SORRY MADAM (17)

0
SEHEMU YA KUMI NA SABA
ILIPOISHIA...
Askari mmoja alizungumza huku akinipiga makofi mazito ya mgongo akinisukumia kwenye gari lao na kuninyanyua juju na kunisukumia ndani ya gari na kujikuta nikiangukia kifua na maumivu makali yakaanza kutawala katika kifua changu

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
Dereva akanisaidia kuninyanyua na kunikalisha katika sehemu aliyo kaa yeye kisha baada ya muda wakaziingiza maiti moja huku ikiwa imefunikwa na askari wawili wakapanda na kukaa nyuma tulipo sisi huku wakiwa na bunduki zao kusha mwengine wawili wakapanda mbele upande wa dereva na safari ikaanza

“Yaani nyinyi ngojeni tu mutaona ngoja mama aje”
“Funga bakuli lako shenzi kabisa wewe na mama yako wote tutawasweka ndani munakazi ya kukaa na kuiba iba”
“Sawa sisi si majambazi basi nyinyi ndio mutakuwa majambawazii”
“Unasemaje dogo”
“Nasema kwa pua mdomo unatia saini”

Nilizungumza maneno ya kejeli yaliyo andamana na hasira kumfanya askari kukasirika nusu anizabe kofi la kichwa
“Mimi nawaambia masaa yenu ya kujidai ni sasa hivi ila ngoja hiyo asubuhi”
“Alafu wewe dogo mbona unaongea ongea kama mtoto wa kike unajua tutakupeleka Soweto ukafanyiziwe”
“Mpeleke baba yako wewe k*** nini?”

Nilizungumza kwa hasira na kumfanya askari kumkabidhi mwenzake bunduki kisha akanishika shati langu na kunivuta kisha akanipiga kichwa kimoja kaniangusha na kujikuta nimeilalia maiti ambayo sikujua ni ya nani kisha akaninyanyua na kunitandika ngumi mbili za tumbo na kujikuta nikitoa vilio vya maumivu makali

“Oya bro Sele muache utamuua mtu mwenyewe anaonekana mwili maji huyo”
“Muache nimfundishe adamu analeta maswala ya kiboya,watu tupo kazini hatupo kwenye sherehe”
“Kaka tuliza jazba mpotezee ngoja tufike kituoni”
“Oya Suka hawa moja kwa moja tuwapandishe Lushoto”
“Powa kamanda OVER”
“Eddy mdogo wangu hembu kuwa mstamilivu”

Dereva alizungumza kwa sauti ya upole huku akinitazama kwa masikitiko kwani nilianza kuchuruzika damu kwenye sehemu aliyo nipiga kichwa askari.
“Powa wewe nionee sasa hivi ila zamu yako itafika”
“John unajua nitamchakaza huyu mwehu kwa risasi alafu nipotelee zangu huko milimani”
“Broo wewe mpotezee”
“Oya suka simamisha gari”

Askari aliye nipiga alimuamrisha askari mwenzake anaye enedesha gari kulisimamisha naye akafanya kama alivyo ambiwa.Kisha akashuka na kwenda kukaa siti ya mbele na mwenzake mmoja akaja kukaa tulipo sisi.Kutokana ni usiku hakuna magari mengi tukawahi kufika wilaya ya Lushoto mjini na moja kwa moja wakatupeleka kwenye ofisi zao
“Msachi huyo chalii na atoe kila kitu”

Yule askari aliye nipiga alimuamrisha askari mmoja tuliye mkuta katika kituo chao.Jamaa akaanza kunipapasa na kutoa waleti yangu kisha akaiweka pembeni kisha yule askari niliye mkremisha kwa jina la Sele akaichukua wallet yangu na kuanza kuhesabu pesa nilizo kuwa nazo na kukuta kuna laki mbili na sabini
“Kweli hi mijamaa ni mijambazi tazama pesa zote hizi”
Alizungumza huku akiwaonyesha wezake waliopo ndani ya kituo hicho ambacho ndio kikubwa katika wilaya nzima ya Lushoto
“Wewe jishaue na hizo pesa zangu najua humo kuna laki mbili na sabini ole wako nikute kumepungua hata kumi”
“Alafu huyu dogo ananitafuta tangu tukiwa kwenye gari hivi unataka nikufanyaje?”
“Usijichekeshe chekeshe kama umepata bwana wa bure acha hizo pesa na ole wako ipungue hata kumi”

Nilizungumza kwa hasira na kuwafanya baadhi ya askari kumcheka mweznao kichini chini kwa maneno niliyo muambia ila alivyo wageukia wezake wote wakakaa kimya.Jamaa akampokonya mwenzake kifimbo alicho kishika na kutishia kunipiga nikasimama nikimtazama huku mwili wangu ukiwa umejaa kwa hasira
“Hembu waingize chemba nisije nikavunja sheria za Jamuhuri bure”

