SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
ILIPOISHIA...
Siku zikaanza kukatika kama mvua mama naye hakutaka mimi nikae nyumbani tu akanianzisha college chuo cha kujifunza computer lakini kilichozidisha kunishangaza nikuwa tangia siku niliyofanya mapenzi na zureiya sikuona messeji yake wala simu na hata nilipojaribu kumpigia hakupatikana na hata nilipojaribu ya dada yake rukaiya hakuna kilichopatikana.TUPATE BURUDANI KIDOGO KISHA TUENDELEE
SASA ENDELEA...
Wiki kama nne zikakatika na kufikia mwezi kabisa lakini siku moja ijumaa simu yangu ikaita wakati nipo chuoni na nilipoangalia alikuwa si mwingine bali ni zureiya ambaye baada ya kuipokea nikasikia akiongea kama mtu aliyekuwa katika simanzi nzito.‘’jamani zureiya nimekumiss sana mbona mwezi sasa nakupigia haupatikani vipi tatizo nini baby.’’
Nilimwambia rukaiya ambaye baada ya kusema vile akanyamaza kidogo kisha nikasikia mtu akihema kwa kwiki ya kama mtu analia.
‘’mmmh jamani baby un alia nini.??’’
‘’pablo sikia kesho njoo nyumbani mpenzi wangu nilikuwa nalia kuwazuga akina mama na baba kuwa sijisikii vizuri kwenda katika shughuli yao ambayo wanaenda kesho Pablo sasa nimefurahi wamenikubalia kwa hiyo kesho mpenzi njoo nyumbani si unapakumbuka baby.’’
‘’jamani usijali mimi kesho nakuja tufanye na kale kamchezo ketu baby maana siku ile tuliishia njiani.’’
‘’hayaaa honey nakupenda sana.’’
Hakika nikajikuta nikifurahia baada ya kuongea na zureiya ambaye alionekana kuwa hayuko sawa lakini kuongea kwake vile alinipa sababu ambayo hata mimi sikuwa na sababu ya kupinga.Mungu si athumani kesho yake kama Mungu alivyopanga nikamka asubuhi na mapema kisha baada ya kumaliza kazi zangu za kawaida nikamtwangia simu zureiya ambaye alipokea nakuniambia ananisubiri mimi tu na amemiss sana mchezo ule.
Mwanaume nikajiona mjanja nikavaa pamba zangu ambazo nilizivaa siku ya kwanza nilipoenda kukutana na zureiya nguo ambazo huaga zinanionyeshanga mimi kama mtanashati nahandsome wa nguvu.haraka nikachukua gari ambalo kutokana na kuwa ni jumamosi asubuhi kulikuwa hakuna foleni haraka tu nikafika katika jumba kubwa la kifahari ambalo lipo morocco hoteli na kujengwa katika mtaa ambao alikuwa akiishi pia Halima.kwakujificha jificha nikajiweka sawa kisha nikampigia simu zureiya na kumwambia nimefika na haikuchukua hata dakika nyingi mlango ukafunguliwa na macho yangu yakakutana na ya zureiya ambaye alikuwa kama mtu aliyevimba macho kwa kulia.nikajikuta nikisita kuingia baada ya kumuona katika hali ile lakini zureiya akanishika mkono.
‘’Vipii mpenzi unaogopa nini twende honey.’’
‘’mmmh mbona macho yamevimba??’’
‘’hahaha jamani baby si kilio cha jana ili wale waondoke.’’
Maneno ya zureiya yakanilainisha na kujikua nikizama ndani ya jumba hilo la kifahari na kukaribishwa na magari manne ya thamani.
‘’mmmh mbona magari yote yapo au kuna kamchezo lakini haaa hakuna kitu kama hicho.’’nikajikuta nikijisemea kimoyomoyo nakujikuta nikipotezea imani ambazo zilikuwa zinanijia.mwanaume kwa hali ya kujiamini nikazama ndani na kwenda kukaa kwenye kochi kama baba mwenye nyumba vile.lakini nilipojaribu kumuangalia zureiya hakika alionekana kabisa kuwa hakuwa poa kabisa jambo ambalo lilinipana wasiwasi.
‘’P…aa..b.lo jisikie upo nyumbani vp nikuletee juice au maji.’’
‘’baby chochote nitakunywaa.’’nikajikuta nikijibu kwa kujiamini na zureiya akaondoka kwenda kuniletea kinywaji na kuniacha mimi katika sofa kubwa huku kukiwa kuna tv kubwa sana ya flatscreen ambayo ilikuwa ikionyesha picha la kihindi kwa wakati ule.lakini ghafla bila ya kutegemea nikamuona rukaiya akija na kukaa kwenye kochi machozi yakiwa yanamtoka hali iliyosababisha mimi kushangaa na kumuangalia huku mapigo ya moyo yakienda mbio.
