SORRY MADAM (16)

0
SEHEMU YA KUMI NA SITA
ILIPOISHIA...
“Eddy Eddy mwanangu jua kuwa mimi ni mtu mzima na kila unacho pitia,mimi pia nilisha pitia kipindi ninakua sasa usitake kunidanganya hembu niambie ukweli mwanangu ni kweli Manka ulitembea naye?”
“Sijatembea naye wewe si umesema ni dada yangu?”

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
“Ndio ni ndugu yako……Kachukue begi lako la nguo dereva akupeleke shule”
Mama jioni yote hii derive anipeleke shule?”
“Maamuzi ndio hayo kavae ngui zako za sule derive akupeleke Arusha”
“Lakini mama sijapona vizuri”
“Hujapona vizuri au unataka kujidekeza dekaza kumbuka kuwa wewe ni A level tena mwenyewe unajiita PCB sasa sijui huko shule kama unasoma au ndio kuruka ruka vaa upelekwe shule”

Kitendo cha mama kuniambia nijiandae nirudi shule kikanikosesha amani katika moyo wangu na sikuwa na jinsi zaidi ya kujiandaa na taratibu ili dereva anirudishe.Hadi namaliza kujiandaa ikawa imeshatimu saa kumi na moja jioni.Nikabeba begi langu la nguo na kulipakiza ndani ya gari
“Eddy nataka huko shule ukasome sihitaji michezo ya kijinga jinga tambua kuwa wewe umesha kuwa mtu mzima unapaswa kuaanza kufikiria maisha yako na yawanao ila sio kufanya ujinga kama ulio ufanya”
“Sawa mama”
“Kama mutakuwa munachelewa mutalala kwenye Hotel yoyote njiani”
“Sawa”

Mama akanipa kiasi cha kutosha cha matumizi ya pesa ya kutumia shukeni pamoja na pesa ya matumizi njiani na safari ikaanza,kutokana na foleni iliyopo jijini Dar es salaam ikatifanya tusimame simame san njiani
“Kaka naomba niendeshe niendeshe gari”
“Ningekupa mdogo wangu ila huna leseni”
“Kwani usiku huu ni trafki gai atakaye tusimamisha njiani?”
“Mbona wapo wengi hii ni bara bara ya mkoani ni lazima tutawakuta wengi”
“Sawa”

Safari ikaendelea huku nikiwa nimelala kwenye siti ya gari na kumuacha dereva kufanya kazi yake.Dereva akaniamsha na nikakuta tumesha fika katika sehemu moja inaitwa Mombo kwenye hoteli moja inaitwa Liverpool,tukaingia na kuapata chakula cha usiku na tukarudi dani ya gari na safari ikaanza.Kutokana sikuwa na mazoea na huyu dereva mpya wa mama nikaona ni bora kulala kwani sikuwa na chakuzungunza naye.Nikastushwa na breki kali za gari letu na kunifanya nistuke na nikamkuta dereva akijitahidi kuikwepa gari ndogo aina ya PREMORE inayo pinduka pinduka katikati ya barabara.Gari inayo bingiria ikatulia na kuingia ndani yam taro ikamlazimu dereva kulisimamisha gari letu mbele kidogo kutoka sehemu gari ndogo ilipo angukia.Mimi na dereva tukajikuta tumetulia kama kwa dakika tano huku kwa upande wangu mapigo ya moyo yakinienda mbio kiasi kwamba nikashindwa nifanyaje

“Kaka imekuwaje?”
“Mmmmmm?”
“Imekuwaje?”
“Nilikuwa ninamuomba dereva wa lile gari anipishe njiani ila akawa anashindana na mimi katika kukimbiza gari…..ila kutokana na taa za gari zangu kuwa uwezo mkubwa basi nikajikuta ninamuwashia zote ndio jamaa akaanza kijuchanganya changanya hadi akadondoka”
“Mmmmm huu msala tusepe zetu basi”
“Mmmm siwezi hata kuendesha gari”
“Ngoja mimi nije kuendesha”

Nikashuka ndani ya gari nikiwa ninazunguka nyuma kwenye gari ili niiingie kwenye siti ya dereva nikapata mstuko baada ya kumuona msichana akianza kujivuta taratibu kutoka ndani ya gari huku akilia kwa maumivu makali ikanibidi nianze kupiga hatua za kwenda kumsaidia ila kadri jinsi nilivyo zidi kwenda moyo ukazidi kunipasuka kwani mtu anaye jitahidi kujitoa ndani ya gari ni Manka

Nikaongeza hatua za haraka kwenda kumsaidia Manka,nikamkuta anatokwa na damu nyingi katika paji la uso wake huku mguu wake mmoja ukiwa umebanwa katika siti,Nikajitahidi kuitoa siti iliyombana Manka hadi nikafanikiwa kisha nikamuweka kando kwenye barabara na kwenda kutazama majeruhi wengine akiwemo Mwalimu Mayange.Nikachungulia chungulia ndani ya gari na ila sikuona mtu yoyote anaye omba msaada kwani ukimya mkubwa ulitawala ndani ya gari na kutokana na giza jingi nikajua moja kwa moja watu waliomo ndani ya gari watakuwa wamefarika dunia ua kupoteza fahamu.

Nikarudi barabarani kumtazama Manka na kukuta hali yake inazidi kuwa mbaya nikamnyanyua na kwenda naye ndani ya gari na kumkuta dereva akiwa amekaa kwenye siti niliyokuwa nimekaa mimi huki akiwa kama amepigwa na bumbuazi kiasi kwamba hawezi kufanya kitu chochote huku jasho jingi likimtoka japo ndani ya gari letu aina ya VX G8 lina Air condition(A.C) ya kutosha.Nikamuingiza Manka ndani ya gari na kumuweka siti ya nyuma kisha na mimi nikaingia kwenye upande wa dereva na kuwasha gari na kuondoka kwa mwendo wa kasi,nikafika kwenye moja ya zahanati na kumkuta daktari mmoja na nesi ambao wapo zamu ya usiku

Nikamtoa Manka ndani ya gari na kumuweka kwenye kitanda cha matairi kilicho tolewa na nesi kisha wakamuingiza ndani ya chumba na kuniomba nisubiri nje na kunihitaji nikatafute PF3 ya polisi ili hata kama kuna hali yoyote itajitokeza juu ya Manka wao wasihusike kwa chochote.Nikarudi kwenye gari na kumkuta dereva nje ya gari akiwa amejiegemeza kwa unyonge huku akionekana kuwa na wasi wasi mwingi

“Oya kuna kituo cha polisi hapa karibu”
Nilimuuliza dereva na kumuacha akiwa ananitazama kama hajalisikia swali langu nililo muuliza
“Oya broo mbona kama umesizi ni wapi kwenye kituo cha polisi ambacho ninaweza kupata huduma yao?”
“Hapo mbele”
“Wapi?”
“Labda Mombo kule nyuma tulipo toka kwani bado tupo Mombo”
“Powa ingia kwenye gari”

Nikawasha gari na kuanza safari ya kurudi kule tulipotoka na safari hii gari nillizidi kuliendesha kwa kasi ili kuwahi kupata alicho niagiza daktari.Nikajikuta nikifunga breki za gari gafla na kusimama hii ni baada ya trafki mmoja kunisimamisha katika sehemu waliyo pata ajali Manka na ndugu zake na kukuta kuna askari wengine wakiendelea na vipimo vya ajali imetokea tokea vipi huku kukiwa na watu watatu wakiwa wamelazwa kando ya barabara na huku wakiwa wamefunikwa na mashuka maalumu ya polisi na baadhi ya wananchi wakiwa wanashangaa shangaa ajali

“Dreva washa taa ya ndani au ushuke ndani ya gari”
Nikawasha taa ya gari na nikamuona trafki akistuka nikajichunguza na kugundua kuwa chati langu la shule kidogo lina damu.Trafki aliye nisimamisha akaniomba tena nishuke ndani ya gari huku bunduki yake akiishika vizuri na sikuwa mbishi nikashuka huku funguo nikiingiza mfukoni
“Ninaomba leseni yako na kadi ya gari”
Nikaanza kujipapasa kama ninatifafuta leseni yangu kwenye mifuko yangu japo najua kuwa sina leseni ya aina yoyote kwenye mfuko wangu zaidi ya wallet yangu yenye kitambulisho cha shule na pesa za matumizi

“Afande nahisi nimeishahau leseni yangu kwenye gari”
“Mbona shati lako limejaa mijidamu.Lete funguo za gari”
Nikamkabidhi trafki funguo za gari na kwaishara akaniomba niende kumchukulia leseni yangu na kumuacha akimnong’oneza mwenzake.Nikafungua mlango wa gari na kumkuta dereva akiwa na wasiwasi mwingi
“Oya kaka hivi una leseni yoyote hapo ulipo?”
“Ninayo ya kwangu”
“Siwezi kutumia ya kwako?”
“Huwezi kwani ina picha yangu”

Nikaufunga mlango na kumfwata trafki aliye nisimamisha na kila nilipozidi kumfwata huku nikimuita akajifanya kama hanisikii na kuzidi kwenda mbele kuwafwata wezake walipo huku mwenzake aliyekuwa akizungumza naye akielekea kwenye gari letu huku akimulika mulika ndani ya gari kwa kutumia tochi aliyo nayo.Nikamkimbilia trafki kidogo na kumshika shati
“Afande si nina kuita”
“Nahitaji leseni yako na kadi ya gari”
“Kiukweli mimi sina leseni ya aina yoyote hapa nilipo nilikuwa ninakuja kituoni kwenu kuchukua PF3 ya majerugi wa hiyo ajali hapo”
“Ahaaa kumbe nyinyi ndio muli wasababishia ajali hawa watu?”
“Hembu kuwa na akili wewe mimi nimsababishie ajali alafu nije kwenu.Mimi nimewasaidia kama masamaria mwema tu”

Nikajikuta nikizungumza kwa hasira huku nikimtazama trafki kwa jicho la hasira.Kabla hajazungumza kuna mwenzake mmoja akamuita akitokea lilipo gari letu huku akimuamrisha dereva wa gari letu kushuka ndani ya gari
“Oya afande John haya ni mijambazi huku kwenye gari lao kumetapakaa mijidamu siti za nyuma na hakuna mtu”
Askari aliyekuwa kwenye gari letu alizungumza na kuwafanya wezake wapatao sita kuzikoki bunduki zao na kuzielekeza upande nilio kuwepo mimi na dereva
“Wee jamaa yangu vipi hivi ukituona hapa kuna sura ya jambazi.Mimi nimemsaidia huyu mmoja wa majeruhi katika hii ajali na wewe unaniletea habari za kise***”

Nilizidi kuzungumza kwa hasira na kuwafanya askari kunijia juu huku kila mmoja akizungumza lake kwa hasira huku mmoja wao akitishia kunipiga mateke
“Jaribu kunipiga hayo mateke yako uone kama hii nchi utaiona tamu kama unavyo iona sasa hivi”
“Afande hembu niachie nimuonyeshe shuguli huyu kijana tandu nitoke depo nijamuwasha mtu mateke siku nyingi”
“Aroo hembu lipige pingu hilo jambazi linajifanya jeuri.Na haya ndio yale yanayoiba magaria Moshi na kwenda kuyauza Dar”

Dereva wetu akakubali kufungwa pingu na akaanza kupelekwa kwenye gari ya polisi aina ya Toyota.
“Aisee wewe nimekuambia lifunge pingu hilo likijana lisiumize vichwa vyetu”
“Sikilizeni hamuwezi kunifunga pasipo kujua kosa langu ni lipi kwani hamuwezi kukuta damu ndani ya gari na moja kwa moja mukaniambia kuwa mimi ni muhalifua”
“Aisee wewe lipige risasi kama linaleta ujinga”

Nikaitoa simu yangu mfukoni na kumpigia mama ila simu yake ikaita hadi ikakatika,nikarudia tena kuipiga na akapokea simu huku akionekana alikuwa amelala
“Vipi wewe mbona muda huu mumesha fika?”
“Hapana mama kuna askari wametukamata eti wanasema kuwa sisi ni majambazi”
“Majambazi tangu lini na mumekamatwa wapi?”
“Maeneo ya Mombo njia ya kuelekea Arusha…..”
Gafla askari mmoja akanipokonya simu na kuanza kuzungumza na mama huku akionekana kuw na hasira nyingi

“Kumbe wewe ndio unaye watuma hawa washenzi wako waje wateke teke magari ya kifaharii na munakazi ya kujikalia na kuitana mama mama pumbavu weee mwanamke mzima umekalia kazi ya kuwatumikisha vijana wadogo ili wakuletee mijigari ya kifahari na hili limoja umelivalisha minguo ya shule ili idanganyie raia barabarani wakati wa usiku Malaya mkubwa wee”

Askari akakata simu na kuidumbukiza mfukoni mwake na kuzidi kunipandisha hasira kwani katika maisha yangu kitu nisicho kipenda ni kuzalilishwa kwa mama yangu
“Aisee hatukubembelezi wewe”
“Sasa niacheni nitakwenda mimi mwenyewe sitaki munishike”
“Pumbavu hakuna kuliachia ndio maana jishati lako limejaa damu kwa ujambazi ujambazi wako”
“Mabroo nawaheshimu sana sitaki tuvunjiane heshima”
“Nenda kule”

Askari mmoja alizungumza huku akinipiga makofi mazito ya mgongo akinisukumia kwenye gari lao na kuninyanyua juju na kunisukumia ndani ya gari na kujikuta nikiangukia kifua na maumivu makali yakaanza kutawala katika kifua changu

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)