Nikageuka na kumtazama dereva nikamuona mwenzangu akitetemeka mwili mzima huku machozi yakimwagika kisi kwamba hadi nikaanza kumuonea huruma.
“Oya broo simu yako iko wapi?”
“Nimeiacha kwenye gari niliichomeka kwenye chaji”
“Ahhaaa sasa kwa nini na wewe usishuke nayo”
“Niliisahau ndugu”
“Ahaa na wewe umezidi uzembe”

Askari aliye kuwa akitukagua akatusukuma akiashiria tutembee kuingia ndani ya chumba chenye mwanga hafifu wa taa ya duara kwa haraka haraka ni kama Walti 40 huku kikiwa na nondo ndefu na pana kwenye mlango wake kiasi kwamba sio rahisi kwa mtu kuuvunja mlango huo
“Ingieni ndani hizo story zenu mutazizungumzia humo ndani”
“Na wewe acha sifa za kutusukuma sukuma unajua hili shati limenunuliwa shilingi ngapi?”
“Sina haja ya kujua limenunuliwa shilingi ngapi cha msingi wewe ingia huko chemba ukakutane na vigego wezako”
“Sawa ila sio kutusukuma sukuma uachage ufala wewe”
“Powaa mimi fala ila ingia ndani”

Sikujua hata maneno machafu nina yatolea wapi kwani nilizungumza maneno yasiyo na maana na kwa mtazamo wa haraka haraka mtu ukinitazama huto tegemea kuwa ninaweza kuzungumza vitu vya ajabu kiasi hicho.Tukaingia ndani ya chumba na kukuta kuna njemba(Jamaa wenye misuli mikubwa) nne zimakaa huku wakiwa hawajavalia mashati na kuvifanya vifua vyao vikubwa kuonekana kirahisi huku sura zao zikiwa mbaya na za kuogopesha kiasi kwamba mtu hata uwe mbabe kiasi gani ni lazima uyasome mazingira ya humo ndani na ndio uendelee na ubabe wako
“Niaje raia?”

Niliwasalimia kwa ucheshi huku nikijitahidi kuiweka sura yangu katika tabasamu ila salamu yangu haikuitikiwa na mtu hata moja zaidi ya wao kuniangalia kwa macho makali.Dereva akazidi kutetemeka hadi ikafikia hatua suruali yake ikaanza kulowa akiashiria ameshindwa kuizuia hali ya kujikojolea.Mkojo wa dereva ukaanza kusambaa kwenye baraza uku ukienda kwenye mfumo wa kajimstari na kufika katika sehemu aliyo kaa jijamaa moja jeusi lenye mwili mkubwa na ndevu nyingi kama za masanii maarufu duniani Rick Rose
“Oya jibaba huyo mse***kakukojolea”

Jamaa jengine lilizungumza kwa sauti nzito na ya kuogopesha na kumfanya mwenzake atazame mstari wa mkojo ulio igusa suruali yake iliyo chafuka kisha kamtazama dereva na taratibu jamaa likaanza kunyanyuka na kunifanya nikae kimya huku mapigo ya moyo yakinienda mbio kiasi kwamba ujeri wote ukakata kama umeme wa Tanesco
“Oya unyonye huo mkojo wako”

Jamaa lilizungumza huku likimuinamisha dereva wetu kwa nguvu zake zote na kumfanya aanguke kifudi dudi na mimi nikajibanza kwenye kona ya ukuta nikiaangalia nini kitakacho fwata kwa dereva.
“Usinitazame kwa macho ya kike kike nimekuambia linywe hilo kojo lako”
Jijamaa lilizungumza huku mguu wake mmoja akiuweka mgongoni mwa deeva na kumfanya dereva kuanza kuunyonya mkojo wake uliopo juu ya sakafu inayo onekana ni mpya na haina sikiu nyingi tangu iwekwe
“Nimekuambia fastaa”

Jijamaa likazidi kumuamrisha dereva wetu na kumfanya aongeze kasi ya kuunyonya mkojo wake hadi akaumaliza ndipo jamaa akamruhusu dereva kukaa kando.Jijamaa likanitazama mimi kwa macho makali na mimi nikanyanyuka na kujifanya na mimi ninamtazama kwa macho ya kibabe ila ndani ya moyo wangu unao enda mbio kama saa mpya laiti jamaa akijaribu kunitisha kwa kitendo chochote ninaweza kudondoka na kuzimia kwa woga hapo hapo
“Dogo unaonekana mjanja sana wewe”

