BABU G (11)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
ILIPOISHIA...
Humo humo kwenye meseji babu G alinambia siri ya ushindi kwa mwanamke yeyote hasa hao wenye mashauzi na wanaokatisha tamaa ni kujiamini. Kwa mujibu wa babu G “ linapokuja suala la kujiamini hata mwanaume awe mbaya kiasi gani kama anajiamini lazima atakuwa kivutio kwa wasichana wanaokutana nae. Wasichana siku zote wanapenda ulinzi, mtu ambae atakuwa kinga yake sasa ushawai kuona mlinzi hajiamini?.NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
Kujiamini ni ngao kwa sabababu wanaume wanafanana kwa vitu vingi kwa mfano mavazi yao huwa hayawatofautishi sana, kwa hiyo kwenye kundi la wanaume wanaovaa sawa lazima mwanaume anayejiamini ataonekana wa kipekee zaidi. Kujiamini kunamfanya mwanamke ajihisi kuwa salama pindi atakapo kuwa na wewe kwa hiyo wanavutiwa sana na wanaume wanaojiamini tupilia mbali sura na uhandsomboy. Badika ndugu jiamini na kujikubali jinsi ulivyo”.
Maneno haya ya babu G yalinitia hamasa sana na kujikuta sasa nikianza kutafuta mbinu za kuongea na huyu madamu. Niliwaza haraka haraka kuwa kwa kuwa babu G anasema kujiamini ni silaha kwa msichana yoyote basi na mimi nitajiamini kwake na kumlazimisha aongee.
Hivyo nilimau kuonesha hisia zangu kwake.Kwa mila na tamaduni zetu za kiafrika hata mwanamke awe anakupenda vipi ni ngumu kusema kuwa anakupenda. Cha msingi kama umegundua kuwa anakupenda na wewe unampenda ni vizuri ukafunguka kuliko kukaa kimya kwani kukaa kimya kutamfanya aone huna hisia na yeye hivyo kuwa mbali na wewe. Ila kuwa makini sio kwa sababu anavutiwa na wewe basi ukamtongoza tuu ata kama sio chaguo lako hiyo ni dhambi kubwa. Wakati mwingine msichana anaweza kuvutiwa na wewe kwa jinsi ulivyo na confidence, very attractive and sexuality lakini akakuchukulia kama rafiki wa kawaida tu kwa hiyo kwa kuonesha hisia zako kwake utakuwa umevunja mipaka ya urafiki na kuingia kwenye mahusiano..
Haya maneno pia niliyakumbuka sana aliwahi kuniambai babu G.
“Madam” nilijikuta nimeita jina hilo bila kutarajia.
“Yes sir” naye alijibu kisha akaweka pozi.
“Katika maisha yako unapenda kuamini nini hisia zako au uhalisia kwenye maisha”.
“Napenda kuamini uhalisia wa kimaisha huwa siamini sana hisia maana zimeshawahi kunidanganya mara nyingi sana na kuniingiza kwenye matatizo makumbwa. Kwani nini umeniuliza lakini?”. Madamu alijibu swali na kuuliza swali. Sikumshangaa ndo desturi yetu waafrika. Tena kimoyomoyo nilimpongezaa maana hakuuliza swali kabla hajajibu kitu.
“ Kama unaamini kuhusu uhalisia mbona hutaki kuamini kuwa huyu uliyekaa ni mtu wa jinsia tofauti na wewe na pia hutaki kuamini kuwa huyu uliyekaa naye pia ni mtu wa rika lako.
Madamu ilimlazimu kutoa hearphone kwenye masikio yake na kumfanya sasa atege sikio kunisikiliza. Hapa kimoyomoyo nilitamani kujipigia makofi maana nilifanikiwa hatua moja ya kuanza kumshawishi anione mimi ni mtu wa tofauti. Nilianza kumponda kwa njia ya kijanja na kumtolea mifano mingi ya kimaisha ambayo ilikuwa ikimtaka hasijione yeye ni bora sana na hasione kuwa kwa uzuri wake eti basi anaweza kuwa matawi kushinda wengine. Mdam akaanza kujitetea kuwa yeye ni mtu poa na wala nisihisi kama ninavyotaka kuhisi. Nikamwambia inaeleka anaongozwa na hisia kwa maana kitendo changu cha kwenda mbele kimemfanya aone na kujaji kuwa mimi napenda sana wasichana.
Tulionga mengi na nikajikuta sasa madamu anaongea vitu vingi huku nikimchokonoa kwa maneno ambayo yalimfanya aongee zaidi. Sasa utamu wa safari ukaanza kuonekana na kunifanya nisitamani kuhama siti hiyo au kushuka kabisa. Hapo sasa ile simu ilibidi niweke silent na kujifanya namsikiliza kwa umakini sana. Madam akajikuta amenizoea ghafla na kuanza kunaimbia ameshangaa kuna kuwa na upeo mkumbwa sana na pengine nimemuuliza maswali magumu kwa wakati huo. Hiki ndicho nilikuwa nakitafuta kwa muda mrefu. Maana huyu hata staff kule shuleni walikuwa wakimsema kuwa alikuwa akiringa.
Safari iliendelea na hatimaye tulifikka huko tulipokuwa tunaenda. Tulishuka na purukushani za kuoneshwa sehemu za kufikia zilianza. Na zilipokamilika sasa kila mwanafunzi akawa amepata sehemu ya kufikia. Ila sisi yaani mimi na madamu ilitulazimu kwenda kulala nje na shule hiyo. Kwa maana ingine ilitulazimu kwenda kulala kwenye nyumba za kulala wageni. Huko sasa ndipo nilipopanga kupindua matokeo na kujipima kama kweli nilikuwa nimeiva au la. Tuliondoka na madamu huku nikiwa na mpango wa kuhakikisha kuwa nalala na madamu huyo guesti moja kama sio chumba kimoja.Lengo langu lilitimia kwa sababu lodge tuliyoelekezwa tulikuta vimebaki vyumba viwili tu. Kila mtu alichukua chumba chake lakini vilikuwa vinafuatana. Nilipanga kumfanyia vituko usiku huo mpaka atoke chumbani kwake ili aje kulala kwangu.
“Je mipango hii ya Jose itafanikiwa. Nini kitafuata na kutokea kwenye mashindano hayo”.
Wakati mimi najiandaa kumfanyia vituko kumbe na yeye alikuwa na mpango mwingine kabisa ambao mimi sikuujua. Baada ya dakika kadhaa simu yangu iliita. Niliiangalia na kukuta ni madam. Akaniuiliza kama tunalala bila kula siku hiyo. Nilimwambia kama wanafunzi wameshakula basi na sisi tufanye mpango twende tukale. Wote ni wageni lakini kwa sababu tupo wawili bado kuna nafasi kumbwa ya kutoka kwenda kula. Tulikubaliana hivyo na kweli kila mtu alijiandaa na baada ya muda tulitoka. Inaonekana madam alikuwa na ajenda yake ya siri moyoni maana usiku huo alivaa kisichana utadhani labda tulikuwa tunaenda mahali.
“Kuna kiu nimemiss sana na pia leo sipo vizuri je unaweza kunisindikiza?”.
“Kitu gani nilimuuliza kwa haraka haraka”.
“Kiukweli sipo sawa kabisa mchumba wangu ananichanganya sana”. “Anakuchanganya na nini?”
“Usaliti yaani wewe acha tu sijui wanaume mpoje. Kama sasa hivi ameanza uhusiano na rafiki yangu wa karibu”.
“Pole sana ila utahitaji utulivu unielezee kwa urefu huenda labda nitakushauri jambo la kufanya.
“ Yaani acha tu kuna picha nimetumiwa sasa hivi nahisi hata usingizi naweza nisipate.
Ilibidi tutoke nje ya lodge hiyo. Kwa kuwa wote tulikuwa wageni niliamua kumwita dereva tax na kumwambia atupeleke mahali ambapo pana utulivu tunaweza pata chakula kizuri. Dereva tax hakuwa na hiyana alitupeleka mahali ambapo tulipata chakula. Baada ya kula huku madam akionekana kuwa mwenye stress sana alinza kunielezea kwa nini anakosa amani kwa kipindi hicho ambacho kilikuwa ni muhimu sana kwake katika kuelekea harakati za kufunga ndoa yeye na huyo mwanaume ambaye anamsaliti.
Alinieleza kuwa huyo mwanaume anampenda sana na ni mwanaume wa ndoto zake. Anasema huyo alikuwa ni mwanaume wake wa kwanza na ndio aliyemwingiza kwenye ulimwengu huu wa mapenzi. Anasema wamekuwa wakipita kwenye vipindi vigumu vya mapenzi na wakati wote huo wamekuwa wakiachana hata kwa zaidi ya miezi sita na baadaye kurudiana.
Anasema amemjua mwanaume huyo tangu akiwa hana kitu mpaka sasa ni kijana mdogo mwenye mafanikio makumbwa. Kwa hiyo mafanikio yake imekuwa kivutio cha wanawake wengi na kujikuta akiwa anamsaliti mara kwa mara. Ili kuepusha kupotezeana muda alimwambia achague kitu kimoja aende nyumbani kujiambulisha na michakato ya kufunga ndo aianze au waachane. Kwa hiyo huyo mwanaueme akasema hawezi kuachana na mwanamke anayempenda mwanamke anayejua alipotoka.
Kwa hiyo michakato ya harusi ilianza na wakaenda mpaka nyumbani kutambulisha na akavishwa pete ya uchumba. Wamepanga kuwa harusi yao itafanyika mwisho wa mwaka lakni bado mwanaueme huyo hajaacha tabia ya umalaya. Mbaya zaidi anatembea mpaka na marafiki zake wa karibu. Madam alinionesha mpaka picha za hayo anayoyasema. Kwa kweli iliniuma sana kwa sababu nilishindwa kuelewa wanawake ni watu wa namna gani. Yaani rafiki yake ambaye anajuafika kuwa mwenziye amevalishwa pete ya uchumba na atarajiwa kuolewa bado anatembea na shemeji yake.
Ilibidi nimuulize madamu juu ya aina ya urafiki wao. Yaani kwa maneno mengine nini kilikuwa kikiwaunganisha. Akanambia kuwa urafiki wao ni wa chuo. Wamekutana chuo tangu mwaka wakwanza na waliendelea kuwa marafiki mpaka wanamaliza chuo
Shida ni kwamba yeye alipongiwa kazi mbali na jiji hiyo ndo ikawa chachu na fursa ya hayo kutokea. Nilimuuliza baada ya hayo yote kujiri na kujirudiarudia kila mara nini msimamo wake. Madam aliangalia kisha kuniambia kwa sasa hawezi kumuacha huyo mwanaume kwa sababu itakuwa ni aibu kwa familia. Akasema pia amemshirikisha mama yake jambo hilo na mamaye amemwambia kwa wakati huo kuolewa ni jambo la heshima kwa familia hivyo hasiruhusu nafasi ya kuachana itokea bali atafute njia zitakazo mfanya mwanaueme huyo kubadilika. Kwa mujbu wa mama yake ni kwamba hakuna mwanaume huku duniani hasiyekuwa na tamaa na kinachotakiwa kwa mwanamke sio kumuacha mwanaume kwa sababu ya usaliti bali ni kumtengezea mazingira hashindwe kumsaliti.
Niliona pia mama yake alimshauri jambo jema. Nilichomsihi kwa sasa hasijipe presha na zaidi ni bora akawaambai ukweli rafiki zake na kugombana nao kabisa. Nilimwambia hasiwe mpole apambane kutetea kile anachokiamini kuwa ni kitu chake. Basi nilishauri vitu vingi ambavyo kutokana na uwezo wangu niliweza kumshawishi. Akaniuliza swali la kizushi kwa sasa yupo mbali na mchumba wake je na yeye anaruhusiwa kuanza kuandaa plan B kama huyo wakishindwana. Nilimwambia ni sawa ila awe makini hasije akazama kwenye plan B na kuacha pla A. Tulikaa hapo na mara tukaanza kuona watu wanaongezeka huku kwa mbele ikiwekwa stagi na vyombo vya musiki. Kwa akili za haraka haraka nilihisi kuwa kulikuwa na live band siku hiyo.
Muda ulizidi kwenda huku madam akigiza pombe mara baada ya kumaliza maji ambayo alikuwa akinywa kama kishushio cha chakula. Ilibidi aungane na mimi kwa maana mimi nilivyofika tu niliagiza kinywaji nilichokuwa nakipenda yaani sikuvunga wala kumuogopa kuwa ataionaje. Eneo hilo likaanza kuleta raha maana ilikua ikipigwa miziki niliyoipenda. Hata madamu alionekana kufurahi na alipunguza mawazo yake kwa staili hiyo.
Eneo hilo likaanza kuleta raha maana ilikua ikipigwa miziki niliyoipenda. Hata madamu alionekana kufurahi na alipunguza mawazo yake kwa staili hiyo. Madam alikuwa anakunywa pombe kwa fujo sana mpaka nikaingiwa na uwoga. Yaani mimi sijamaliza chupa moja yeye tayari yupo ya pili.
“Jose usinishange nataka niweke kichwa changu sana ili nikienda kulala nilale usingizi mzito kabisa..
“Usiwe na hofu madamu kunywa kadiri uwezavyo kwa sababu ulinzi upo wa kutosha.
Madamu sasa ikawa kama nimemruhusu anioneshe kuwa yeye ni nani. Alikunywa za kutosha na alianza kuchangamka. Akaanza kunilalia lalia mara aninyanyue tuendee tukacheze mziki. Kwa watu ambao walikwa hawatujui ni dhairi kuwa walijua sisis ni wapenzi. Pombe na mziki vikazidi kumchanganya madamu. Wakati huyo yule mwanafunzi ambaye nilichukua namba zake kwenye gari alikuwa akinisumhua sana na kutaka tuoanane usiku huo.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni