SORRY MADAM (15)

0
SEHEMU YA KUMI NA TANO
ILIPOISHIA...
“Eddy nakuomba unisaidie katika kesi hii wewe ndio kiongozi wangu wewe ndio unaweza kuzizima ndoto zangu katika maisha yangu……..Eddy sikukusudia kukuua na wala sikuwa na lengo baya la kukudhuru yote yalitokea kwa sababu ninakupenda Eddy na sikujua ni jinsi gani ya kukushawishi ili unipende nilidhani utanichezea na kuniacha”

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
Manka alizungumza kwa huzuni huku akilia kwa uchungu akionekana kujutia kwa kitu alicho kifanya
“Sasa Manka kwa nini hukuwa mstaarabu mpaka tushikiane bastola kwa kitu kidogo”
“Eddy nakuomba unisamehe ila nakuomba unisaidie katika hili swala”
“Manka siwezi kukusaidia katika lolote inakubidi na wewe ulipe kwa kitu ulicho nifanyia”
“Kaka muda umekwisha anatakiwa kuingizwa kizimbani”

Askari alizungumaza na kunifanya nianze kupiga hatua za kutoka nje ila Manka akaniwahi na kunishika mkono huku akilia
“Eddy hata nikinyongwa au kuhukumiwa kifungo cha maisha ila tambua kuwa ninazawadi yako nitakayo kupa kama ukumbusho katika maisha yangu”
Nikautoa mkono wake kisha nikaondoka na kwenda katika chumba cha mahakama,Manka akaingizwa na askari huku akiwa analia huku sura yake akiielekeza chini ila mara kwa mara nikiwa ananitazama.Kesi ikaanza kusikilizwa huku mawakili wa pande zote mbili wakianza kumuhoji maswali Manka na kila kitu ambacho Manka alicho kuwa akiulizwa hakujibu zaidi ya kulia.Ikafika zamu yangu ya kuhojiwa maswali na nikaanza kuhojiwa swali moja baada ya jengine

“Mr Eddy ulifwata nini kwa nyumbanni kwa Mwalimu Myange?”
“Nilikwenda kuchukua pesa ya matumizi”
“Ulikuwa una ruhusa ya kwenda kwake?”
“Hapana?”
“Kwahiyo ulitoroka shuleni kwenu?”
“Ndio”
“Basi ninaweza kusema kuwa wewe ni jambazi umwekwenda kuvamia nyumbanni kwa mwalimu mayange ndio maana Manka akakupiga risasi?”

Wakili wa upande wa Manka akaendelea kunibana na maswali yake ambayo ni magumu kupita maelezo nikamtazama Manka kwa jicho la kuiba na kumkuta sura yake akiwa bado ameielekeza chini
“Mimi sio jambazi na Manaka si mtu aliye nipiga risasi”
Miguno ikaanza kusikika ndani ya mahakama nikamtazama mama nikaona jinsi sura yake ilivyo badilika gafla na kuwa na hasira,kutokana na minong’ono hakimu ikamalzimu kugonga nyundo mezani na kuwaomba watu wakae kimya
“Kwa nini unasema kuwa Manka siye aliye kupiga risasi na kwa madai yenu ya washtaki munasema Manka anahusika na wewe kupiga risasi?”

“Narudia kusema Manka hausiki na kitu chochote katika kunipaga risasi wala kunijeruhi mimi.Nilikwenda nyumbani kwa Mwalimu Mayange na kukuta hayupo ila nikamuomba Manka nimsubiri mwalimu hadi atakapo rejea ila kutokana alipata safari ya gafla yeye na mke wake ikanilazimu kuondoka na kupita njia za vichochoroni ndipo nikakutana na majambazi walio waliokuwa wakinilazimisha nitoe pesa ila kutoka na ubishi wangu mmoja wao akanipiga risasi ya kifua na baada ya hapo sikujua ni kitu gani kinacho endelea”

Mahakama nzima watu walikaa kimya huku wakinisikiliza ninavyo zungumza kidogo nikamuona Manka akiwa na tabasumu usoni mwake.
“Kwa hiyo Manka sio mtu aliye kupiga risasi?”
“Wewe vipi kwani hukunisikia nilivyokuwa nikizungumza au?”
Nilizungumza kwa jazba kidogo na umfanya wakili anaye nihoji kuanza kujichekesha chekesha
“Sijasikia labda wewe ndio unaweza ukawa unaidanganya Mahakama tukufu Mr Eddy”
“Sijamdanganya mtu na Manka hajanipiga risasi na muheshimiwa hakimu moja ya sura za majambazi nilio waona mmoja kama ni huyo wakili anaye nihoji maswali yake ya ajabu ajabu”
“Wewe kijana kama umekosa kitu cha kuzungumza sema kuliko kuanza kunipakazia vitu vya kishenzi”
“Kwa hiyo mimi mshenzi si ndio….Hakimu ndivyo jinsi munavyo afundisha hawa mawakili wenu kutukana watu?”

Nilizungumza huku nikiwa makini na kuzidi kumchanganya wakili ambaye nimeamua kumeuzia mastaka
“Muheshimiwa hakimu huyu kijana atakuwa amechanganyikiwa ninaomba mahakama yako akapimwe akili”
“Nani akanipime akili kama si wewe uliye nipiga risasi nna wezako na mbaya zaidi wewe si ulikuja kunichimba mkwara hapo nje kuwa nikikutaja utaniua au sio wewe?”
Hakimu akalazimika kuihairisha kesi na kuomba turudi ukumbini muda wa mchana kwa ajili ya keundelea kwa kesi,Mama hakunisemesha kitu hadi tukatoka nje ya mahakama na kuingia ndani ya gari

“Hivi wewe mtoto ni kitu gani kilicho kupata?”
“Mama hakuna kilicho nipata zaidi ya kwamba Manka hakunipiga risasi ila ni yule wakili na alikuwa na wezake wamelewa”
“Sasa mwangu mbona hayo yoyote hukuyazngumza wakati uatambua fika kwamba Manka ninamchukia kama baba yake?”
“Baba ya ke yupi?”
“Ok tuachane na hiyo mada”
“Mama tena nakumba unaimbie ni kitu gani kinacho endelea kati yako wewe na baba kwani niliwasikia maneno yenu yote kuanzi mwanzo hadi mwisho”
“Unataka kujua ukweli si ndio ni hivi Manka ni mtoto wa baba yako alizaa na mwanamke mwengine kabla hajakutana na mimi”

Nikaanza kuhisi kijasho kikianza kunimwagika huku mwili ukinza kunitetemeka huku nikaanz kufikiria ni jinsi nilivyokuwa nilifanya mapenzi na Manka
“Kwa hiyo nilifanya mapenzi na dada yangu?’
“Unasemaje wewe?”
Nlistuka baada ya mama kuniulizwa swali ambalo nilijikuta nikiopoka bila kutarajia kuwa nitazungumza kitu kama hicho,nikabaki nikimtazama mama huku naye akinitazama kwa macho ya uchungu na hasira

“Hapana mama sijasema kitu chochote”
“Ujasema kitu chochote wakati umezungumza hicho ulicho kizungumza?”
“Mama tupotezee hiyo mada”
“Eddy Eddy wewe lete huo ujinga wako tuu na ole wako nichunguze hilo swala alafu nijue ni kweli oune jinsi itakavyo kama sinto kufunga”

Mama alizungumza kwa hasira huku akishuka ndani ya gari na kuelekea sehemu aliyoingizwa Manka.Sikujua atakwenda kuzungumza nani ikanilazimu nishuke ndani ya gari na kumfwata kwa haraka,nikamkuta mama amesimama na Manka huku akimuonya
“Nisikie siku una uhusiano na mwangangu utanitambua mimi ni nani hapa si anajifanya anakutetea ila ukiingia ndani ya mikono yangu utajuta kuzaliwa”
“Mama mbo……”
“Tena na wewe funga bakuli lako nenda nikukute kwenye gari”
“Lakini mam……”
“Hakuna cha lakini nimekuambia funga bakuli lako na sihitaji uzungumze upumbavu wowote sawa.Angekuua huyo ndio ungefurahi si ndio?”
“Ila mama si nimesha sema Manka hausiki na kitu chochote”

Mama akanitazama kwa jicho la hasira kisha akanisunya na kutoka huku akitembea kwa hatua ndefu kurudi kwenye gari huku mlinzi wake akimfwata kwa nyuma akimtuliza jazba.Wakati wote mama alipokuwa akizungumza Manka alikuwa ameinama chini huku analia kwa uchungu,nikamsogelea taratibu na kumkumbatia japo mikono yake imefungwa pingu kwa mbele.

“Eddy niache tu nikafungwe mama yako amesha tengeneza chuki juu yangu”
“Manka ni maneno gani unayo yazungumza ehee sipo tayari iwe kama hivyo nahitaji utilize akili katika hili nakuomba tena sana mmmm”
“Eddy hata nikiwa huru sinto weza kuwa na uhuru kama mwazonni….Laiti baba yangu angekuwapo nisinge nyanyasika kiasi hichi”
“Kwani baba yako nyupo wapi?”
“Ni historia ndefu Eddy ila kwa ufupi baba yangu ana uwezo mkubwa wa kiuchumi ila alimtelekeza mama baada ya kunizaa mimi……….ila sijui ni wapi alipo japo ninasikia sikia amependishwa cheo kazini kwake”
“Ulisha wahi kukutana naye hizi siku za karibuni?”
“Hapana mara ya mwisho kukutana naye nilikuwa na umri wa miaka mitano kuanzia hapo nina msikia sikia”

Nikajikuta ninapata maumivu mengi moyoni mwangu huku mawazo ya kwa nini baba anafanya hivi yakitawala kichwani mwangu.
“Eddy mama yako anacho kizungumza ni kweli nakuomba uniache nikafie jele”
“Manka acha kuzungumza kitu kama hicho ila tambua kuwa nipo upande wako hadi dakika ya mwisho”
Nilizungumza na kuondoka na kumuacha Manka akibaki ananishangaa.Muda wa kuingia mahakamani ukawa tayari umesha wadia sikuhona haja ya kumsubiria mama kuingia naye kwenye ukumbi wa mahakama nikatangulia mwenyewe na kumkuta mwalimu Mayange na familia yake wakiwa wamekaa kwa masikitiko

“Eddy”
Mwalimu Mayange liniita na nikamfwata katika sehemu waliyo kaa
“Eddy mwanangu nakushukuru kwa masaada wako japo tunasubiria majibu ya mahakama”
“Usijali mwalimu Mungu atasaidia yatakwisha”
“Kumbe mama yako ni waziri?”
“Ndio”
“Hongera”
“Asante”

Nikaondoka na kwenda kukaa katika eneo nililo kuwa nimekaa mwazoni na baada ya muda kesi ikaanza,kutokana muhusika mkuu nilikataa Manka kuwa sio muhusika ikalazimika kesi kufutwa na Manka kuachiwa huru.Upande wa familia ya Manka ikatawaliwa na furaha ila kwa upande wangu mama amekasirika
“Kwenye gari langu hupandi na utakuja kwa miguu”
“Mama….
“Hakuna cha mama Zuhura hembu mpe alfu ya daladala”
“Sawa bosi”

Mlizi wa mama akafungua kipochi chake na kunipa alfu moja ya daladala kisha wao wakaingia ndani ya gari na wakaondoka nikabaki nimesimama ninawashangaa kwani sikuamini kama mama anaweza kunifanyia kitu kama hicho.Nikiwa bado sijui cha kufanya nikasikia sauti ya Manka ikiniita kwa nyuma nikageuka na kumkuta amesimama huku akiwa na tafbasabu usoni mwake
“Eddy nashukurukwa msaada wako yaani sijui hata nikushukuruje”
“Usijali best yangu”
“Ila Eddy nina zawadi yako kama nilivyo kuambia pale mwazoni”
‘Una zawadi gani?”
“Nina ujauzito wako”

Kusema kweli mapigo ya moyo nikahisi yamepoteza muelekeo na kunifanya mwili mzima kuanza kuzizima kiasi kwamba jasho likaanza kunimwagika huku mdomo ukiwa mzito kuzungumza kitu ninacho taka kukizungumza hadi Manka akahisi kitu
“Eddy una tatizo?’
“Hapan…..munarudi Arusha leo?”
“Ndio ninamsubiria shemeji aje kutuchukua amelipeleka gari gereji”
“Ahaa basi Mungu akibariki hilo swala la mtoto tutakuja kulizungumza huko Arusha”
“Lakini mbona unaonekana kama huna furaha nilivyo kuabia kuwa mimi ni mjamzito?”
“Haaa nimefurahi ila tutatafuta muda tulizungumze”

Tukaagana na Manka kisha mimi nikaondoka na kumuacha akazungumza na ndugu zake kisha,Nikakodi boda boda ya pikipiki hadi nyumbani nikamuacha jamaa getininikingia chumbani kwangu kumchukulia pesa ambayo ilipungua kwenye malipo yake kisha nikarudi ndani na kumkuta mama sebleni akionekana akinisubiri.Nikaanza kupandisha ngazi za kwenda ndani kwangu

“Wewe Eddy”
“Naam”
“Hembu shuka hapa”
Nikashuka na kukaa kwenye moja ya sofa kisha na yeye akakaa kwenye sofa jengine
“Hembu wewe mtoto niambie ni nani aliye kupiga risasi?’
“Mama kile nilicho kizungumza mahakamani ndio hicho hicho”
“Ila Eddy manangu kwanini siku ya kwanza nilivyo kuuliza ukasema Manka ndio muhusika?”
“Hapana labda nilikosea”

“Kukosea tena mwanangu…..Ila na kwanini ulisema umetembea na Manka?”
“Ahaaa mama ulinisikia vibaya”
“Eddy Eddy mwanangu jua kuwa mimi ni mtu mzima na kila unacho pitia,mimi pia nilisha pitia kipindi ninakua sasa usitake kunidanganya hembu niambie ukweli mwanangu ni kweli Manka ulitembea naye?”
“Sijatembea naye wewe si umesema ni dada yangu?”

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)