishia matatizo hayo”
“Amenisababishia matatizo hayo kivipi?”
“Ngoja nikuambie kitu usicho kijua kuhusu yule msichana”

Nikajiweka vizuri kwanye stuli niliyo ikalia huku nikimtazama bibi kwa umakini
“Yule binti anaitwa Hilda si ndio?”
“Ndio”
“Hilda yule binti amefunga ndoa na jini moja linaitwa Seifh na jini hilo lipo katika kifungo baada ya kukiuka sheria zao za ujini.Na binti yule Alisha zoea kufanya mapenzi na jini ambeye tayari amevishwa pete ya uchumba na mangasuti?”
“Ngoja bibi….Mangasuti ndio nini?”
“Mangasuti ni kitambaa Fulani hivi hutumiwa na watu wenye asili ya India katika swala zima la ndoa”
“Ahaa apo nimekuelewa…Sasa imekuaje kuaje Hilda akafunga ndoa na jinni?”
“Amefunga ndoa na jini bila yeye kujua na ndoa yao siku inafanyika ilifanyikia chini ya baha-ri…..Na baada ya jini aliye muoa kuwekwa kizuizini basi imekuwa ni ngumu kwake yeye kuweza kukaa bila mwanaume kwani hamu zote zilikuwa zinamalizwa na huyo jinni”
“Walipo kuwa wanafanya mapezni alikuwa anamuona jinni huyo?”
“Ndio alikuwa akimjia kwenye njozi kiasi kwamba anajibadilisa badilisha kwenye sura za tofauti tofauti leo anaweza akajiweka sura ya mtu maarufu duniani…..Yaani humjia katika naamna yeye atakavyo”
“Mmmm sasa bibi yule msichana ameniganda kiasi kwamba hataki kutoka nyumbani kwangu”
“Nilazima akugande kwani amepata ladha ya mwanadamu mwenzake tofauti na majini ambao ladha zao ni tofuati sana na mwanadamu na wengi wao ladha zao huwa si nzuri kwa yule anae fanya naye”
Nikajikuta nikichoka baada ya kuyasikia maneno aliyo niambia bibi na kujikuta nikianza kum-pangia mbaya Hilda
“Tuje sasa katika tatizo lako linalo kupelekesha na lisipo tatuliwa mapema litakuondoa duniani”

Moyo ukanipasuka kiasi kwamba nikajikuta nimemtumbulia mimacho bibi hadi mwenyewe akaanza kuogopa
“Babu weeee unanitisha na hiyo mijicho yako…Umesikia kuondoka duniani ndio unashangaa kiasi hicho”
“Bibi acha tu nishangae katika hilo”
“Maana yangu ya kuondoka duniani sio kufa”
“Una maana gani?”
“Unaondoka duniani na kuhamishiwa katika ulimwengu mwengine ambao utaishi kama Mzi-mu?”
“Mzimuuu!!?”
‘Makelele ya nini sasa”
“Ahaaa bibi sasa huko ni kwengine kabisa”
“Ndio ukweli wenyewe siwezi kukuficha kwani maisha yako sasa hivi yapo hatarini”
“Sasa bibi kwanini ni mimi kila siku?”
“Eddy kunakitu sikuwahi kukueleza mwazoni nikijua kwa wakati ule halikuwa na maana sana kuweza kukuambia”
“Jambo gani?”
“Eddy katika watu wenye nyota kubwa duniani wewe ni mmoja wapo.Na nyota yako hiyo in-awindwa na watu wengi ili kuweza kuichukua……Ndio maana unaweza kuona jinsi unavyokubalika katika sehemu nyingi na watu wa kila aina.Wewe unaweza kuona ni kitu cha kawaida ila si hivyo una kitu kinacho kufanya uwe hivyo”
“Sasa bibi kama ni hiyo nyota basi waichukue mimi waniache niishi kwa amani kwani saa hivi kuna mwanamke ananitokea toke asana na kunifanyia vituko vya ajabu kiasi kwamba nijikuta ninachoshwa na mambo yake”
“Tena shukuru Mungu huyo msichana amekutokea kwani ni mwema kwako…..Ila angekutokea yule mwenye mke wake ungekuwa umeshakufa na isitoshe huku alipo anaona kila kitu unacho kifanya na mke wake na anamipango mibaya ya kukuangamiza ndio maana ninakuambia kuwa nyota yako inanguvu sana”
“Sasa bibi mbona unazidi kunichanganya inakuwaje yule mwanamke anaye nitokea ni awe mzuri kwangu wakati yeye sio binadamu?”
“Ni mzuri na ndio mwenye jukumu la kuilinda nyota yako la sivyo utakuwa mzimu kama nilivyo kuammbia”
“Mmmm bibi hakuna hata dawa ya kulamba kidogo nisimuone kwa leo usiku?”
“Eddy mmjukuu wangu dawa ya kulamba wala mimi sina kwani yule sio kiumbe wa kawaidana laiti kama nikimuingilia kwenye mipango yake nilazima na mimi niudhurike”

Nikakaa kimya kwa muda huku wazo la kuondoka likanijia kwani hadi hapa nilipo fikia ninaona bibi anataka kunichanganya kiasi kwamba anataka nianze kuamini vitu visivyo aminika
“Bibi ngoja mimi niende wewe baki salama”
“Sawa mjukuu wangu japo umechelewa ningekuandalia hata kitu cha kula”
“Bibi hapa ni kwangu nitakuja kula siku yoyote”
“Sawa mjukuu wangu”
“Hivi hapa kumeshapata mpangaji?”
“Hapana si umehama jana tu”
“Mmmm haya mwaya bibi ninakutakia siku njema na maulidi mema”
“Na wewe pia mjukuu wangu ninakutakia mapumziko mema na Olvia Hitler”