Zureiya naye akaja mkononi akiwa ameshika glasi ya juice naye akiwa analia akiongozana na mwanamke wa makamo ambaye alikuwa amefanana naye vilevile ikiashiria alikuwa mama yake.akanisogelea taratibu zureiya nakunipa ile juice ambayo hakunipa mkononi aliniwekea karibu kabisa nilipokaa mimi ambapo kulikuwa kuna meza.
Yule mama naye akakaa kwenye kochi huku akiniangalia kwa chijo kali la hasira hali iliyosababisha nianze kutetemeka kama nasikia baridi.nikiwa katika hali ya mshangao huku macho yangu yakiwaangalia Yule mama,rukaiya na zureiya ghafla jamaa mmoja mrefu akatokea pale sebuleni na nilipomuangalia sura yake nikaikumbuka alikuwa ni Yule jamaa aliyenishika na kunibinya mkono kule palmbeach.
‘’hiyo juice nikwaajili yako Pablo au unataka uletewe damu,’’……………
Ghafla nikasikia sauti nyingine besi ambayo ilisababisha nigeuke sehemu ambayo niliisikia ikitokea macho yangu yakagonga na sura moja ya kizee ya kiarabu ambaye kwa asilimia mia moja alikuwa kafanana sana na zureiya kuliko hata Yule mama aliyekuwa akiniangalia alionekana kabisa ndio alikuwa baba wa familia ile yani baba yake zureiya na rukaiya ambao kwa wakati ule walikuwa kimya huku machozi yakiwa yanawatoka.ghafla baada ya kumuangalia vizuri nikajikuta nikishtuka sana na kuanza kutetemeka huku majasho yakianza kunitoka ghafla kama nilikuwa nimekimbia sana vile kilichosababisha nishtuke sana ni baada ya kuangalia katika mikono ya Yule mzee wa kiarabu ambaye alikuwa mkono wa kulia kashika kisu na mwingine alikuwa ameshika bastola.
‘’Aiseee nimekwisha.’’nikajikuta nikijisemea kimoyomoyo huku mikono nikiweka kichwani kwa masikitiko makubwa majasho yakiendelea kunitiririka kama mvua mwanaume uzalendo ukanishinda nikaanza kudondosha machozi ambayo yalisababisha kilio kizidi kupamba moto kwa zureiya ambaye alikuwa kanipeleka katika mtego ambao nilikuwa nimeshanasa na kutoka hapo ilikuwa si rahisi
‘’hahahahahaha Pablo mbona unalia kijana??’’yule mzee akaongezea huku akijisogeza kabisa karibu na pale nilipo kisha akatafuta sehemu ya kukaa akakaa huku akiniangalia mimi katika kochi ambalo lilikuwa likiangalia na kochi nililokaa mimi.hakika Yule mzee akaanza kuniangalia kwa umakini kuanzia juu mpaka chini kisha akaangua kicheko cha nguvu sana kisha akamuangalia mke wake kwa jicho la hasira sana.
‘’mama zureiya aibu gani hii katika familia yetu na mimi nilikuwa nakuambiaga chunga watoto angalia watoto ona sasa wote hawa watoto wanamimba hivi niambie mwenyewe nikufanye nini.??’’yule mzee akaendelea na kunishtua baada ya kusema zureiya na rukaiya wanamimba jambo lililofanya moyo uzidi kunienda mbio baada ya kusikia kauli ile ambayo moja kwa moja mimi nilishajua kuwa zile mimba zao wote wawili.
‘’lakini baba zuu eeee mimi………’’
‘’kimya wewe pumbafu nimekwambia unijibu nikufanye nini mwanaharamu mkubwa wewe.’’
Ghafla bila ya kutegemea Yule mzee akanyanyuka na kumtandika kibao kikali mama zureiya na rukaiya na kusababisha Yule mama atoe ukulele mkali na hapo hapo damu zikaanza kumtoka mdomoni na kusababisha akina zureiya wapige makelele ya vilio lakini yalinyamazishwa na vibao vikali kutoka kwa Yule baba ambaye alionekana kutokuwa na huruma kabisa muda huo.
‘’haya sasa ninaanza na maswali kwa zureiya nambie hiyo mimba umekupa nani ndio huyu mbwa pablo sio??’’yule mzee akamrukia ghafla zureiya nakuanza kumkaba kwa nguvu nakumuuliza swali la kwamba mimba ile amempa nani.zureiya akaanza kupapalika kwa nguvu nakurusha miguu huko huko huku akitaka kujaribu kujibu lakini alishindwa kutoka na nguvu aliyoitumia kumkaba.