Kwa sentensi ya jamaa kidogo mapigo ya moyo yakakaa sawa na kijiubaridi kikapenya kwenye mwili wangu kwani tangu niingizwe ndani ya hichi chumba sikuweza kuihisi hali ya ubaridi
“Yap”
Jamaa likanitazama kwa muda kisha likatafuta sehemu na kukaa hapo ndipo nikapata wazo la haraka haraka la kuzungumza huku nikikaa katika sehemu yangu
“Broo yaani ingekuwa sio polisi hawa kutuwahi ningemalizia kumkata yule mwenye gari kichwa chake kama nilivyo wafanya watoto wake wawili na mkewe”

Maneno yangu kidogo yakawafanya jamaa kunitazama kwa wasiwasi huku wakinitazama kwenye shati langu na kuziona damu zilizo jaa kidogo laiti wangejua ni damu za Manka nahisi wangenibamiza mamgumi mengi
“Alafu ninausongo wa kujito muhanga na bomu bora nife kuliko kwenda jela.Hivi ule mfuko wa mabomu uliuficha pale pale ulipo uficha?”
Nilimuuliza dereva swali amabalo naye akabaki anashangaa kwani nahisi ananiona kama nimechanganyikiwa ila lengo langu ni kujitengenezea hofu ya kuogopwa na mijamaa kwa maana bila ya kufanya hivyo usiku kwetu utakuwa mbaya na mrefu japo kwa dereva ulishaanza kuharibika.Nikamkonyeza kwa haraka dereva akatingisha kichwa kwa ishara ya kukubali

“Tatizo lako wewe muoga ndio maana ukashindwa kuyachukua yale mabomo sasa kwa mfano polisi wakiyashika itakuwaje?Na huo uoga uoga wako ndio umekufanya umekunywa mikojo yako laiti ingekuwa ni mimi ningehakikisha asubuhi haifiki chumba kizima kimetapakaa damu”
Mijamaa ikanitazama huku ikionekana kuwa na wasiwasi huku nahisi kila mmoja ananifikiria kivyake.Nikaanza kujipapasa kwenye mifuko yangu huku nikijifanya ninatafuta kitu ambacho sikujua ni nini

“Kile kisu hao jamaa wamekichukua?”
“Ita..akuwa”
“Ingekuwa sio hivyo ningeondoka na roho ya mtu”
Jijamaa moja likavunja ukimya wao huku likijikoholesha koholesha na kunifanya nikae kimya kumsikiliza anataka kusema kitu gani
“Oya daogo umeshatoa roho za watu wangapi hadi sasa hivi?”
“Daaa wengi sana kama kwenye tisini na nane au tisini na tisa”
“Ahaa utaonaje wewe ukamalizia list hiyo na ukawa wa mia moja”
“Mmmm……?”
“Usigune kwa maana tangu uiingie humu ndani una kazi ya kuropoka ropoka tuu oohhoo sijui nijitoe muhanga ohhooo nitamwaga damu.Jinsi unavyo tuona sisi humu ndani ni waauji na nimajambazi sugu tena sana kama unajipenda funga domo lako tuna mawazo yetu sawa?”

Jamaa alizungumza na kunifanya nikaae kimya bila kuzungumza kitu cha aina yoyote huku nikimuomba Mungu asaidie asubuhi ifike mapema ili jamaa wasije wakanifanyia kitu cha aina yoyote.Asubuhi na mapema akaja askari huku akiwa ameongozana na mwanamke mmoja aliye valia suti na nikajua moja kwa moja nikajua atakuwa ameagizwa na mama kujua kutuoa
“Ni wapi hao unao watafuta kati ya hao watu humo ndani?”

Askari alimuuliza mwanamke yule na akaanza kutuangalia mmoja baada ya mwengine na mwisho wa siku akatingisha kichwa kuashiria hayupo mtu anaye mtafuta kati yetu nikajikuta machozi yakianza kunilenga lenga huku nikimtazama mwanamke aliye simama nje ya ya mlango wa nondo.Mwanamke akaondoka na kumuacha askaria akisimama na kututizama kisha akaanza kucheka
“Dogo bado upo eheeee”
Askari akazidi kucheka huku akininyooshea kirugu chake na kuanza kukipiga piga kwenye nondo za mlango wa chumba hicho

“Oyaaa wewe fala unatupigia kelele”
Jijamaa limoja lilizungumza kwa sauti ya kukwaruza kwaruza huku likimnyooshe askari kidole
“Nyamaza wewe subirini hukumu yenu ya kunyongwa”
“Afande hadi sisi!?”
Nilimuuliza askari kwa mshangao na kuyafanya machozi yaanze kunimwagika
“Tena nyinyi ndio mutakuwa wa kwanza na hiyo minjemba mine itafwatia”

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)