Nikastuka kusikia jina na Olivia ikanibidi nisimame kwa sekunde kadhaa huku nikimtazama bibi
“Mbona unanishangaa?”
“Nashangaa hilo jina umelijuaje?”
“Kwani ni mangapi ninayo kuambia ambayo huyajui ndio sembuse la huyo Olvia”
“Mmm sawa bibi kigiza hichi kinaingia ngoja nikawahi dalala”
“Sawa mjukuu wangu”

Nikapita nyuma ya watu walio kaa kwenye majamvi huku wote wakinishangaa nikajua ni lab-da nilivyo katiza nyuma yao bila kuwasalimia.

Naikaanza kupiga hatua za haraka huku nikidha-miria kummfukuza Hilda aondoke zake pale tu nitakapo fika nyumbani asije akaniletea matatizo ambayo sikutarajia yaweze kunipata kwa wakati huu.

Kabla sijafika mbali na nyumbani kwa bibi nikasikia ninaitwa kwa nyuma na sauti ambayo ninaifahamu.Nikageuka na kumkuta ni Mama Fety akija kwa hatua za haraka huku tenge lake alilo livaa likimdondoka dondoka huku akijitahidi kulifunga vizuri
“Mambo vipi?”
“Safi tuu Eddy mzima wewe?”
“Mimi mzima “
“Kuna mtu amenifwata na kunitaarifu kuwa wewe umechanganyikiwa?”
“Nimechanganyikiwa na nini…Au ndio umbea wenu munao anza kuzungumza zungumza kwa watu”
“Eddy hasira ya nini jamani wakati nimekuuliza kwa ustaarabu jamani”
“Hakuna cha jamani nyinyi wanawake wa mtaa huu wambea sana”
“Eddy kama nimefanya kosa kukuuliza ninakuomba unisamehe na wala sikuwa na haja ya kutaka kukuudhi ila ulicho kifanya pale msibani kwa watu sio vizuri”
“Msibani wapi?”
“Si pale kwa bibi Mwanavita”
“Bibi Mwanavita mimi mbona simjui?”
“Ni yule bibi aliyekuwa anaishi jirani yako pale si amefarika dunia asubuhi ya kuamkia leo na wewe umekwenda pale wala hukutaka kusalimia na watu waliopo kwenye msiba na mwenyewe ukatafuta sehemu uakajikalisha na kuanza kuzungumza peke yako”

Moyo ukanipasuka nikahisi mwili unaishiwa na nguvu ikanibidi nikae kwenye kibaraza cha pembeni ya nyumba tuliyo simama nje yake huku mapigo ya moyo yakinienda kasi na kwa mbali kajasho kikaanza kunimwagika huku nikijiuliza yule niliye zungumza naye atakuwa ni nani na mbona nimeogea naye ina maana watu wengine hawakumuona.

Maswali yangu yote sikuyapatia majibu ya kuaminika
“Wee unataka kusema yule bibi amefariki?’
“Bibi wa watu amefariki na amezikwa leo saa sita mchana kwenye makaburi ya kwa Minchi sasa nakushanga wewe uanye kwenda pale na kuzungumza peke yako unaonekana kama umetumwa”
Maneno ya Mama Fety yakazidi kunichanganya kwani sikulewa kitu kinacho endelea.
“Ina maana yule niliye zungumza naye sio bibi?”
‘Sasa unamuuliza nani aliye muona huyo unaye zungumza naye?”

Nikakosa kitu cha kuzungumza na kujikuta nikinyanyuka taratibu huku nikijihisi vibaya vibaya nikapiga hatua mbili mbele na kizunguzungu kikali kikanipata na kujikuta nikienda chini kwa kasi ya ajabu na kuanguka kama gunia na giza kali likayatawala macho yangu na sikujua ni nini kinacho enedelea

Nikaja kuzinduka na kumkuta Mama Fety akiwa pembeni yangu amekaa nikakitizama vizuri chumba nilichomo na kugundua nipo hospitali kwani nilijikuta nimetundikiwa dripu la maji kwenye mkono wangu wa kushoto.

Nikakaa kimya huku akili yangu ikinirudisha nyumbani kwa bibi na kuaanza kuyakumbuka maongezi yatu kisha nikayakumbuka maongezi ya mama Fety nikajikua nikipiga kelele na kumfanya mama Fety kutoka kwa haraka uku akiwaita manesi ambaao baada ya muda mfupi wakaingaia ndani ya chumba nilicho kuwepo na kujikuta nikinyamaza kimya na kuwatazama
“Huyu mgonja wako usinge muwahisha hii malaria ingempanda kichwani”

Nesi mmoja alizungumza huku akitoa dawa kwenye kichupa kidogo kwa kutumia sindano yenye bomba kisha akanishika mkono wangu wa huku mwezake akinifunga mpira unao vutika kwenye msuli wangu kisha nesi aliye shika bomba la sindano akanipaka dawa kwenye kiungio cha mkono wangu kisha akanichoma sindano na kuisukuma dawa yote kwa nguvu kisha akaniachia na kusimama pembeni
“Nesi atapona kweli?”
“Ndio atapona wala usijali.Kwani huyu ni nani yako?”
“Mume wangu”
“Usijali mwaya mama ataponana tuu”

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)