‘’jamani baba zuuu utamuua jamani mwanao muachee!!!’’
Mama zureiya akang’aka na kumsogelea Yule mzee ambaye ndio alikuwa baba yake zureiya na kuanza kuangaika kwa lengo la kumtoa baba zureiya asifike mbali katika kumkaba huko.
‘’paaaaaaaaaaaaaaa’’kibao kikali kikatua usoni mwa Yule mama zureiya na kumrudisha alipotoka kibao ambacho alipigwa na baba yake zureiya ambaye alimuachia zureiya ambaye alikuwa akikohoa kwa nguvu kutokana na kuingiwa na kabali ile.hakika mimi miguu iliisha ganzi nikabaki naangalia tu huku machozi yakiwa yananitiririka sana mikono yangu ilikuwa ipo kichwani sikuwa na la kufanya hakika nilitulia tuli nikiangalia yote na hata wala sikunyanyua hata mkono kufanya lolote nikabaki kimya kama mtu aliyebemendwa.
‘’Hayaaa sasa narudia swali nani aliyekupa mimba hiyo ya mwezi mmoja??’’yule mzee akauliza tena
‘’babaa ni pablooo…’’zureiya akajibu swali lile na kusababisha Yule mzee aangue kicheko tena cha nguvu sana kisha akageuka na kuniangalia mimi kisha katika hali nisiyoitegemea akanikonyeza na kusababisha nishtuke.
‘’safiii kumbe kidume yupo hapa shekheeee nimependa sana kukufahamu Pablo kijana mdogo.’’yule mzee akaniambia na kusababisha na kuzidisha hofu itande nikabaki nakodoa macho nisijue nini cha kufanya.baada ya kujibiwa na zureiya Yule mzee akamgeukia rukaiya aliyekuwa kimya akiwa anatetemeka kama mtu anayesikia baridi kali huku akilia kilio cha kwikwi.
‘’Haya nawe dada mtu una mimba ya mwezi mmoja na wiki nne inakaribia miezi miwili hebu nambie maana familia yangu sasa inachezewa na vidudu ambavyo sasa naanza kukivalia njuga mwenyewe nambie kwanza mwanaharamu gani kwanza kakutia mimba hiii ambayo tukichelewesha itaniletea aibu kubwa kwa sababu nishakula mahali ya mtu na sheria ulitakiwa uwe bikra lakini ukaamua kuruka ruka haya nataka uniambie kwanza ni nani alitekupiga na kukuharibu uso wako uliojariwa na allah[s.w]’’
‘’[kimya]’’hakika rukaiya baada ya kuulizwa vile yeye akakaa kimya nakuzidi kumtia hasira baba yake ambaye alizidi kuwa mwekundu usoni kutokana na hasira kali aliyokuwa nayo huku akimuangalia rukaiya aliyekuwa akiangalia chini.
‘’Rasheed niletee ule mkia wangu wa taa haraka.’’ yule mzee akamtua Yule jamaa aliyenishika mkono kule palmbeach ambaye alikuwa ametulia kimya akiusoma mchezo.baada ya kusikia hivyo haraka akageuka na kuingia sehemu ambayo sikujua alikuwa kaingia wapi.haikupita hata dakika Yule jamaa muarabu aliyeitwa rasheed akatoka huku mkoni akiwa ameshika mkia ule wa taa ambao ulikuwa una mimba na kuja kumkabidhi Yule mzee ambaye hakurembea akamrushia rukaiya na kumchapa mguuni rukaiya ambaye akaachia ukulele mkubwa sana wa maumivu baada ya kupata maumivu makali ya kuchapwa na mkia ule.
‘’nakuambia unijibu mwanaharamu wewe usie kuwa na haya.’’yule mzee akang’aka kwa hasira kisha akajiandaa na kutaka kumpelekea mwingine.
‘’baaaaaa basiii nasemaaaaaa usinichape haya nambie.’’rukaiya akamwambia Yule mzee huku akiwa amenyoosha mikono kuomba msamaha Yule mzee ili asimpige tena
‘’hayaa nambie ni nani aliyekupa mimba hiyo??..’’
‘’iiiiiiiiiiii baaaaa nisameheee ni pabloooooo.’’
Rukaiya akajibu na kusababisha Yule mzee atoe macho na sii yeye peke hata Yule mama naye alitoa macho kwa mshangao zureiya aliyekuwa amelala kwenye kochi huku machozi yakimtoka akanyanyuka haraka na kutoa macho alionekana kuto amini nakubaki akishangaa na kuniangalia mimi ambaye sikuwa na la kuongea niliinamia chini.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
ENJOY WAKATI UKISUBIRI MUENDELEZO, SUBSCRIBE KAMA HAUJAJIUNGA NA CHANNEL YETU
Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho
Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho