MUUZA MAZIWA (6)
JINA: MUUZA MAZIWA Mwandishi: Gift Kipapa SEHEMU YA SITA ILIPOISHIA... Akiwa kitandani hapo alisikia mlio wa mluzi ukisikika kwa mbali karibu kabisa na dirishani sehemu ambapo alikuwa amelala. “it ndizi time!” [ni muda wa ndizi] NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Mwanafunzi mmoja aliongea kwa sauti ya kunon’gona kasha wenzake walicheka kwa sauti za chinichini. Penina hakuelewa chochote kilichoendelea. Mwanafunzi mmoja aliamka na kwenda kufungua mlango. Watu wane wakiwa wamejitanda khanga waliingia ndani, Penina alizani watu hao ni wasichana. Aliduwaa pale walipotoa Khanga zao. Wote walikuwa ni wanaume. Kila mmoja alienda kwenye kitanda chake waliongea lakini sauti zao zilikuwa za kunon’gona. Penina alibaki ameduwaa tu asijue nini cha kufanya , katika chumba hicho ni yeye peke yake ndio alikuwa amelala peke yake. Alijaribu kuutafuta usingizi lakini alishindwa , vilio vya mahaba alivyokuwa akivisikia usiku huo vilimtesa kupita kiasi, alitamani na yeye lakini…